Kwanini Padre hatoi sadaka kanisani?

Kwanini Padre hatoi sadaka kanisani?

Kwanini unizibe mdomo, niache niongee nchi huru hii..... halafu pia nimeandika kulingana na mada husika,
Mwanzo ulisema nazusha sasa hivi Padri amekua mwanaume [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Bado hujasema, utasema yote
Tatizo lako mwanzoni ulikuwa unajibaraguza. Walau sasa umekuwa muwazi. Kwa hiyo tutaenda taratibu. Nataka nimfanyie Padre mapinduzi. Je, uko tayari?
 
Hili ni swali ambalo nimeulizwa na watu wengi sana huku wakitaka kujua, ni sababu zipi zinazomfanya Padre ashindwe kutoa sadaka Kanisani kama wanavyofanya Waamini wengine?

Maana wakati wa adhimisho la Misa Takatifu, mara nyingi tunamsikia Padre akisema: "𝐒𝐚𝐥𝐢𝐧𝐢 𝐧𝐝𝐮𝐠𝐮 𝐢𝐥𝐢 𝐬𝐚𝐝𝐚𝐤𝐚 𝐲𝐚𝐧𝐠𝐮 𝐧𝐚 𝐲𝐞𝐧𝐮 𝐢𝐤𝐮𝐛𝐚𝐥𝐢𝐰𝐞 𝐧𝐚 𝐌𝐮𝐧𝐠𝐮 𝐦𝐰𝐞𝐧𝐲𝐞𝐳𝐢".

𝐒𝐖𝐀𝐋𝐈: Sasa sadaka anayoitoa Padre hapo ni ipi wakati hatuioni?

𝐉𝐈𝐁𝐔: Ni kweli kabisa kwa macho ya kawaida, ni vigumu kuiona sadaka anayoitoa Padre altareni kama vile wanavyofanya Waamini wengine, lakini nikuambie kwamba, sadaka ya Padre ni kubwa zaidi kuliko ya mtu yoyote yule.

Ngoja nikuulize swali: Hivi ushawahi kujiuliza kwanini wakati wa utoaji wa sakramenti ya daraja takatifu, Mapadre huwa wanalala chini kifudifudi huku akisaliwa sala maalumu pamoja na litania ya Watakatifu kabla hajawekwa wakfu na Askofu kwa kupakwa mafuta kwenye viganja vyake mikono na kuvalishwa rasmi mavazi ya kikuhani?

Hakika wengi wanadhani kitendo hicho cha kulala kifudifudi kwa Padre, basi anaweka nadhiri za utii kwa Askofu na kumuahidia kuishi maisha ya usafi wa moyo bila kufunga ndoa, ili aweze kumtumikia Mungu kwa uhuru zaidi.

Niseme tu kwamba, hayo yote yanaweza kuwa majibu ila sio kwa mantiki hiyo ya kulala kifudifudi. Kwani kitendo cha Padre kulala kifudifudi, inaashiria kujitoa sadaka kwa ajili ya kuutangaza Ufalme wa Mungu na kuufia ulimwengu kama Yesu alivyofanya.

Kwa sababu hiyo katika hatari yoyote ile ya kifo, ni rahisi sana kumuona Padre akiwa yuko radhi kutoa maisha yake kwa ajili ya Mungu na Kanisa ili kutetea imani iliyoachwa tangu zamani na Mitume wa Yesu.

Kadhalika ukiachana na sababu hiyo, pia hata maisha yake kwa ujumla ni sadaka tosha. Maana wakati wewe unalala usiku, Padre hutumia muda huo kuwaombea watu, yuko tayari kuacha chakula chake ili kumuwahi mgonjwa anayekaribia kufa na kumpa Sakramenti ya Upako. Wakati wote anashinda Kanisani ili kusikiliza shida za watu na kuwasaidia, daima aachi kutoa Sakramenti ya Kitubio hata kama afya yake haiko vizuri siku hiyo.

Maisha ya Padre kwa nje unaweza kuona ni mepesi, ila ukweli ni magumu sana, bila sala na moyo wa majitoleo huwezi. Kwa sababu kokote pale Padre akihitajika huwa anafika kwa wakati licha ya kuwa na kazi nyingi. Tena muda mwingine kwenye msiba utamkuta Padre anahuzunika na wale waliofiwa hata kama msiba huo haumuhusu, na wakati wa harusi hufurahi pamoja na wale waliofunga ndoa. Kwangu hiyo ni sadaka, sasa sijui muuliza swali alikuwa anataka sadaka ipi?

Maana Padre hawezi kutoa sadaka ya pesa, mazao au mnyama wa aina yoyote yule kama Wakristo wengine wanavyotoa. Ukweli nikuambie tu kuwa, muda mrefu Padre kashajisadaka tayari mwili na roho yake kwa lengo la kumtumikia Mungu na Kanisa. Na ndio sababu nasema, sadaka ya Padre ni kubwa zaidi kuliko zile tunazozitoa sisi kila siku.

Pia hata tukisema leo hii sheria ipitishwe rasmi, eti Padre naye atoe sadaka sawa na Waamini wengine. Je unafikiri sadaka hiyo Padre ataitoa wapi, wakati hana kazi wala kitega uchumi chochote kitachomuwezesha kufanya hayo yote?

Nadhani hapo ndio mwanzo wa Kanisa kuingia katika migogoro, kisa tu Padre ameanza tabia ya kuiba sadaka za watu ili apate pesa za kutoa Kanisani. Suala hili sio nzuri na halifai kabisa.

Kwani ukisoma vema Biblia, utakutana na kisa cha makabila 12 ya Waisraeli, ambayo makabila hayo yote yalipewa urithi katika sehemu yake ila kasoro kabila moja tu la Walawi, maana urithi wao ulikuwa kwa Bwana pekee na walipewa kibali cha kutumia sadaka zote zilizotolewa na Waisraeli wa wakati ule Hekaluni. (𝐌𝐰𝐚𝐧𝐳𝐨 14:17-20).

Biblia inatuambia kabila hilo la Walawi ndilo lililowekwa wakfu kwa lengo la kutoa Makuhani kwa kazi ya Mungu tu, utaratibu ambao unatumika hadi sasa kwa Mapadre wetu. (𝐖𝐚𝐥𝐚𝐰𝐢 22:1-33).

Kwahiyo nihitimishe kwa kusema kwamba, sote kama wanadamu tuna wajibu wa kutoa sadaka ingawa sadaka zetu zinatofautiana kidogo. Maana Padre hutoa sadaka yake ya mwili na roho kwa ajili ya Kanisa, na sisi basi tutoe sadaka za pesa na mali tulizonazo kwa ajili ya kujiombea wenyewe baraka na wale wote wanaotuzunguka.

𝐓𝐔𝐌𝐒𝐈𝐅𝐔 𝐘𝐄𝐒𝐔 𝐊𝐑𝐈𝐒𝐓𝐎 [emoji120]View attachment 2763637
Picha inajieleza vizuri mapadre wamejitoa sadaka maisha yao yote.
 
Nampenda Padre anajua kuhandle na kuhonga sadaka za kanisa....[emoji847]
Hata ukija kwangu nitaku handle vizuri sana tu. Na kuhusu kuhonga, hilo usiwe na shaka. Mimi ninaweza kuuza hata mashamba yote ya ukoo, halafu hela yote nikakukabidhi ili uanzishie biashara.
 
Padre Rayns Kuna swali huku?
mara ya mwisho mimi kukanyaga RC Church ni mwaka 2012 sikumbuki kama padri alikua anatoa sadaka au hapana... Kwasabu padri ndio huwa ananufaika na sadaka labda ndio maana... Maana hata akitoa zinarudi kwake(kwa baadhi ya madhehebu niliyoona nikiwa mkubwa)...
 
Sadaka ya Padre ni kule kujitoa kwake kwa ajili ya kazi ya Mungu.

Tukumbuke hawa wanatokana na jamii zilizokuwa na hamu ya kuona wajukuu za watoto zao(baba&mama zao),wao wenyewe kama wanaume walitamani waitwe baba lakini wito walioitiwa umewaondolea uhuru huo,mimi nina uwezo wa kufanya kazi zaidi ya moja kwa wakati mmoja wao kazi yao ni moja tu na haina kusitasita.

Akiamshwa usiku kuna dharura ya mgonjwa hana kujiuliza,akiambiwa penye uhitaji wa ibada yoyote ile hana kujiuliza ni kwenda tofauti na mimi always nina option ya kukubali au kukataa,ile siyo kazi rahisi kama inavyochukuliwa siku hizi tuna mpaka sala za kuombea miito mitakatifu kutokana na wapo baadhi ya wazazi kukataa kuruhusu watoto wao kuitikia wito wao kwa sababu wanajua ni kitu kinawakosesha baadhi ya vitu kama wanajamii.
 
mara ya mwisho mimi kukanyaga RC Church ni mwaka 2012 sikumbuki kama padri alikua anatoa sadaka au hapana... Kwasabu padri ndio huwa ananufaika na sadaka labda ndio maana... Maana hata akitoa zinarudi kwake(kwa baadhi ya madhehebu niliyoona nikiwa mkubwa)...
🤣🙏🙏
 
Back
Top Bottom