Kuchapisha pesa noti kuhudumia mkopo au baadhi ya shughuli kuna sababisha matatizo mengi kuliko suluhisho.
Ujerumani ikijiita Weimar republic waliprint noti nyingi mwaka 1922 kilichotokea ni mfumuko wa bei uliopitiliza(hyper inflation)
Ujerumani ilikuwa na deni kubwa baada ya kushindwa vita vya kwanza vya dunia, njia waliyotumia ni hii ya kuchapisha noti nyingi.
Pesa ikawa nyingi kwenye mzunguko kuliko kile ambacho nchi inaweza kuzalisha.
Mfumuko wa bei ukaibuka na kusababisha thamani ya tharafu yao kushuka thamani, na matokeo yake kushindwa kulipa deni kabisa.
Ukiangalia huo mfano unaweza kuona madhara ya kuchapisha noti nyingi.
Kikawaida kiwango cha noti kinachotolewa kinatakiwa kiendane na level ya uzalishaji wa bidhaa na huduma.
Ili kuelewa zaidi tuchukulie mfano wa muonyesha banda la video.
Uwezo wa banda la video ni kuingiza watu hamsini.
Kwa hiyo mwenye banda la video(mtengeneza noti) atatengeneza tiketi(noti) 50 kila tiketi iwe sh 2.
Kama mwenye banda la video akawa ana uhitaji sh 108, akaamua azalishe 54 kinachofuata hizi tiketi zitapanda bei kwa sababu siti ziko hamsini tu.
Sasa kama kuna mtu mwingine naye anaonyesha video wateja wanaweza kuhamia huko kwa sababu bei ni ya chini. Huyu mwingine atashindwa hata kuipata hiyo 108.
Kwa hiyo hapo njia nzuri ni kuwakopa wale baadhi walionunua tiketi 50, kwa sababu kuna wengine hawatoangalia movie wakati huo kwa hiyo utazikopa zile tiketi mfano 4 (mfano saving au kuuza dhamana za serikali,bond nk) na kuziuza kwa wengine ama kuzifanyia shughuri nyingine.
Ndio maana serikali inapokuwa na uhitaji wa kiasi cha pesa cha ziada na kodi ikawa haitoshi, hukopa kwa kwa kuuza treasury bill, treasury bonds nk au kukopa nje ya nchi kuliko kuchapisha noti mpya kwa sababu uchapishaji wa noti mpya haiongezi uzalishaji bali inaongeza pesa kwenye mzunguko.
Nadhani wenye uelewa zaidi watakufafanulia.
Baadhi ya link unazoweza pitia.
National debt of the United States - Wikipedia
Why do governments borrow money instead of printing it? - Quora
Hyperinflation in the Weimar Republic - Wikipedia
The problem with printing money - Economics Help
Mishahara itapandishwa mkuu, posho zitakuwa nyingi, masharti ya kukopa bank yatapunguzwa, kutakuwa na unafuu kwenye ulipaji kodi n.kSWALI LA KIJINGA
Je pesa inakuwaje nyingi mtaani kama mshahara unaolipwa ni uleule, au hata ukifanya kibarua pesa unayolipwa ni ileile,?
Sent using Jamii Forums mobile app
"Kwanini Serekali inakopa kama inaweza ku-print noti mpya"Mbona swali lilikuwa wazi sana, je inaprint hela kama mbadala wa kukopa pesa au huwa haiprint? Jaribu kujikita kwenye swali
Wabongo bwana daah! Hivi waziri anaweza toa amri ela zika printiwa?Kuna waziri sijui wa zambia au Zimbabwe, aliamka zake akasema watu wanalia maisha magum hamna pesa, wakaagiza pesa kibao ziwe printed zikaletwa nchini duh ikaharibu uchumi wao completely, kwenye principles of money mojawapo ni it should be scarce, yani pesa isiwe nyingi kwenye mzunguko maana ukiprint mihela mingi currency yako itashuka thamani ndio ka zimbabwe unaenda nunua mkate na bunda la pesa.. it's a very huge aspect this is the real world vitu haviwi solved kirahisi hivyo kijana
Sent using Jamii Forums mobile app
Exactly, nilitaka uondoe ile presumption inayojengeka kwamba hawaprint pesa kama namna moja wapo ya kukopa, pia nilitaka ufahamu kwamba hata kuchapisha pesa ni kukopa pia, means unawakopa wananchi wako, na usipowalipa in time basi bidhaa hupanda bei as a means of balancing the accounts"Kwanini Serekali inakopa kama inaweza ku-print noti mpya"
Swali lipo hivi mkuu, yaani kwa mfano kama huu. Sasa hivi serikali inajenga reli ya SGR kwa mkopo, ni kwanini basi tusiprint note mpya ili tujenge SGR kwa hela zetu hizo mpya badala yake tumeenda kukopa?
Kiuchumi kukopa kuna faida zaidi kuliko kuprint note mpya ila sometimes huwa wanaprint ila kwa taadhari kubwa sana na pia kutegemeana na sera za nchi kwa wakati huo.
So kuprint wanaprint ila lazima kufanywe kwa tahadhari kubwa sana otherwise uchumi utaanguka vibaya sana.
Yes uko sahihi mkuuWala sio demand na supply..
Asome briefly concept ya monetary policy,money supply and interest rate...
Pesa sio yale makaratasi,Nithamani.Ndio maana sio lazima ulipwe cash,unaweza lipwa kwa checki,kwa bank trnasfer kwa mobile money etc kwa sababu ya value.So kwa lugha nyingine serikali hata ikichapa note lazima value iwe created ili kuwe na exchange.Habari zenu. Wanauchumi na wadau wengine wote humu ndani..
Naleta mada hii kwa misingi ya kutaka kuelewa, kama nchi inaweza Ku print noti mpya. Kwanini inakopa pesa?
Kwanini ina madeni kama uwezo wa kuyalipa na pesa mpya ipo
Kwa wenye uelewa. Tusaidiane tafadhali.
Mnisaidie concept ya "inflation" piaView attachment 1400170
Sent using Jamii Forums mobile app
Hao hao wanaomponda ni zero kichwani , hata wao hawajui wamjibu nin wamebaki kukariri Tu madesa ya demand and supply ,Jamani, mtu anaomba kujizwa na ameonyesha kutokua na uelewa na ameuliza maswali ya msingi badala mumjibu munamcrash. Bragging eti nyie ndo wachumi. Aisee. Pole kaka. Bila shaka majibu umeshayapata.
Sent using Jamii Forums mobile app
Asanteni wachache mliojaribu kumjibu, swali zuri la uelewa ila anajibiwa kihuni.
Subiri ukikua utajua bado ungali mtoto.
Jamani, mtu anaomba kujizwa na ameonyesha kutokua na uelewa na ameuliza maswali ya msingi badala mumjibu munamcrash. Bragging eti nyie ndo wachumi. Aisee. Pole kaka. Bila shaka majibu umeshayapata.
Sent using Jamii Forums mobile app
Nakupa msaada kidgo ti,ila uende ukachimbue zaid:
Serikali yoyote,huwa na central bank yake ambayo inasimamia maswala ya fedha na kuhakikisha mzunguko wa pesa inakuwa vyema.
Katika uchumi,tuna sera kadhaa ambazo zinazungumzia uchumi wa taifa kwa ujumla na uchumi wa mtu mmoja mmoja,yaan aggregate economy and individual economy.
Aggregate demand ndio inahusika na mada yako.
Na hapo utasoma sera tofauto ambazo zinaelezea uchumi wa nchi unavyoendeshwa.
Kwa uchache,kuna sera ya monetary policy,ambayo yenyewe inazungumzia suala la usambazaji wa pesa na interest rate.
Hapa utaona namna ambavyo central banks,inavyopunguza bonds notes,na kuongeza interest rates ili ku control inflation katika taifa.
Naomba niishie hapo ila naomba utafute vitabu vya uchumi usome aggregate demand,macro economics.itakusaidia kukupa elimu zaid.
Siku zijazo nitafundisha somo la uchumi.
Lakin hadi jf watoe fulsa yakuwanyanyua watu wanaotoa mada hapa..atleast rewards,kuliko kupoteza mda bure.
Daah haya ngoja niweke neno. Kusema serikali haichapishi pesa si kweli, serikali huwa inachapisha pesa kama njia moja wapo ya kuwakopa wananchi wake (pesa kama pesa yenyewe ni worthless kama haiwi backed by goods na services zinazozalishwa au zilizopo)
Yaani serikali inapokosa fedha lets say ya mishahara, basi inaweza ikachapisha kiasi (limited amount) ili kulipa hiyo mishahara, ila hii inabidi ifanyike kwa kiasi kidogo sana ili kuepusha kushuka kwa thamani ya pesa (over inflation) ambapo utakuta mkate unapanda toka 1,000/= hadi 10,000/= pengine,
Hivyo pesa inaweza ikakosa thamani katika manunuzi na ikawa sawa na toilet paper tu. Sasa njia nyingine ya kukopa ndio hiyo ya mabenki ya kibiashara, mikopo toka mataifa rafiki na mashirika ya maendeleo kwa masharti/ riba maalum.
Na ukitaka kuamini serikali huwa inawakopa wananchi wake kwa kuchapisha pesa jiulize kwanini soda ilikuwa inauzwa 150/= ila leo inauzwa 500/=, means imewakopa wananchi na haijawalipa bado, otherwise soda ilipaswa iuzwe bei ile ile ya 150/=
Ukiona hivyo wao wenyewe walikariri hawakuelewa ndio maana hawatoi jibu direct.Badala ya kumjibu mnazidi kumchanganya,hajui kuhus Uchumi ndio maana kauliza, waswaili bwana!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app