Kwanini Rais hajawapa pole Clouds?

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,803
48,959
Kituo cha Clouds media juzi kilivamiwa na mkuu wa mkoa Paul Makonda, watu mbalimbali wamekuwa wakitoa pole na hata maneno ya kuwatia moyo, ajabu hadi sasa sijasikia tamko lolote kutoka kwa kiongozi mkuu wa nchi kuwapa pole rafiki zake waliomfanyia kampeni ya nguvu nchi nzima.

Rais kama kiongozi wa nchi anatakiwa awe mfano wa kuigwa na upendo kwa wananchi wake wote bila kujali ni rafiki zake au adui wa rafiki yake.

Namkumbusha tu kwamba aelewe kuna kesho, Makonda peke yake asingeweza kumuingiza madarakani kama anavyodhani, atakuja kuwahitaji tena kipindi kingine.
 
pole ya nini? wakati hakuna ata video moja ambayo inaonesha kuna uharibifu uliofanywa na makonda wowote, zaidi ya makonda kuingia mapokezi.ruge anasema kuna cctv camera kila kona kwenye mjengo.na kama aliweza kusimama mbele ya media yake na kusema uovu wa bwana makonda kwanini anashindwa kuweka na video inayoonesha sudi na timu yake wanapigwa??
 
Neno Pole kwake SUMU!
 
Hivi ndugu mbona unakua mgumu kuelewa? Swala la kupigwa au kutokupigwa ni secondary....sio la msingi. Swala la msingi ni mkuu wa mkoa kuvamia kitu cha media usiku akiambatana na maaskari wenye silaha za moto. Kwenye nchi yoyote inayojiheshimu swala kama hilo ni ishara ya kupindua nchi! Jambo kama hili halitakiwi kuchukuliwa kiwepesiwepesi tu eti "Rais amefunga mjadala". No!
 
Back
Top Bottom