Nimeshuhudia mara kadhaa,wimbo wake wa TUPOGO,popote unapopigwa basi kama watu hawasimami kuucheza,utaona hata wenye aibu wanatingisha mabega au kugongagonga miguu,ni wimbo huko juu,kuanzia maudhui na hata beats zake.Nilienda nchi za jirani hivi karibuni nikashangaa kukuta hata huko huo wimbo uapendwa sana,kwa maoni yangu wimbo huu ni bora kuliko wimbo wowote uwe wa Diamond au nani,hapo ndipo nilishangaa na kujiuliza ni kwanini kwenye hizi tuzo za Kili huu Wimbo haukunyakua japo tuzo moja