Kwanini ninahitaji Katiba mpya?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Kuna watu hasa viongozi wachache ambao kwa makusudi na maslahi yao binafsi wanayoyajua wao wamekua wakitumia mwanya wa ujinga wa wananchi na shida zao kuwaambia maneno ya Kitapeli eti katiba mpya haiwezi kuwapa maji,afya wala Barabara,eti wanaotaka katiba mpya ni wenye uchu wa madaraka. Huu ni utapeli mtupu.

KWANINI NINATAKA KATIBA MPYA?
Pamoja na upotoshwaji mkubwa unaofanywa na haya makundi kuwadanganya wananchi eti wanaotaka katiba mpya shida yao ni madaraka, siyo kweli!

1.Matokeo ya Urais yahojiwe Mahakamani.
Moja ya vitu vinavyoharibu amani na umoja wa taifa ni uchaguzi, kukiwa na haki katika hili kwamba kila mtu yupo chini ya sheria basi taifa litakwenda vizuri. Hii sheria ya kutohojiwa mahakamani matokeo ya urais ni uonevu na Umungu mtu, kwamba kuna walio juu na walio chini ya sheria.

2.Wakurugenzi waisimamie chaguzi zote.
Bila shaka hawa hutumika kama wasimamizi wakuu wa uchaguzi Wilayani huko, kwakua imebainika wengi ni makada wa CCM,ili kuepusha double Standards, NEC iajiri Makamishina wake ngazi za wilaya nchi nzima na hawa ndio watakaoratibu shughuli zote za Uchaguzi maeneo walipo. Wateuliwe watu wasiokua na chama chochote wenye viapo vyao.

3.Viongozi wakuu wa NEC wasiteuliwe na Rais.
Viongozi wote wa juu wa NEC kuanzia mwenyekiti wake na wakurugenzi wasiteuliwe na Rais bali iwepo tume maalum ambayo ni Independent kwa ajili ya kuteua majina ya wenye sifa ambao watatuma maombi ya kazi kupitia anwani za tume ambapo ajira yao lazima itangazwe kwenye gazeti la serikali.

4.MAJAJI WAKUU NA VIONGOZI WA MIHIMILI YA DOLA WASITEULIWE NA RAIS.
Ili kuepusha the so called conflict of interest, Kuwepo na tume maalum ambayo ni independent itakayopokea maombi ya nafsi hizo na kisha kuchambua majina yao na kupata majina ya watu wachache wenye sifa na kufanyiwa usaili, atakayeshinda usaili jina litapelekwa kwa Rais kutia saini na hatimaye kuteuliwa kua kiongozi. Hii itapunguza uoga kwa watendaji hawa kuogopa kutumbuliwa na Mamlaka za uteuzi, kutasaidia MIHIMILI hii kua huru kuchukua hatua tofauti na sasa. Hapa pia Rais anaweza kuingiza watu wake ndani ya tume lakini kunaweza kukawa na unafuu kiasi flani.

6.Kumuondolea Rais uhalali wa kuwa mwamuzi wa mwisho kuhusu ardhi ya Tanzania.
Hali hii imepelekea shida kubwa sana pale kiongozi anapo futa hati ya umiliki wa shamba la mtu ambaye amelimiliki kihalali na kugawiwa kwa watu wengine. Hii haijakaa sawa ni uonevu mkubwa na wala siyo haki. Umiliki wa ardhi ubakie mikononi mwa wananchi wenye uhalali wa kumiliki.

Kiufupi kuna mambo mengi yanatakiwa kubadilishwa katika taifa hili tuanze kuishi katika taifa litakalostawi kwa amani, umoja,upendo na demokrasia. Hivi vyote huongezewa na kustawi kukiwepo na usawa utakaopatikana ndani ya katiba mpya.
 
Imekaa vizuri isipokuwa kwenye ardhi nina maoni tofauti. Wazo langu ni kuiboresha tu hizo kanuni zake ila ardhi ibaki kuwa mali ya Serikali.
 
Naunga mkono hoja!

Katiba Mpya itambue uwepo wa Serikali tatu ili kuondoa kabisa kero za Muungano.

Katiba Mpya itakayo punguza ukubwa wa serikali kwa kuondoa vyeo vya kisiasa kama vile vya Wakuu wa Wilaya, Mikoa, nk.

Katiba mpya itakayo punguza ukubwa wa Bunge kwa kuondoa Viti Maalum, Wabunge wa kuteuliwa, wabunge kutoka Zanzibar, nk.
 
Back
Top Bottom