Kwanini Reginald Mengi utumia muda mrefu?

Nunua na wewe kipindi kama alivyofanya wema utaonekana hata saa nzima.
 
Kuna swali umeulizwa mtoa mada humu kwamba mbona wewe mke wako/mume wako huwa unalala nae muda mrefu kuliko majirani zako. Si uwe unawapa kidogo nao?
 
Inategemea anjishughulisha na issues gani,,
Kama anajishughulisha na mambo yanayogusa jamii inayomzunguka moja kwa moja, au kitaifa na kimataifa, lazima ataonekana kwenye tv anapokuwa katika shughuli hizo nilizotaja, na sio katika tv yake tu, ni hata tv zingine. Hapa swala ni habari inayostahili kuonyweshwa, sio mtu anayestahili kuonyweshwa.
 

ulitaka nani aongee muda mrefu?na nyie fungueni yenu acheni majungu,ITV NI MALI YA REGNALD MENGI!!!!!,PERIOD!
 
Anakuwa kalipia air time hata ww ukilipia unaweza kuongea masaa 24
 
ni hatari mtu kutumia chombio chake cha habari kwa manufaa yake binafsi wote mnakumbuka baada ya uchaguzi mkuu wan kwanza wa vyama vingi tanzania kuvurugika alitumia vyombo vyake vya habari kuwatisha wananchi kwa kuonyesha mauaji ya Rwanda kama kila mtu atatumia chombo chake anavyotaka ni rahisi watu wengine kutumia vyombo vyao kuleta machafuko mtoa hoja ana swali la msingi nashangaa mnaomponda
 
mkuu ngoja shemeji yako akifungua tv yake na wewe utakuwa unauza sura
 
Kuna kitu cha kujadili hapa jibu swali sio unajifanya eti hakuna swala la kujadili hapa. eti bakhresa na yeye awe anajiweka kwenye kioo cha Azam TV muda mrefu kama Mengi? hiyo haitawezekana kamwe.
Atajiweka akiwa anakanda unga wa chapati?Mengi ana jitokeza kwa mambo ya kitaifa,ni kiongozi katika sekta mbalimbali.
 

Kwa mtu mwenye akili nzuri hii sio tija sana sana labda tujiulize huwa anazungumza mambo yenye mantiki kwa mtanzania na msikilizaji wake?
 
ni mwenye TV so hamna shida acha atumie vyombo vyake bana
 
Watanzania kwa kubishana kura ya wazi/ siri ilichukua mwezi mzima bungeni.

Hivi Mengi Utamlinganisha na nani kwa Viongozi na Wamiliki wa Vyombo vya Habari vingine kwa kuitumikia Jamii?
Dialo au Bahareza? Tumikia jamii utangazwe kila cku.
 
wote ni muhimu

Mimi nilidhani kuwa rais ndo mtu muhimu wa kuweza kuonyeshwa mda mefu kumbe ni wote. Kama ni hivyo basi matukio ya ajali n.k yangekuwa yanaonyeshwa kwa mda mrefu ili wananchi waelewe vizuri kuliko kuonyesha juu juu tu.
 
ulitaka nani aongee muda mrefu?na nyie fungueni yenu acheni majungu,ITV NI MALI YA REGNALD MENGI!!!!!,PERIOD!
unaongea kirahisi sana lakin linapokuja suala la kumiliki media ni tofauti na kumiliki duka! kama kumbukumbu zangu zipo sawa, nadhan hata sheria au kanuni zinakataza suala hilo coz media ni lazima itoe priority 4 national interest-e.g, n'the same event, huwez mpa JK 2 min, Mengi 5min unless kuna strong reason! mkùu Pasco, njoo utusaidie huku
 
Last edited by a moderator:
Watanzania kwa kubishana kura ya wazi/ siri ilichukua mwezi mzima bungeni.

Hivi Mengi Utamlinganisha na nani kwa Viongozi na Wamiliki wa Vyombo vya Habari vingine kwa kuitumikia Jamii?
Dialo au Bahareza? Tumikia jamii utangazwe kila cku.
ktk hilo, suala la kutangazwa inategemea na intention ya muhusika! kwa mtu anayesaidia jamii ili apate fadhila za mungu hawez hata cku moja akataka kutangazwa lakin ikiwa unataka fadhila za mwanadamu, ndo hivyo tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…