robby one fashion
New Member
- Aug 25, 2014
- 4
- 20
Na Bikira konk
1. Miaka mingi iliyopita nilialikwa kwenye "listening party" ya wimbo na video ya "My Favorite Artist Wangu Of All Times Lady Jay Dee. "Listening party au watch party" ni "closed event" ambayo watu wachache wanaalikwa kusikiliza wimbo au kuona video inayotarajia kutoka kabla wengine wote hawajaiona au kusikia ili kutoa mawazo yao au kuwa "champions" wa ule wimbo au video.
2. Miaka michache iliyopita kwa kushirikiana na rafiki yangu Dada Mary Mgurusi tuliandaa na kualika watu wachache katika "watch party" ya sinema yetu iliyoitwa Tatu Chafu chini ya BongoHoodz kabla hatujaionyesha rasmi ile sinema kwa watu wote. Baadhi ya "maoni" ya wale waalikwa yalitumika kuboresha sinema kabla haijatoka.
3. Miaka michache iliyopita nikiwa mjumbe wa TRA Stakeholders Forum nilialikwa kujadili baadhi ya sheria za kodi ili kupata maoni ya sisi wadau "wawakilishi wa sekta binafsi" kabla rasimu hiyo haijapelekwa katika vyombo husika. Moja ya "ajenda" ilikuwa ni "wazo" la kupata mapato ya kodi kupitia biashara za kimtandao au "online businesses"
Wapo wanaoamini kuwa hakuna mtu anatakiwa kujua wazo lako au mpango wako au bidhaa yako au "ajenda" yako kabla haijatoka au kabla haujaanza kuuza bidhaa husika sokoni kwa sababu watu watakuibia wazo lako au watakufanyia fitina na majungu au wata ku"discourage" ili usifanikiwe [kosa kubwa].
Japo ni vizuri kulinda "wazo" lako lakini ukweli ni kwamba unaweza ukawa unapeleka sokoni "the wrong thing" au kitu kisichokubalika au kisichouzika. Kwa lugha ya kitaalam tunaita "product market unfit".Kimsingi, kabla hujafungua au kusajili kampuni au kufanyia kazi wazo lako unatakiwa kupata "product market fit".
Sababu ya Lady Jay Dee kuandaa "listening na watch party" ya wimbo wake ni kuangalia "product market fit". Sababu ya BongoHoodz kuandaa "watch party" ni kuangalia "product market fit" na sababu ya TRA kuandaa "stakeholders" forum ni kuangalia "product market fit"
75% ya biashara nyingi mpya zinakufa ndani ya miaka 3 kwa kukosa "product market fit". Nyingine baada ya kuingia sokoni zinagundua "bidhaa waliyotengeneza" haihitajiki au haina "product market fit" na inabidi wabadili "bidhaa" hiyo watengeneze bidhaa yenye "product market fit".
Mfano mzuri ni kilichoitokea kampuni ya Colgate. Kampuni ya Colgate haikuanza kwa kutengeneza dawa ya meno. Ilianza kwa kutengeneza sabuni. Wakagundua hakuna "product market fit. Ikabidi wabadili mwelekeo kuokoa jahazi "pivot".
Changamoto ya kutengeneza bidhaa au kufanyia kazi wazo lako pasipo kujua kama ndilo ilnahitajika sokoni ni kwamba uwezo wa kupoteza hela na nguvu zako na muda wako ni mkubwa sana. Ndio sababu unapokuwa na wazo lako na unataka kuingia sokoni usiogope kuibiwa.
Lisajili ili uweze kulijaribu "test and validate" sokoni kabla haujafungua au kusajili kampuni. Kama ni kampuni kongwe basi lijaribu hilo wazo au bidhaa kabla hujatengeneza "full product" Vinginevyo utaongeza takwimu ya 75% ya biashara mpya na "bidhaa" mpya kufa ndani ya miaka 3.
Ndicho nilichokifanya kabla ya kutengeneza www.paulmashauri.com. Kutengeneza "coaching platform" ya namna hii peke yake bila gharama za uendeshaji ni uwekezaji usiopungua shilingi milioni 32 mwanzo mwisho.
Hapo hujaanza kuuza ni kujenga "platform tu". Unahitaji watu wa "data entry", watu wa kutafsiri au "translations", " site security", "payment gateways", "assessment tools", "software intergrations" nk. Ndio sababu hata mimi sikuanza kwa kujenga "platform". Nilianza kwa kuandika makala na kuomba watu wa "subscribe".
Hii "methodology" inaitwa "Lean start Up". Ni muunganiko wa "Lean Methodology na Agile Product Development". Lengo lilikuwa ni kuangalia "product market fit". Kwa lugha nyingine "idea au product validation". Nilitaka kabla sijatumia fedha nyingi, nijue na nithibitishe; je kuna mtu yuko tayari kulipia "product' kama hii?
Na je soko ni kubwa kiasi gani kwa mimi kufikia "break even point"? yaani mapato yazidi uwekezaji? Na mwisho itachukua muda gani kufikia "break even point"? Mara tu nilipopata "subscribers" zaidi ya 1,000 walio tayari kulipia kabla ya "launch" nikathibitisha "product market fit".
Ndivyo makampuni makubwa ya Real Estate na Property Development" yanavyofanya biashara. Wanapokuwa tayari wameandaa "architectural plan" au "blue print" namna jengo au nyumba zitakavyokuwa, wanaanza kuuza "space" kabla hata ya jengo kuanza kujengwa.
Usiwaite "matapeli" au usifikiri kwamba "wanauza" space kabla hawajajenga illi wapate mtaji. Hapana! Uwekezaji katika "Real estate" ni wa muda mrefu na hautegemei kabisa mauzo ya awali "advance payments". Sasa kwanini waanze kuuza wakati hawajajenga bado? Wanatafuta "product market fit". Je kuna mteja yuko tayari kulipia?
Hata katika siasa. Lengo la kutangaza nia ni kuangalia "product market fit". kama ulipotangaza nia tu watu wakaandamana kukupinga kwanini unaendelea kupoteza nguvu zako, muda wako na fedha zako? Tayari hiyo ni "product market unfit. Lakini kama ulipotangaza nia tu wananchi wenyewe bila shuruti wakaanza kuchanga na fedha kukupa "support" kuna "product market fit". Ndicho kilichomtokea Barack Obama.
Haijalishi unafanya nini; unasuka, unapika chakula, unapiga mziki, unaimba, unatengeneza "software", una biashara ya magari, biashara ya "real estate", biashara ya mafuta nk kama huna "mteja aliye tayari kulipa" huna "biashara". Usijidanganye "eti" kwa sababu "wewe mwenyewe unaona "idea" yako ni nzuri basi kila mtu anaona hivyo hivyo". Sio kweli.
Ndio maana ukiwauliza wanamuziki wote watakuambia nyimbo ambayo ili "hit" sio nyimbo ambayo walitegemea kuwa ni "hit". Kwa sababu mawazo yao sio mawazo ya wateja. Kwahiyo usitegemee "bahati nasibu" kwenye jambo lako. Lazima ufanye "scientific experimentation" kuthibitisha kwamba wazo lako ni "product market fit"
Kuna namna nyingi za kufanya hivyo ndio maana tukatengeneza The Start Up Academy. The Start Up Academy sio tu kwa wale wanaoanza biashara. Hata kwa makampuni makubwa yanayotengeneza "product" mpya kila siku. Nao pia ni "start ups" kwa sababu "product mpya" inaweza ikawa ni "market unfit" bila kujali uko sokoni miaka mingapi.
Mfano mzuri ni "Business Times" na "IPP Media". Walikuwa sokoni miaka mingi lakini waliyafunga magazeti ya "ALASIRI" na "DAR LEO" kwa sababu yalikosa "product market fit". Yalikosaje? Hayakuwa tena "breaking news" baada ya "blogs" hasa Michuzi Blog kuingia sokoni.
Kwanini mtu asubiri kutoa pesa yake kununua "DAR LEO" au "ALASIRI" la saa 9 mchana kupata habari ya saa nne asubuhi wakati "blogs", "Facebook" na " You Tube" wamesha post habari hiyo hiyo tena bure kabisa muda huo huo wa saa nne tukio lilipotokea?