Kwanini NSSF wanahitaji 'Bank Statement' ya Mwanachama?

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,486
8,706
Nini huwa wanataka kuona kwenye 'Bank Statement' kwa wale wanao jaza fomu za mafao ya kutokuwa na ajira? Wanaojua siri ya wao kutaka 'Bank Statement' wanisaidie nisije ingia kichwa kichwa ikala kwangu, na je kama nina account mbili za bank inakuwaje hapo?
 
Lengo lao ni kuthibitisha kama kweli ulikuwa unapokea mshahara, pia kuthibitisha kama mshahara uliingiziwa kiasi gani kwa kila mwezi husika maana wakati mwingine mishahara hubadilika kutokana na mazingira mbalimbali.
Kwa hiyo wanachofanya ni kulinganisha kilichopo kwenye payslip kama kinaendana na kwenye bank statement.
 
Lengo lao ni kuthibitisha kama kweli ulikuwa unapokea mshahara,pia kuthibitisha kama mshahara uliingiziwa kiasi gani kwa kila mwezi husika maana wakati mwingine mishahara hubadilika kutokana na mazingira mbalimbali.
Kwa hyo wanachofanya ni kulinganisha kilichopo kwenye payslip kama kinaendana na kwenye bank statement.
Kwani watu wote mishahara hupitia bank?
 
waajiriwa wote lazima mishahara ipitie bank.
Ukiona mtu anapewa mshahara mkononi ujue huyo ni kibarua tu au deiwaka.
Hata hao vibarua kama watakaa kwa muda mrefu hairuhusiwi kuwalipa hela mkononi ni lazima walipwe hela benki.

Naomba kuuliza hivi na hao vibarua ( wanao pewa hela mkononi) mf; wafanyakazi wa viwandani
wanakidhi vigezo vya kukatwa nssf?
 
Wanataka kuhakikisha kama account yako ina hela angalau kuanzia Tsh 7,000/=
Nilimuuliza meneja wa NSSF Arusha kuhusu hili jambo akanijibu hivyo. Kama account yako ya Bank haina hela kabisa au iko pungufu ya 7,000 wanashindwa kukuwekea michango yako kwenye account.
 
Wanashindwa nini?
Wanataka kuhakikisha kama account yako ina hela angalau kuanzia Tsh 7,000/=
Nilimuuliza meneja wa NSSF Arusha kuhusu hili jambo akanijibu hivo. Kama account yako ya Bank haina hela kabisa au iko pungufu ya 7,000 wanashindwa kukuwekea michango yako kwenye account
 
Na vipi kama ina hela nyingi zaidi ya Milion?
Wanataka kuhakikisha kama account yako ina hela angalau kuanzia Tsh 7,000/=
Nilimuuliza meneja wa NSSF Arusha kuhusu hili jambo akanijibu hivo. Kama account yako ya Bank haina hela kabisa au iko pungufu ya 7,000 wanashindwa kukuwekea michango yako kwenye account
 
Naomba kuuliza hivi na hao vibarua ( wanao pewa hela mkononi) mf; wafanyakazi wa viwandani
wanakidhi vigezo vya kukatwa nssf?
Kwa mfumo wa sasa wote wanatakiwa wakatwe NSSF, ambao hawakatwi ni wale vibarua wa muda mfupi lakini ukishakaa na kibarua kuanzia miezi 6 kama sikosei huyo anakuwa muajiriwa.
 
Nini huwa wanataka kuona kwenye Bank statement kwa wale wanao jaza fomu za mafao ya kutokiwa na ajira? Wanaojua siri ya wao kutaka bank statement wanisaidie nisije ingia kichwa kichwa ikala kwangu, na je kama nina account mbili za bank inakuwaje hapo?
Huo ni utapeli ulianzishwa na NSSF kwa kushirikiana na mabenki kusudi kama ulikuwa na mkopo na hujamaliza wakate juu kwa juu ndio maana wanataka account uliyokuwa unapitishia mshahara kwani wana uhakika lazima benki iliyokukopesha iwe ndiyo ile unayopitishia mshahara wako. Huu ni wizi kwani sheria ya mafao hairuhusu mtu kuingilia mafao yako.
 
Nini huwa wanataka kuona kwenye Bank statement kwa wale wanao jaza fomu za mafao ya kutokuwa na ajira? Wanaojua siri ya wao kutaka bank statement wanisaidie nisije ingia kichwa kichwa ikala kwangu, na je kama nina account mbili za bank inakuwaje hapo?
Mkuu samahani nje ya mada, hapo unashughulikia nssf wakupe mpunga wako wote sio? Au watakupa kiasi gani.

Na swali la nyongeza unatakiwa u submit documents gani wakupe huo mshiko?
 
Nia hasa ni kuhakikisha particulars zako za kibenki ziko sahihi na ulivyo jaza kwenye form zao kuepuka kudeposit hela kwenye account fake.
 
Huo ni utapeli ulianzishwa na NSSF kwa kushirikiana na mabenki kusudi kama ulikuwa na mkopo na hujamaliza wakate juu kwa juu ndio maana wanataka account uliyokuwa unapitishia mshahara kwani wana uhakika lazima benki iliyokukopesha iwe ndiyo ile unayopitishia mshahara wako. Huu ni wizi kwani sheria ya mafao hairuhusu mtu kuingilia mafao yako.
Kwahiyo wewe hutaki ukatwe mkopo au? lipa mkopo acha ujanja wa kijinga
 
Hahaaaa hawatoi yote now day wanatoa 30% tu
Mkuu samahani nje ya mada, hapo unashughulikia nssf wakupe mpunga wako wote sio? Au watakupa kiasi gani.

Na swali la nyongeza unatakiwa u submit documents gani wakupe huo mshiko?
 
Kuna Process ndefu sana, wanataka Barua, Bank statement, Copy ya vitambulisho, Certificate of Service kutoka kwa mwajiri wako na pia kuna sehemu ya fomu inajazwa na mwajiri wako
Mkuu samahani nje ya mada, hapo unashughulikia nssf wakupe mpunga wako wote sio? Au watakupa kiasi gani.

Na swali la nyongeza unatakiwa u submit documents gani wakupe huo mshiko?
 
Back
Top Bottom