Kwanini radi au thunderstorm haijawahi kuangusha ndege?

Kwanini radi au thunderstorm haijawahi kuangusha ndege?

Kwa hiyo ndio unaomba Hilo litokee kwa kuwa wewe si mtumiaji wa usafiri huo?
 
Mi nimekuwa nikijiuliza sana kuwa iweje radi iko mawinguni lakini sijawahi kusikia imepiga watu waliomo ndani ya ndege au kusambaratisha ndege badala yake inawinda chini ya ardhi tu? Au kwanini sijawahi kusikia radi imepiga Dar es salaam. Mi naona ni mauzauza ya kichawi tu!!
Nijuavyo ndege ina ruka 30,000ft sasa ni juu zaidi ya hayo mawingu .....

Fanya siku unaenda #Dubai au #Qatar utaona mawingu yapo chini kama uwanja flani usio na mwisho
 
Mleta uzi, radi ni umeme hivyo hakuna kitu kisichopigwa na radi hata hizo ndege unazosema bali ni issue zinazohusiana na kanuni za umeme na ndio maana unaona hazipigwi radi na hata gari pia...kuhusu Dar es salaam, kimsingi hata Dar radi zinapiga kila siku sema tu mijini kuna vizuia radi vingi kuliko vijijini na ndio maana kesi ya radi maeneo ya vijijini ni kubwa kuliko mijini yaani minara ya simu, mitambo ya umeme, minara ya radio na hata milima maana radi zina mtindo wa kupiga zile sehemu ambazo zipo juu na ndio maana mtu akikaa kwenye mti uwezekano wa kutandikwa radi ni mkubwa
 
Kwenye mada hii niwajulishe tu kuwa asilimia kubwa ya sehemu zinazopigwa na radi ni shule za msingi, kwanini hata mimi sijui.
 
wewe naye umeambiwa juu kuvuka mawingu ya mvua inamaana hata kukiwa na mawingu huko sio ya mvua soma climatology aina za clouds
Muonee huruma mwenzako maana wengi hawajui hayo mawingu wanayoyaona yapo karibu sana kiasi ndege ikiruka inayaacha chini...siku akipanda ndege atajifunza kitu mkuu ni maswali ya kidadisi tu hayo
 
Kwenye mada hii niwajulishe tu kuwa asilimia kubwa ya sehemu zinazopigwa na radi ni shule za msingi, kwanini hata mimi sijui.
Maeneo mengi ya shule huwa kuna miti mingi mirefu na radi huwa ina mtindo kupiga ile sehemu ambayo ipo juu hivyo nahisi ndio sababu kwanini inaleta madhara zaidi mashuleni (ngoja wataalam waje zaidi)
 
Radi inapendelea mikoa yenye milima,pia kwa kanda ya ziwa na magharibi radi zingine n za ulozi
Upande wa magharibi mwa nchi ndipo pepo mbili hukutana, yaani upepo kutoka mashariki(bahari ya Hindi) na upepo kutoka magharibi (bahari ya Atlantic).Hivyo basi,mgongano wa hizo hewa ndo unazalisha radi even if hakuna mvua au mawingu.Hii ni kijiografia zaidi sio ushirikina.
 
Au hata gari wakuu nani amewahi sikia imepigwa radi ikiwa inatembea?
Kwenye gari hasa malori makubwa au mafuso kuna kama mnyororo hivi huwa una ning'inia chini ya uvungu wa gari, chunguza utauona..ingawa utaniuliza vitz na ist vipi?

Maelezo yangu sio sharia naweza sahihishwa.
 
Back
Top Bottom