Kwanini nimeandika kitabu cha historia ya Beyonce na Jay Z

Kwanini nimeandika kitabu cha historia ya Beyonce na Jay Z

SkyTanzania

Member
Joined
Nov 4, 2015
Posts
11
Reaction score
15
SKY KWANINI UMEAMUA KUANDIKA KITABU CHA BEYONCE NA JAY Z BADALA YA KUANDIKA HISTORIA ZA WATU WA TANZANIA NA AFRIKA? HILI NI SWALI NINALOULIZWA SANA NA NADHANI NITAULIZWA ZAIDI KITABU KIKIZINDULIWA RASMI DECEMBER 4 MWAKA HUU

1. Nimewahi kutoa kitabu cha sauti cha Mtemi Mirambo: Sultani Mkuu wa Afrika. Kinapatikana mtandaoni na kwenye CD.

2. Siku za usoni nimefikiria kuandika vitabu vyenye mkusanyiko wa historia za wasanii wa Tanzania, mtavinunua? Au ndio mtasema mnawaona kila siku so kwanini ununue kitabu?

3. Maisha, Mapenzi na Maumivu ni vitabu vinavyozungumzia historia za maisha ya wanandoa maarufu duniani. Matoleo yajayo yatawahusu Barack na Michelle Obama, Kanye West na Kim Kardashian, David na Victoria Beckham nk. Kama wakifunga ndoa, Diamond na Zari, Vanessa Mdee na Jux au Nahreel na Aika watahusika pia, why not!


4. Beyonce na Jay Z si watu wageni katika maisha yetu. Tumewafahamu kwa takriban miongo miwili sasa. Wengi, hususan vijana tunajua nyimbo zao na kwa kiasi kikubwa muziki wao hutuchangamsha. Hakuna tofauti na jinsi ambavyo mtu anakuwa shabiki wa Manchester United, Chelsea, Arsenal, Real Madrid au Barcelona wakati ni timu za nje ambako hajawahi hata kufika au kuonana nao.

5. Walengwa wa kitabu hiki ni wale wanaowafahamu Jay Z na Beyonce na wanaopenda kuwafahamu zaidi. Pia kitabu hiki kitawafungua pia wale wasiowafahamu kabisa. 6. Kitabu kimeandikwa kwa Kiswahili na kinawezwa kusomwa na mtu yoyote duniani anayezungumza lugha hiyo au anayejifunza

7. Beyonce na Jay Z wana historia ya kuvutia sana ambayo inaweza kumfurahisha mtu yoyote. Wana vingi tunavyoweza kujifunza katika maisha ya kawaida

9. Kibiashara kitabu hiki kina nafasi kubwa zaidi ya kufanya vizuri kwakuwa hawa ni watu wanaofahamika dunia nzima. Mfano mzuri ni audio book ya Mirambo ambayo niligundua kuwa watu nje ya Tanzania hawamjui ama hawako interested na mwisho wa siku sifanyi kwa kujifurahisha tu. Hii ni sehemu yangu ya kutumia uwezo nilionao kujiongezea kipato


10. Mimi ni shabiki mkubwa wa Beyonce na Jay Z. Kitabu hiki nimekiandika kwa kufurahia sana na ile feeling ya kukikamilisha ni kubwa zaidi kuliko hata kitakavyouza

Nataka kufanya kitu tofauti

Wasiliana nami kwa namba 0766173514
 
ungeandika historia ya diamond kutoka alivyokuwa anauza mitumba manzese mpaka kuja kuwa mwanamuziki mkubwa nadhani ingekuwa poa zaidi...
 
Hili bandiko lako kumbe liko Mara mbili au mod walilitoa lile jengine?
Nalog off
 
Kujipendekeza nacho ni kipaji, unacho kipaji hicho, na yangekuwepo mashindano ya dunia ya kujipendekeza hakika ungeliletea taifa hili medali ya dhahabu.
 
Julius K Nyerere na Maria Nyerere
J k Kikwete na Salma
Edward Lowasa na Regina (nimezoea kumuita D
First lady so jina naweza kuwa nimekosea)

King Majuto na mkewe
Paul Kagame na Janeth Kagame
Reginald Mengi na mkewe namba 1 hadi sasa
Azam Bakhresa na mkewe? wakeze
 
Umefurahi sana,

Ila Ulipata ruhusa yao na pia je wanajua na kukubaliana na uliyoyaandika?

Kwanini hao? Sosi ya kuwaandika habari zao ni nini tena eti kuushi nini?


Hata jina lako haujaweka wanaowaka kusoma watakujuaje?
 
Hiki kitabu hakina tofauti na yale magazeti yanayouzwa kwenye meza ya magazeti mfano Utamu wa mtoto wa kitanga,ZEE LA NYETI,for future prediction umepotea.
 
Hiki kitabu hakina tofauti na yale magazeti yanayouzwa kwenye meza ya magazeti mfano Utamu wa mtoto wa kitanga,ZEE LA NYETI,for future prediction umepotea.

Sijapotea. It's actually very deep
 
Umefurahi sana,

Ila Ulipata ruhusa yao na pia je wanajua na kukubaliana na uliyoyaandika?

Kwanini hao? Sosi ya kuwaandika habari zao ni nini tena eti kuushi nini?


Hata jina lako haujaweka wanaowaka kusoma watakujuaje?

Suggestions nzuri, asante
 
Kujipendekeza nacho ni kipaji, unacho kipaji hicho, na yangekuwepo mashindano ya dunia ya kujipendekeza hakika ungeliletea taifa hili medali ya dhahabu.

Lol.. nashukuru nimepewa kipaji hiki
 
Back
Top Bottom