Mwanamageuko
JF-Expert Member
- Oct 31, 2010
- 8,602
- 5,570
Ndio maana nikasema kunahitajika fikra za ziada, ikiwa dogo hujalielewa je kubwa utalielewa??? Nilisema nanyi kwa mithali lakini sasa nimeamua kuwaweka wazi bado mnashindwa kuelewa??? enyi wana wa kizazi hiki:bowl:Kichwa Cha habari hakiendani na hoja ulizotoa,i weke kivivingine labda tutakusoma.Mtiririko mna mpangilio wa hoja utaleta hitimisho sahihi,ila kwa sasa hitimisho halina uhusiano wa kina na hoja zako
Ndugu:
Embu fikiria mtu unapewa pesa za kukusaidia kampeni wakati kampeni zimeshaanza, je kama ni kweli wana mapenzi na wewe kwanini hawakukupa miezi mitatu kabla? ukiwaza ukaenda mbali sana (wanapokupa wanataka hizo pesa mtoane nazo macho kwanza) kwa maana vyama vyetu hivi vinaishi kwa mizinga (watu kujitolea) na mikopo, inakuwaje pale waliowakopesha wakisikia kwamba kuna pesa mamilioni zimekuja???:A S angry:
Hili ndilo neno kuu hapa, neno la hekima, neno lililojaa likashiba. HAYO NDIO MAPAMBANO YA KWELI, Nyumba haianzwi kujengwa paa bali msingi wake. na msingi ukiwa imara ubora wa nyumba utaanzia hapo. Je wale wanaodai kuandamana na kudai haki kwa nguvu je wakishapata vilema wataidai tena???Jamani falsafa ni kuwa marafiki wakati mkitofautiana mitizamo!hata hivyo hoja za jamaa zipo makini.anatualika tufikiri mbali zaidi ya tunayoona kwa macho yakawaida na tunayosoma ama kusikia ama kunusa.ukihisi harufu ya mzoga unaenda mbele unajiuliza mzoga huu mbwa, mtu ama myama yupi?
Tena jk ni dikteta mbaya zaidi maana wajinga wengi wanaishia kumwona anachekesha uso wakaishia pale,beyond the smile kuna tatizo,visasi, unafiki,na ufisadi wa aina saba hadi kumi.tunayoona kwenye tume, kewnye uchaguzi huu na tutakayoshuhudia miaka hii mitano ni shule kubwa kabisa!haya tungoje tuone
lakini kama vyama vya upinzani ni vyetu, na tuvijenge sasa kuanzia serikali za vijiji, kata, halmashauri na later tukirudi kwenye election 2015 tutawapiga bakora mara tano ya hizi,tutapata wabunge 150 na uchaguzi wa rais tutagawana kura neck to neck!
Tupate pa kuanzia!
Nawasilisha
brother naheshimu mchango wako lakini uake ukitambua nchi yetu iko ktk transion period(kipindi cha mpito) katika safari za kisiasa ni kiutawala.unapokuwa na watu wenye elimu duni,uelewa mfinyu ni ngumu sana kuendesha siasa za ki mapinduzi maana hawa watu huwa wanaamini chochote wananachoambiwa na wanaowaamini hata kama si chanya.kwa mazingira hayo inakuwa ngumu sana sumaku kunasa chuma kilicho ndani ya ganda gumu la mbao.kuhakikisha tunajenga mfumo mzuri wa kidemokrasia na kisiasa lazima gharama zihusike katika mchakato mzima wa kufikisha elimu na ujumbe kwa raia walio wengi.vyama vingi havina ruzuku ya kufikia kujiendesha,hivyo mizinga na misaada inachangia kutufanya kufikia angalau lengo moja.vp basi jamii ya wasomi wakubali mabadiliko wakati jamii kubwa ya mbumbumbu wakikumbatia maradhi na uozo kwenye jamii.hivi ni vita na katika vita huchagui siraha,kikubwa ni ushindi na ushindi ni safari ndefu.lets join hands than being realistic than pesmistic.karibu tuendelee kujadilindugu:
Embu fikiria mtu unapewa pesa za kukusaidia kampeni wakati kampeni zimeshaanza, je kama ni kweli wana mapenzi na wewe kwanini hawakukupa miezi mitatu kabla? Ukiwaza ukaenda mbali sana (wanapokupa wanataka hizo pesa mtoane nazo macho kwanza) kwa maana vyama vyetu hivi vinaishi kwa mizinga (watu kujitolea) na mikopo, inakuwaje pale waliowakopesha wakisikia kwamba kuna pesa mamilioni zimekuja???:a s angry: