Kwanini NMB tu itumike kulipia maduhuli ya TRA?

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,523
Kila ninapkwenda kukdadiriwa mapato yangu na TRA na baada ya makadiro hayo ninaelekezwa kwenda kulipia kupitia NMB.

Wengine makazi yetu na shughuli zetu ziko mbali na NMB lakini bado tunaelekezwa kwenda NMB. Taasisi zingine huwa ni uchaguzi wa mteja aidha aende NMB, CRDB, EXIM na hata kwa wakala. Ninaomba mtindo wa kulipia NMB uwe ni uchaguzi wa mteja na muwe na orodha ya Mabenki mengine yanayoweza kupokea maduhuli yenu na isiwe tu NMB.
 
Unaweza kuamulia taasisi iwe na akaunti benki unayotaka wewe?
 
Control number unalipia hata kwa simu yako. Kama hujapewa control number basi umepigwa kweupe
 
Kila ninapkwenda kukdadiriwa mapato yangu na TRA na baada ya makadiro hayo ninaelekezwa kwenda kulipia kupitia NMB.

Wengine makazi yetu na shughuli zetu ziko mbali na NMB lakini bado tunaelekezwa kwenda NMB. Taasisi zingine huwa ni uchaguzi wa mteja aidha aende NMB, CRDB, EXIM na hata kwa wakala. Ninaomba mtindo wa kulipia NMB uwe ni uchaguzi wa mteja na muwe na orodha ya Mabenki mengine yanayoweza kupokea maduhuli yenu na isiwe tu NMB.
Una uhakika au unalaumu tu kabla ya kufanya utafiti?
 
Unaweza kuamulia taasisi iwe na akaunti benki unayotaka wewe?
Ni haki yake kama mdau(mlipa kodi)
Taasisi za uma zipo kwaajili ya kutoa huduma.. (kumrahisishia mlipakodi kutekeleza wajibu wake)
 
Na wao wana haki ya kufanya kazi na benki wanayoona inawafaa
 
Kila ninapkwenda kukdadiriwa mapato yangu na TRA na baada ya makadiro hayo ninaelekezwa kwenda kulipia kupitia NMB.

Wengine makazi yetu na shughuli zetu ziko mbali na NMB lakini bado tunaelekezwa kwenda NMB. Taasisi zingine huwa ni uchaguzi wa mteja aidha aende NMB, CRDB, EXIM na hata kwa wakala. Ninaomba mtindo wa kulipia NMB uwe ni uchaguzi wa mteja na muwe na orodha ya Mabenki mengine yanayoweza kupokea maduhuli yenu na isiwe tu NMB.
naomba kwanza nikiri mimi ni nafanya biashara na ninalipa walau kodi mamlaka ya mapato tra ila sijawahi sikia hii sababu mm huwa nalipia crdb nachoambiwa control nam,ba yangu na ninaamua bank gani crdb au nbm kulipia au hata mawakala wa bank au simu .mzee hebu angalia vizuri au muulize inchaji au meneja wa ofisi hiyo
 
Kwanza
Unaweza kulipa kwa kutumia simu au bank kwa malipo ya tra. Si lazima uende bank.
Pili, malipo ya serikali wakala wa mabenk hasa nmb na crdb na benki ya posta wanapokea. Nje ya kwenda ndani ya benki.
Pia hata kwa kutumia Hundi Ila makato ni makubwa.
Pia unaweza kufanya interbank transfer pia makato so haba.

Tatu kila benki Ina Uhuru wa kuingia mkataba na taasisi ya serikali ukiona miamala yake. Ina manufaa .hivyo hata benki zingine zikiona hakuna faida kwenye kupokea miamala hawalazimishi kuingia kwenye mfumo.
Nne tra iko tanzania nzima kila wilaya na sehemu nyingine ndaninya wilaya moja Kuna ofisi zaidi ya moja. Hivyo km traa inaingia mkataba ili mteja wake apate huduma. Inabidi aingie mkataba na mabenki yanayopatikana karibu kila wilaya na mikoa.sasa nipe jibu benki zipi Tanzania zina mtandao mkubwa kuanzia mawakala mpaka matawi?.
 
Back
Top Bottom