Kwanini ni muhimu ku-restart simu yako angalau mara 1 kwa wiki

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Ni wazi kuwa smartphone zimekuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku kiasi kwamba pale simu yako inapokuwa imezima angalau kwa dakika chache unakuwa na wasiwasi wa kushindwa kufanya mambo yako ya kila siku.

Lakini ni kweli kwamba “kila kitu huchoka” nahisi hii ni sababu ya wewe kuendelea kusoma makala hii kama unataka kujua kwanini ni muhimu ku-restart au kuzima na kuwasha simu yako angalau mara moja kwa wiki. Pia kupitia makala hii nitakueleza ni kwanini ni muhimu kufanya hivyo hasa pale simu yako inapokuwa na matatizo mbalimbali ambayo nitakutajia kwenye makala hii, basi bila kupoteza muda twende kwenye sababu ya kwanza kabisa.

Husaidia Simu Kufanya Kazi Haraka

1573827666932.png


Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanatumia programu nyingi kwenye simu yako na ungependa simu yako iwe inafanya kazi kwa haraka zaidi basi ni muhimu kuzima na kuwasha simu yako angalau mara moja kwa siku au ukishindwa sana angalau mara moja kwa wiki.

Hii husaidia baadhi ya programu unazo tumia kuacha kutumia kiasi kIkubwa cha RAM mpaka hapo utakapofungua tena. Kama ulikuwa hujui, mara nyingi smartphone huwa na mtindo wa kutofunga programu kabisa na badala yake huifadhiwa programu husika kwenye memory (RAM) ili wakati mwingine unapo fungua programu hiyo iweze kufunguka kwa haraka. Mara nyingi kama umefungua programu nyingi kwa kipindi kirefu basi zote huwekwa kwenye memory na kufanya simu yako ichukue kiasi kikubwa cha RAM.

Kuzima na kuwasha simu yako husaidia programu hizo kufutwa kwenye memory (RAM) hadi hapo utakapofungua programu hizo kwa mara nyingine, hivyo ni muhimu kuzima na kuwasha simu yako angalau mara moja kwa wiki au mara moja kwa siku hasa kama unatumia programu nyingi kwenye simu yako.

Husaidia Programu Kama WhatsApp, Instagram na Facebook

1573827681917.png


Kama umekuwa ukikutana na matatizo mengi ya kushindwa kutumia programu yako ya WhatsApp, Instagram na Facebook basi ni wakati wa kujaribu kuzima na kuwasha simu yako. Programu hizo zinajulikana kwa kutumia kiasi kikubwa cha memory (RAM) kwenye simu yako hii ndio maana ni muhimu kuzima na kuwasha simu yako hasa unapokuwa unaona matatizo mengi kwenye App moja kati ya hizo.

Pia vile vile unaweza kujaribu kuondoa cache ya programu hizo kwani programu hizi zinakuja na mtindo ambao unawezesha programu hizo kuendelea kuwa na kumbukumbu ya matumizi yako kwa kipindi cha muda maalum, unaweza kuondoa cache kwenye moja kati ya programu hizo kwa kufuata hatua hizi.

1573827711286.png


Ingia kwenye Settings > Apps > “Chagua App unayotaka” > Storage > Clear Cache. Kumbukwa kwa kufanya hivi itakubidi kuingia tena kwenye akaunti zako kwa njia hii itaondoa data zote zilizo hifadhiwa kwenye simu yako. Kama unatumia simu za iPhone unaweza kufuata hatua hizo hapo chini.

1573827737828.png


Ingia kwenye Settings > iPhone Storage > “Subiri App zote zionekane kisha chagua app unayoitaka” > Offload App. Kwa kufanya hivyo utakuwa umeweza kuondoa Cache kwenye app hizo za instagram, Facebook na WhatsApp.

Husaidia Simu Kudumu na Chaji

Kama simu yako imekuwa na mtindo wa kuisha chaji haraka kuliko kawaida basi moja ya sababu ni hii ya kutokuzima kabisa simu yako. Hii husababishwa na jambo lile lile ambalo tumekua tukiongelea tokea mwanzo wa mada hii. Mara nyingi app huifadhiwa kwenye RAM hata baada ya wewe kuacha kuzitumia, sasa hii husababisha simu yako kutumia kiasi kikubwa cha chaji kuweza kuendasha RAM ya simu yako ili kusaidia programu hizo kuendelea kuweko kwenye RAM.

Source: Tanzania Tech
 
Back
Top Bottom