Kwanini ni Tndu Lissu na si Magufuli?

Kwanini ni Tndu Lissu na si Magufuli?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
1. MAGUFULI anayeng'ata na kupuliza. Anakwambia maendeleo Hayana chama huku anakashifu wananchi wa majimbo ya Upinzani wakimhoji.

2. Lissu ni mpambania ukweli na haki za watu hata kwa kuweka rehani Maisha yake.

3. Magufuli anasiasa za kuwafanya watu wote Kama wajinga, watoto. Ahadi hewa za mil.50 Kila Kijiji, laptop kwa walimu, nitaheshim katiba halafu yote hayatimizi.

4. Lissu akiahidi anatenda, wanasingida, Iramba pale wanajua alivyokuwa akiwapambania.

5. CCM imejaa kiburi, Kila mwanaCCM Sasa anajiona Ni Askari usalama wa taifa na kuoneaonea watu ovyo. Hawatufai.

6. CHADEMA wamewekeza katika nguvu ya umma, wao Ni watu wawatu na wataongoza kwa mamlaka ya watu. Hawa ndio wakwetu.

7. Miaka 5 ya Magufuli tumepigwa, tumetekwa, tumefungwa, tumebambikwa kesi, tumefirisiwa na uhuni mwingi tumefanyiwa. Sasa Basi hatumhitaji Tena, inatosha.

8. Lissu ni mhanga mwenzetu pia katika madhila hayo yote. Huyu ndiye atakayerejesha furaha na amanai ya mioyo tuliyoipoteza miaka 5 Sasa.

9. Magufuli anajiita injinia, yeye Ni mzee wa kupambana na vitu tu. Barabara na reli, ndege hata Kama watu wanakufa na njaa, matetemeko na majanga Hana time na wakihoji majibu yake kulia watatamani. Huyu jamaa hatufai kwakweli.

10. Lissu ni mwanasheria anayeshughulika na watu na amekuwa mtetezi wa wanyonge hata mahakamani huko wanaobambikwa kesi Lisu akiingia wanapata furaha. Sasa tumpe Ikulu Maisha yawe matamu Tena.

Ewe Mtanzania, ishinde njaa, ushinde uoga, pambania mgombea wako wa udiwani na Ubunge aliyeenguliwa kihuni arudishwe Mara moja. Mpigie kura Lissu na Linda kura yako isichakachuliwe.

Mwanahabari Huru
 
Vipi, wewe mbona hutembezi bakuli tutoe buku buku zetu, zile pesa zilizochangwa na wabunge kwa ajili ya uchaguzi kwa miaka 5 Mbowe amezificha wapi ?
 
Ni ukweli mtupu.....
Rais ni Tundu Lissu tumechoka matusi na masimango........
Ccm ni chama cha kishetani
 
Kuanzia 1-10, kwa nini ? Sababu Tundu kapigwa risasi, kwa hiyo tumchague kwa sababu kapigwa risasi? Tundu anastahili kupewa pole tu ya kupigwa risasi na siyo zaidi ya hapo, na pole tumeshampa, tena sana tu, hivyo hana deni na nchi yetu!
 
Huyu mpenda madege. Anayanunua kama fasheni apumzishwe kwanza. Tunataka hali bora za maisha siyo vitu bora.
 
Back
Top Bottom