Kwanini replacements zote ni UDSM?

Kila anayetumbuliwa, mbadala wake utatoka chuo kikuu Dar Es Salaam, kuna nini jamani?
wanaofanya vetting awamu hii wameona kitu gani chuoni hapo?
Kuna hasara ya idara kupata misukosuko maana wengi ya wateule ni watu very seniors kwa maana ya levels za taaluma, mwenye PhD akitolewa kuna kazi kuumba mwingine, siku zote tumekuwa na idadi ndogo za wafanyakazi wa umma na vyuo vikuu navyo vinaumia kama idara nyingine za umma. kwa awamu hii nadhani Zaidi ya watu 10 wameshateuliwa kwa nafasi mbalimbali! sijui itakuwaje hadi majipu yote yakiisha, tutaanza kuumba tena wakufunzi wabobezi wapya!
mamlaka za uteuzi naomba zizingatia majukumu ya hawa watu na uhitaji wa chuo, sio kuwanyang'anya tu UDSM, chuo kita-suffer!
Sio mbaya akifanya hivyo, kumbuka udsm ni chuo kongwe hivyo kimetoa wataalamu wengi zaidi kuliko vyuo vingne kwa level ya phd. Udom imeanza kutoa phd nadhani 2010+ kwa level ya phd.
 
Sio mbaya akifanya hivyo, kumbuka udsm ni chuo kongwe hivyo kimetoa wataalamu wengi zaidi kuliko vyuo vingne kwa level ya phd. Udom imeanza kutoa phd nadhani 2010+ kwa level ya phd.
Kuna Chuo gani zaidi ya UDSM
 
Hicho ndio chuo kikuu cha Taifa,vingine ni vyuo vya serikali sasa kulijenga Taifa lazma uwatumie wana chuo.wa Taifa
hivi ni product za hii hii udsm zilizotufikisha hapa tulipo au kuna udsm nyingine.?
UDSM ni zaidi ya chuo, ndio engine ya Tanzania bahati mbaya mfumuko wa vyuo nchini unalifanya hili lisionekane. Kiukweli pale it's a Home of intellectuals sasa sijui angeenda wapi zaidi ya UD kuwapata hao intellectuals .

UDSM NDIO CHUO KIKUU NA KINA VICHWA BALAA..HUWEZI KUKIFANANISHA NA CHOCHOTE HAPA TZ HATA EAST AFRICA
 
Acheni kubwabwaja nyie watoto mwaka jana JPM kmteua Prof Mahalu wa CUHAS-BUGANDO kua mwenyekiti wa board ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute pia Prof Mtabaji wa hapohapo Bugando kua mwenyekiti wa board ya TCU, wameshateuliwa pia mafundi kibao kutoka MUHAS lakini vijana hawakuja majukwaani kupiga makelele , hebu punguzeni ushabiki nyie watoto wa UD, huu muda mgeutumia kufanya mambo ya maana ingependeza sio kushinda JF mnabishana na sisi wa SAUT-Songea.
 
Umaskini wa watanzania ni wa wasomi wa UDSM kwani pamoja Na usomi wao wameshindwa kuikwamua nchi hii badala yake wanazidi kupewa nyadhifa ndani ya serikali
 
Ndio watu wenye uelewa sana na hata alama za wanaopangiwa pale si kama za vyuo vingine vile vya kata... asilimia 90 ya viongozi wote wa umma wamemalza pale
Kumbe tunaangalia alama!!! No wonder tupo hapa tulipo.
 
Binafsi nadhani tumeenda kidogo nje ya mada....
Nadhan mtoa mada alikuwa na swali lenye maslahi makubwa kwa chuo kikuu cha Udsm... Kwani no hatari sana kuondoa wasomi wengi kwa mkupuo!....
Natambua sana mchango was chuo kikuu cha Dar es Salaam, lakini so lecturers wote wanaofundisha pale wamesomea pale, lakini pia sio kila zao la Udsm no zao jema ndio maana hata hao wanaotenguliwa pia no zao la Udsm kwa idadi kubwa!...
Hata humu pia kuna watu wanapochangia mada jnanifanya kusikia aibu kama kweli chuo kikuu mahiri kama Udsm kinaweza kutoa makapi kama hayo.....
Eti mtu anasema hata waajiri hawataki watu was vyuo vingine, hahahahahahaha! Kumbe kwa uelewa was huyu jamaa anadhani tatizo la ukosefu was ajira haliwahusu wale wanaotoka Udsm?!
Fikra finyu sana, bado naamini Udsm no chuo bora hata kama mtu kama huyu amemaliza chuo hicho....
 
Kila anayetumbuliwa, mbadala wake utatoka chuo kikuu Dar Es Salaam, kuna nini jamani?
wanaofanya vetting awamu hii wameona kitu gani chuoni hapo?

Kuna hasara ya idara kupata misukosuko maana wengi ya wateule ni watu very seniors kwa maana ya levels za taaluma, mwenye PhD akitolewa kuna kazi kuumba mwingine, siku zote tumekuwa na idadi ndogo za wafanyakazi wa umma na vyuo vikuu navyo vinaumia kama idara nyingine za umma. Kwa awamu hii nadhani zaidi ya watu 10 wameshateuliwa kwa nafasi mbalimbali! sijui itakuwaje hadi majipu yote yakiisha, tutaanza kuumba tena wakufunzi wabobezi wapya!

Mamlaka za uteuzi naomba zizingatia majukumu ya hawa watu na uhitaji wa chuo, sio kuwanyang'anya tu UDSM, chuo kita-suffer!
Jamani sio UDSM peke yake hata SUA. Naelewa Mh. Rais ana nia nzuri sana kwa kuwa tukubali tusikubali wenzetu hawa waliosoma PhD uelewa wao huwa ni wa juu. Si rahisi kama mtu hana uelewa wa juu kusoma PhD. hivyo Mkuu anaona kuwa ni rahisi kufanya nao kazi.Lakini ni ukewli usipingika kuwa Vyuo navyo vitakosa Wahadhiri waliobobea, wenye uzoefu. Niliongea na Prof. mmoja, Chuo sitakitaja ananiambia kuna wanaoteuleiwa kutoka Chuoni kwao wamebobea kisasi kwamba uili kumpata Prof. aliyebobea kama huyo aliyeteuliwa bais atoke university of nairobi au Zambia or so! Hivyo Mkuu awe makini katyika teuzi otherwise vijana wajao watakosa lecturers ( wenye ujuzi na uzoefu) wa kuwafundisha. Aidha pesa za kuwajengea uwezo wahadhiri zitengwe kwani imeonekana sasa umuhimu wao ( licha ya kutakiwa Vyuoni) wanatakiwa pia kwenye uongozi wa serekali!
 
Binafsi nadhani tumeenda kidogo nje ya mada....
Nadhan mtoa mada alikuwa na swali lenye maslahi makubwa kwa chuo kikuu cha Udsm... Kwani no hatari sana kuondoa wasomi wengi kwa mkupuo!....
Natambua sana mchango was chuo kikuu cha Dar es Salaam, lakini so lecturers wote wanaofundisha pale wamesomea pale, lakini pia sio kila zao la Udsm no zao jema ndio maana hata hao wanaotenguliwa pia no zao la Udsm kwa idadi kubwa!...
Hata humu pia kuna watu wanapochangia mada jnanifanya kusikia aibu kama kweli chuo kikuu mahiri kama Udsm kinaweza kutoa makapi kama hayo.....
Eti mtu anasema hata waajiri hawataki watu was vyuo vingine, hahahahahahaha! Kumbe kwa uelewa was huyu jamaa anadhani tatizo la ukosefu was ajira haliwahusu wale wanaotoka Udsm?!
Fikra finyu sana, bado naamini Udsm no chuo bora hata kama mtu kama huyu amemaliza chuo hicho....
Fanya utafiti ndugu yangu kuhusu vyuo vingine ( esp. vya Private) vina matatizo kwa hao wahitimu wake. Kwanza kabisa ni Siri ya wazi kuwa UDSM pamoja na vyuo vya serekali hucukua Cream, nadhani hili unalielewa ukianzia hapo tu jawabu unaweza kulipata. Na Tanzania ingefanya utafiti wa wahitimu kutoka vyuo mbalimbali ili kusaidia hivyo vyuo vingine viweze kujiongeza! Kwani esp. hapo zamani wakati ajira ni kwa vimemo hivyo hata wahitimu wabovu waliweza pata ajira, walisumbua sana viongozi wa idara kwani waliletewa wafanyakazi ambao hata ukimwambia andika simple letter kujibu barua fulani hawezi!
 
Hivi SEKUCO, SJUT, SAUT, SUPUKA, UDOM, THE AMAZON, ST JOSEPH, n.k kuna wasomi huko?

kama wapo mbona wahitimu wao wako shallow, haajiriki na wanatengwa na waajiri?

acha mkuu achukue wabobezi toka chuo kongwe lenye sifa lukuki.
Thinking ya msomi Nguli!
kuajiriwa ni sifa kubwa ya ubora wa chuo!?
wasomi wa chuo kikuu, huwa wanavitu wanagundua, huwa wanavitu wanafanya kuwapa sifa za usomi, sio hizi za kuishi na madesa!
kwa bahati tu wanaotoka UDSM huwa wazuri!
na bahati inajengwa na sifa za ufaulu wa wanafunzi ktk matokeo ya form six, endapo selection isingewa-favour then tungekuwa na picha mbaya mno!
Arusha Tech, DIT, SUA kweli vinasuka watu, yaani mtu anaingia mburula ktk fani na anatoka mtaalam!
UDSM mtu anaingia Mburula ktk fani na anatoka Kasuku ktk fani!
 
Ndio watu wenye uelewa sana na hata alama za wanaopangiwa pale si kama za vyuo vingine vile vya kata... asilimia 90 ya viongozi wote wa umma wamemalza pale
Ni kweli asilimia kubwa ya viongozi wamemalizia pale na wengi wao sasa ni mafisadi.
 
Jaribu kusoma ranks za vyuo vikuu duniani, then utaona vyuo vikuu vingine East Africa vinanafasi ipi! Tazama ranks za Makerere na Nairobi then uje utueleze!
na kukusaidia Zaidi, just google: Best Universities in Africa 2016. maana ukiambiwa tafuta rank ya UDSM ktk list ya dunia unaweza usiione kabisa maana itakuwa imefichwa ndani kabisa!
kwa msomi yeyote East Africa anajua Nairobi na Makerere ni vitu gani!
UDSM NDIO CHUO KIKUU NA KINA VICHWA BALAA..HUWEZI KUKIFANANISHA NA CHOCHOTE HAPA TZ HATA EAST AFRICA
 
Back
Top Bottom