Kwanini Rais Samia ni mzito kuchukua hatua?

Football hooliganisim..kwanini unakuwa termed as such?

Football hooliganism, also known as soccer hooliganism,[1] football rioting or soccer rioting constitutes violence and other destructive behaviours perpetrated by spectators at association football events.[2]

Football hooliganism involves a wide range of behaviour, including:

  • taunting, often with racial slurs, ethnic slurs or hate speech
  • spitting
  • unarmed fighting
  • use of laser pens to disorient players of the opposing team
  • throwing of objects on to the pitch, either in an attempt to harm players, fans and officials or as a gesture of insult.
  • throwing of objects at opposing supporters, including stones, bricks, coins, flares, fireworks and Molotov cocktails.[3][4]
  • fighting with weapons including sports bats, glass bottles, rocks, rebar, knives, machetes and firearms.[6]
  • disorderly crowd behaviour such as pushing, which may cause stadium fixtures such as fences and walls to collapse. Similar effects can occur when law-abiding crowds try to flee disorder caused by hooligans.[7]
  • burning the pitch and placing the emblem of a rival team in the grass.
  • In some places, there is vandalism in the form of graffiti sprayed to promote football teams, especially in derby cities.
  • committing an act of arson
  • promotion of racism or extremist ideologies such as white supremacism, and neo-Nazism.
  • A highly violent and severe hooliganism may considered as an act of terrorism, especially those involving weapons. Violent hooliganism may cause intervention from a riot police or in some countries, the military.
Tony Blair aliulizwa ungependa waingereza wakukumbuke kwa kitu gani haswa!
Akajibu ningependa wanikumbuke kama kiongozi niliye waachia ligi bora na tajir duniani ya mpira wa miguu yaani EPL
Tuseme na Blair nae alikuwa mu uhuni?
Vicente company ana holde masters ya mathematics na ana cheza mpira.
Mifano ni mingi lakini itoshe tu kukwambia una mawanda mafinyu sana ya kuangqlia mambo
Wacheza mpira wanalipa kodi, wana familia, wanawekeza na kutoa ajira, kuna wadau wengi wameajiriwa kwenye mpira kuliko sekta nyingi sana.
 
Tony Blair aliulizwa ungependa waingereza wakukumbuke kwa kitu gani haswa!
Akajibu ningependa wanikumbuke kama kiongozi niliye waachia ligi bora na tajir duniani ya mpira wa miguu yaani EPL
Tuseme na Blair nae alikuwa mu
Yes anashabikia uhuni, why not Blair kwani si binadamu? Wengi wanashabikia uhuni wa mpira, hata mimi
 
Tatizo ni mfumo uliojengwa kwenye siasa za CCM zenye kujali kwanza chama, pili madaraka na tatu kutokupiss-off godfathers...
 
Mdude unataka kurudi kule kwenye awamu ya 5 uanze kuteseka tena? Acha nchi iongozwe kwa mujibu wa sheria na sio maamuzi binafsi ya Rais. Kikatiba Rais wa Tanzania ana nguvu kubwa mno na akisema azitumie hali itakuwa sio hali. Tumwombee Rais Samia aendelee na moyo huu huu wa kuacha mambo yaende kusheria.
 
Naunga mkono hoja
Naona hataki kuonekana mbaya kwa watu kitu ambacho hatofanikiwa
 
Umesikia Bakhresa kafungua mnara?

Najua una allergy na majina ya John
Umekosa hoja unakimbilia udini! Hujui kwamba kuna watu wanaitwa John halafu siyo wa imani yako.
Nicholas Anelka alikuwa muislamu je wajua?
Watu mliozaliwa 2000- kuja juu . Yaani wanyoa viduku na vinjunga mna matatizo sana.
Kina nyerere wangekuwa na akili kama za kwenu leo sijui tungekuwa wapi??
 
Mdini mimi au bibi faiza

Ujaelewa nilichomaanisha
 
Ukiona mtu , Rais anajiingiza kwenye mipira (ambayo ni michezo ya kihuni, football hooliganism) ujue kuwa huyu mtu ni weak in all aspects of leadership anatafuta cheap popularity kutoka low minded people
Hili la mpira liache.

Michezo ni muhimu ndiyo maana tuna wizara ya michezo.

Ongelea mambo mengine ya msingi bila kugusa furaha za watu, utaeleweka tu!
 
𝑴𝑮𝑶𝑴𝑶 𝑾𝑨 𝑲𝑨𝑹𝑰𝑨𝑲𝑶𝑶 𝑵𝑰 𝑴𝑨𝑻𝑶𝑲𝑬𝑶 𝒀𝑨 𝑼𝑲𝑰𝑴𝒀𝑨 𝑾𝑨 𝑹𝑨𝑰𝑺.

Ni miaka miwili imepita tangu Samia aapishwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika miaka yake miwili tumeshuhudia Rais akiwa mzito wa kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi na viongozi wasiokuwa waaminifu kwa Jamhuri ya Muungano. Sijui ni kigugumizi gani au uwezo wake wa kiutendaji umewekwa kwenye koma/ICU na wala nchi?

Kuna mambo mengi sana Rais yuko kimya na kwa uchache ngoja nizungumzie mambo matatu ambayo ni Mauwaji mikononi mwa polisi, Tozo na mfumuko wa bei pamoja na ufisadi.

1. 𝐌𝐀𝐔𝐖𝐀𝐉𝐈/𝐔𝐓𝐄𝐊𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐈𝐊𝐎𝐍𝐎𝐍𝐈 𝐌𝐖𝐀 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈.

Kumekuwa na mwendelezo wa utekaji pamoja na mauwaji ya watuhumiwa katika vituo vya polisi. Baada ya Rais Samia kuchukua ofisi pale ikulu Machi 2021 watu wengi waliamini kwamba ule ulikuwa mwisho wa watu kutekwa, kuteswa na kuuwawa. Lakini baada ya muda mambo ya mauwaji na utekaji yalijirudia. Tena safari hii wahanga wakubwa wakiwa raia wa kawaida na si wakosoaji wa serikali kama enzi za Magufuli. Wakati mwingine nawaza kwamba huenda Rais Samia kubadilisha viongozi na wakuu wa vyombo vya dola kulilenga kusuka safu yake mpya ya uongozi na sio kukomesha mauwaji na utekaji unaofanywa na baadhi ya watumishi vyombo vya dola.

Tulishuhudia vijana watano wafanyabiashara wa Kariakoo wakikamatwa na watu waliodaiwa kuwa ni polisi kisha wakapelekwa kusikojulikana. Hata ndugu zao walipoenda polisi kujua hatima majibu waliyopewa yaliwashitua kwani polisi walikana kuhusika kuwashikilia. Ni mwaka mmoja na miezi sasa hawa vijana hawajapatikana. Pamoja na kelele tulizopiga mitandaoni, kelele za ndugu pamoja na vyombo vya habari hazijasaidia kuwarudisha vijana hao. Rais ambaye ndiye amiri jeshi mkuu na moja ya majukumu yake ni kuhakikisha raia wake wako salama hajawajibika na wala hajamwajibisha yoyote sio waziri au IGP ni kama vile kuku zimepotea. Amekaa kimya kana kwamba hausiki au hawajibiki na usalama wa raia.

Sio hao tu orodha ya watu kutekwa na wengine kufia vituo vya polisi iliendelea kila kona ya nchi. Mauwaji ya raia Mtwara baada ya kelele nyingi kwa mbaaali angarau akamwagiza waziri mkuu aunde tume ambayo mpaka leo ni mwaka hakuna ripoti ya hiyo tume. Sijui tatizo ni yeye au waziri mkuu?

Baada ya kuona ripoti ya tume mauwaji ya Mtwara imefungiwa maandazi kashfa za watu kufia vituo vya polisi ziliendelea huku polisi wakisingizia watuhumiwa hujinyonga wenyewe. Ilifika mahali polisi walidai wengine walijinyonga kwa kutumia chupi lakini bado Rais Samia kakaa kimya. Orodha ya watu waliofia vituo vya polisi na wengine kutekwa na polisi kwa upande wangu peke yangu nimepokea majina 20 ndani ya miaka miwili ya Samia. Juhudi zetu pamoja na kelele za kutaka hatua kuchukuliwa haijazaa matunda kana kwamba najiuliza hivi kweli tuna Rais au tumeweka shati golini?

2.𝐓𝐎𝐙𝐎 𝐍𝐀 𝐌𝐅𝐔𝐌𝐔𝐊𝐎 𝐖𝐀 𝐁𝐄𝐈.

Tumeshuhudia baada ya Rais Samia kuapishwa kwa haraka alifanya mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri japokuwa mawaziri wengi alirithi kutoka kwa mtangulizi wake akiwemo waziri mkuu. Watu walianza kuwa na matumaini kwamba huenda angepunguza ukata wa maisha ulioletwa na mtangulizi wake lakini mambo hayakuwa hivyo.

Siku 40 za mwanzo tu serikali ya Samia ilipandisha gharama za vifurushi vya internet DATA mara mbili kuliko ilivyokuwa awali. Shilingi elfu moja ambayo ilikuwa na uwezo wa kununua GB moja ya internet sasa ikawa inanunua MB 400 tu. Wananchi wakaanza kulalamika kelele zikawa nyingi lakini ndio kwanza Rais alikausha kimya kana kwamba haishi Tanzania na malalamiko hayaoni. Waziri wake sijui anaitwa Nape anajibu kwa kiburi kwamba kama vifurushi ni gharama zimeni data na Rais yupo kimya tu.

Wakati kidonda cha kupanda kwa data kikiendelea kuuma likafuata pigo lingine la tozo kwenye miamala ya simu na bank. Unatumiwa buku 5 unatoa buku 3 buku 2 imeishia kwenye makato achilia mbali aliyekutumia naye kukatwa tozo. Katikati ya kilio cha tozo likapigwa kombola lingine la mfumuko wa bei. Gharama za maisha zikaongezeka vilio vya machinga na wakulima bei za mbolea lakini bado Rais akaendelea kukaa kimya kana kwamba hahusiki na wala hawajibiki na chochote. Hata akiongea basi naye analalamika kama sisi mpaka najiuliza pale ikulu tuna Rais kweli au tumeweka shati golini?

3. 𝐔𝐅𝐈𝐒𝐀𝐃𝐈

Wengi waliamini kwamba pengine serikali ya Rais Samia kuongeza tozo na kodi mbalimbali kwa wananchi alikuwa analenga kupunguza deni la taifa kama ambavyo Rais Mkapa alifanya katika utawala wake kwa kutokukopa na kupunguza deni la Rais Mwinyi. Takwimu za deni la taifa zikatushitua. Rais Magufuli ndio alishikilia rekodi ya Rais aliyekopa pesa nyingi kwa kipindi cha miaka mitano kuliko watangulizi wake. Lakini rekodi hiyo ilivunjwa na Rais Samia kwa mwaka mmoja tu. Yani pesa ambayo Rais Magufuli aliikopa kwa miaka mitano Samia kaikopa kwa mwaka na wakati huo hata matumizi ya mikopo hiyo hayaeleweki .

Wakati tumepigwa butwaa tukijiuliza imekuwaje mara anaibuka mkaguzi mkuu na mdhibiti wa hesabu za serikali CAG anatusanua namna ambayo watumishi wa umma na viongozi wa serikali walivyovuja pesa za umma. Wengi wakaamini kwamba Rais angechukua hatua kwa ripoti ile lakini hakuchukua hatua yoyote zaidi ya kuwataka wezi hao kula urefu wa kamba zao.

Mwaka mmoja baadaye inatoka ripoti nyingine ya CAG ikionyesha uvujaji na wizi mkubwa wa pesa za umma kukiwa na zaidi ya trillion 2 zilizoibiwa. Hapa Rais angarau alichukua hatua kidogo kwa kuwatukana wezi stupid lakini hakuwawajibisha kwa kuwafukuza kazi au kuwasimamisha ama kuwapeleka mahakamani.

Mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo ni matokeo ya ukimya wa Rais. Kushindwa kusikiliza, kutafuta majawabu na kuchukua hatua ni mambo yaliyopelea mgomo huu. Baada ya kikao cha waziri mkuu na uongozi wa wafanyabiashara wa Kariakoo siku ya jumatatu kushindwa kuzaa matunda na mgomo kuendelea siku iliyofuata, nilitegemea Rais angechukua point 3 kwa kwenda kuwasikiliza mwenyewe na kuchukua hatua. Lakini kama kawaida yake kakaa kimya. Pengine hajui madhara yake. Kuna siku mgomo hautakuwa wa Kariakoo pekee bali utakuwa mgomo wa nchi nzima utakaozalisha maandamano yanayoweza kuangusha serikali yake.

Vipi Rais Samia angeibuka mwenyewe pale MnaziMmoja kusikiliza kero za wafanyabiashara wa Kariakoo zilizopelekea wao kugoma kufungua maduka? Halafu baada ya mkutano avunje bodi ya TRA, afukuze waziri na kamishina wa TRA. Ingempandisha chati kiasi gani? Angepata sifa kiasi gani? Tukio hilo lingerudisha nidhamu kwa viongozi na watumishi wa umma kiasi gani?

Shida ya Samia nini kutochukua hatua?

𝑴𝒅𝒖𝒅𝒆 𝑵𝒚𝒂𝒈𝒂𝒍𝒊 𝟕 𝒙 𝟕𝟎 𝑺𝒖𝒎𝒖 𝒚𝒂 𝑵𝒚𝒊𝒈𝒖.

View attachment 2626057
Remote ipo Msoga. Huelewi mzee. Mpaka baba ridhi atie neno ndo maamuzi yatoke
 
Hili la mpira liache.

Michezo ni muhimu ndiyo maana tuna wizara ya michezo.

Ongelea mambo mengine ya msingi bila kugusa furaha za watu, utaeleweka tu!
najua kuwa nitatukanwa sana, nitapingwa sana, nitabezwa sana, but the truth remains intact! Watertight!
 
Football hooliganisim..kwanini unakuwa termed as such?

Football hooliganism, also known as soccer hooliganism,[1] football rioting or soccer rioting constitutes violence and other destructive behaviours perpetrated by spectators at association football events.[2]

Football hooliganism involves a wide range of behaviour, including:

  • taunting, often with racial slurs, ethnic slurs or hate speech
  • spitting
  • unarmed fighting
  • use of laser pens to disorient players of the opposing team
  • throwing of objects on to the pitch, either in an attempt to harm players, fans and officials or as a gesture of insult.
  • throwing of objects at opposing supporters, including stones, bricks, coins, flares, fireworks and Molotov cocktails.[3][4]
  • fighting with weapons including sports bats, glass bottles, rocks, rebar, knives, machetes and firearms.[6]
  • disorderly crowd behaviour such as pushing, which may cause stadium fixtures such as fences and walls to collapse. Similar effects can occur when law-abiding crowds try to flee disorder caused by hooligans.[7]
  • burning the pitch and placing the emblem of a rival team in the grass.
  • In some places, there is vandalism in the form of graffiti sprayed to promote football teams, especially in derby cities.
  • committing an act of arson
  • promotion of racism or extremist ideologies such as white supremacism, and neo-Nazism.
  • A highly violent and severe hooliganism may considered as an act of terrorism, especially those involving weapons. Violent hooliganism may cause intervention from a riot police or in some countries, the military.
Missile of the Nation kindly refer to the above
 
Ukiona mtu , Rais anajiingiza kwenye mipira (ambayo ni michezo ya kihuni, football hooliganism) ujue kuwa huyu mtu ni weak in all aspects of leadership anatafuta cheap popularity kutoka low minded people
Anajifichia na kutaka cheap populality. Hata huko hana mikakati endelevu zaidi ya kuzengea matokeo na fujo za Simba na Yanga
 
Kwani we mama Unalipwa bilion ngapi kuitetea CCM na uislamu hata pale ambapo mambo ya hovyo yanatendeka?

Poroji ndeefu ilinuweje?

Porojo ndeefu ili iweje? Hii ni "social media" siyo "thesis". Weka mada moja fupi ueleweke, unakimbilia wapi?

Unataka awe mkurupukaji kama bwana yule? Matokeo hasi ya ukurupukaji bado hujayaelewa?

Umeyaongelea ya Kariakoo, ni kipi kimecheleweshwa katika kufanyiwa kazi ya Kariakoo?
 
𝑴𝑮𝑶𝑴𝑶 𝑾𝑨 𝑲𝑨𝑹𝑰𝑨𝑲𝑶𝑶 𝑵𝑰 𝑴𝑨𝑻𝑶𝑲𝑬𝑶 𝒀𝑨 𝑼𝑲𝑰𝑴𝒀𝑨 𝑾𝑨 𝑹𝑨𝑰𝑺.

Ni miaka miwili imepita tangu Samia aapishwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika miaka yake miwili tumeshuhudia Rais akiwa mzito wa kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi na viongozi wasiokuwa waaminifu kwa Jamhuri ya Muungano. Sijui ni kigugumizi gani au uwezo wake wa kiutendaji umewekwa kwenye koma/ICU na wala nchi?

Kuna mambo mengi sana Rais yuko kimya na kwa uchache ngoja nizungumzie mambo matatu ambayo ni Mauwaji mikononi mwa polisi, Tozo na mfumuko wa bei pamoja na ufisadi.

1. 𝐌𝐀𝐔𝐖𝐀𝐉𝐈/𝐔𝐓𝐄𝐊𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐈𝐊𝐎𝐍𝐎𝐍𝐈 𝐌𝐖𝐀 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈.

Kumekuwa na mwendelezo wa utekaji pamoja na mauwaji ya watuhumiwa katika vituo vya polisi. Baada ya Rais Samia kuchukua ofisi pale ikulu Machi 2021 watu wengi waliamini kwamba ule ulikuwa mwisho wa watu kutekwa, kuteswa na kuuwawa. Lakini baada ya muda mambo ya mauwaji na utekaji yalijirudia. Tena safari hii wahanga wakubwa wakiwa raia wa kawaida na si wakosoaji wa serikali kama enzi za Magufuli. Wakati mwingine nawaza kwamba huenda Rais Samia kubadilisha viongozi na wakuu wa vyombo vya dola kulilenga kusuka safu yake mpya ya uongozi na sio kukomesha mauwaji na utekaji unaofanywa na baadhi ya watumishi vyombo vya dola.

Tulishuhudia vijana watano wafanyabiashara wa Kariakoo wakikamatwa na watu waliodaiwa kuwa ni polisi kisha wakapelekwa kusikojulikana. Hata ndugu zao walipoenda polisi kujua hatima majibu waliyopewa yaliwashitua kwani polisi walikana kuhusika kuwashikilia. Ni mwaka mmoja na miezi sasa hawa vijana hawajapatikana. Pamoja na kelele tulizopiga mitandaoni, kelele za ndugu pamoja na vyombo vya habari hazijasaidia kuwarudisha vijana hao. Rais ambaye ndiye amiri jeshi mkuu na moja ya majukumu yake ni kuhakikisha raia wake wako salama hajawajibika na wala hajamwajibisha yoyote sio waziri au IGP ni kama vile kuku zimepotea. Amekaa kimya kana kwamba hausiki au hawajibiki na usalama wa raia.

Sio hao tu orodha ya watu kutekwa na wengine kufia vituo vya polisi iliendelea kila kona ya nchi. Mauwaji ya raia Mtwara baada ya kelele nyingi kwa mbaaali angarau akamwagiza waziri mkuu aunde tume ambayo mpaka leo ni mwaka hakuna ripoti ya hiyo tume. Sijui tatizo ni yeye au waziri mkuu?

Baada ya kuona ripoti ya tume mauwaji ya Mtwara imefungiwa maandazi kashfa za watu kufia vituo vya polisi ziliendelea huku polisi wakisingizia watuhumiwa hujinyonga wenyewe. Ilifika mahali polisi walidai wengine walijinyonga kwa kutumia chupi lakini bado Rais Samia kakaa kimya. Orodha ya watu waliofia vituo vya polisi na wengine kutekwa na polisi kwa upande wangu peke yangu nimepokea majina 20 ndani ya miaka miwili ya Samia. Juhudi zetu pamoja na kelele za kutaka hatua kuchukuliwa haijazaa matunda kana kwamba najiuliza hivi kweli tuna Rais au tumeweka shati golini?

2.𝐓𝐎𝐙𝐎 𝐍𝐀 𝐌𝐅𝐔𝐌𝐔𝐊𝐎 𝐖𝐀 𝐁𝐄𝐈.

Tumeshuhudia baada ya Rais Samia kuapishwa kwa haraka alifanya mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri japokuwa mawaziri wengi alirithi kutoka kwa mtangulizi wake akiwemo waziri mkuu. Watu walianza kuwa na matumaini kwamba huenda angepunguza ukata wa maisha ulioletwa na mtangulizi wake lakini mambo hayakuwa hivyo.

Siku 40 za mwanzo tu serikali ya Samia ilipandisha gharama za vifurushi vya internet DATA mara mbili kuliko ilivyokuwa awali. Shilingi elfu moja ambayo ilikuwa na uwezo wa kununua GB moja ya internet sasa ikawa inanunua MB 400 tu. Wananchi wakaanza kulalamika kelele zikawa nyingi lakini ndio kwanza Rais alikausha kimya kana kwamba haishi Tanzania na malalamiko hayaoni. Waziri wake sijui anaitwa Nape anajibu kwa kiburi kwamba kama vifurushi ni gharama zimeni data na Rais yupo kimya tu.

Wakati kidonda cha kupanda kwa data kikiendelea kuuma likafuata pigo lingine la tozo kwenye miamala ya simu na bank. Unatumiwa buku 5 unatoa buku 3 buku 2 imeishia kwenye makato achilia mbali aliyekutumia naye kukatwa tozo. Katikati ya kilio cha tozo likapigwa kombola lingine la mfumuko wa bei. Gharama za maisha zikaongezeka vilio vya machinga na wakulima bei za mbolea lakini bado Rais akaendelea kukaa kimya kana kwamba hahusiki na wala hawajibiki na chochote. Hata akiongea basi naye analalamika kama sisi mpaka najiuliza pale ikulu tuna Rais kweli au tumeweka shati golini?

3. 𝐔𝐅𝐈𝐒𝐀𝐃𝐈

Wengi waliamini kwamba pengine serikali ya Rais Samia kuongeza tozo na kodi mbalimbali kwa wananchi alikuwa analenga kupunguza deni la taifa kama ambavyo Rais Mkapa alifanya katika utawala wake kwa kutokukopa na kupunguza deni la Rais Mwinyi. Takwimu za deni la taifa zikatushitua. Rais Magufuli ndio alishikilia rekodi ya Rais aliyekopa pesa nyingi kwa kipindi cha miaka mitano kuliko watangulizi wake. Lakini rekodi hiyo ilivunjwa na Rais Samia kwa mwaka mmoja tu. Yani pesa ambayo Rais Magufuli aliikopa kwa miaka mitano Samia kaikopa kwa mwaka na wakati huo hata matumizi ya mikopo hiyo hayaeleweki .

Wakati tumepigwa butwaa tukijiuliza imekuwaje mara anaibuka mkaguzi mkuu na mdhibiti wa hesabu za serikali CAG anatusanua namna ambayo watumishi wa umma na viongozi wa serikali walivyovuja pesa za umma. Wengi wakaamini kwamba Rais angechukua hatua kwa ripoti ile lakini hakuchukua hatua yoyote zaidi ya kuwataka wezi hao kula urefu wa kamba zao.

Mwaka mmoja baadaye inatoka ripoti nyingine ya CAG ikionyesha uvujaji na wizi mkubwa wa pesa za umma kukiwa na zaidi ya trillion 2 zilizoibiwa. Hapa Rais angarau alichukua hatua kidogo kwa kuwatukana wezi stupid lakini hakuwawajibisha kwa kuwafukuza kazi au kuwasimamisha ama kuwapeleka mahakamani.

Mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo ni matokeo ya ukimya wa Rais. Kushindwa kusikiliza, kutafuta majawabu na kuchukua hatua ni mambo yaliyopelea mgomo huu. Baada ya kikao cha waziri mkuu na uongozi wa wafanyabiashara wa Kariakoo siku ya jumatatu kushindwa kuzaa matunda na mgomo kuendelea siku iliyofuata, nilitegemea Rais angechukua point 3 kwa kwenda kuwasikiliza mwenyewe na kuchukua hatua. Lakini kama kawaida yake kakaa kimya. Pengine hajui madhara yake. Kuna siku mgomo hautakuwa wa Kariakoo pekee bali utakuwa mgomo wa nchi nzima utakaozalisha maandamano yanayoweza kuangusha serikali yake.

Vipi Rais Samia angeibuka mwenyewe pale MnaziMmoja kusikiliza kero za wafanyabiashara wa Kariakoo zilizopelekea wao kugoma kufungua maduka? Halafu baada ya mkutano avunje bodi ya TRA, afukuze waziri na kamishina wa TRA. Ingempandisha chati kiasi gani? Angepata sifa kiasi gani? Tukio hilo lingerudisha nidhamu kwa viongozi na watumishi wa umma kiasi gani?

Shida ya Samia nini kutochukua hatua?

𝑴𝒅𝒖𝒅𝒆 𝑵𝒚𝒂𝒈𝒂𝒍𝒊 𝟕 𝒙 𝟕𝟎 𝑺𝒖𝒎𝒖 𝒚𝒂 𝑵𝒚𝒊𝒈𝒖.

View attachment 2626057
Haikuwa na haja ya kuandika kirefu sana,ungeandika kifupi sana, heading inajitosheleza,ungesubiria majibu tu kwa wachangiaji.

Kifupi huyo mama yako kaamua kulitumikia kundi flani na kuona anpendwa na watanzania wote,badala ya kutimiza majukumu yake kwa nchi,ikiwemo kupambana na rushwa, uzembe,na wizi kwa nguvu zake zote
 
Back
Top Bottom