Elections 2010 Kwanini nayakubali matokeo......

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,602
5,569
:sad:
IKIWA VIONGOZI WETU (UPINZANI) HAWATAACHA UJUAJI WAO KATIKA WANAYOSHAURIWA, BASI TUTAENDELEA KUSINDIKIZA (daima) :thinking:

Jiulize maswali yafuatayo:

  1. kwanini mabango ya makampuni ya simu yabebe picha ya mgombea wa aina moja tu?
  2. kwanini promosheni za makampuni hayo zianze na kuishia wiki moja au mbili baada ya uchaguzi? (mnashangaa badala kutafiti) hapo pana zaidi ya hilo...
  3. kwanini yawawekee zawadi zinazotia tamaa ya kupata wakati mnapatwa? je kama ni kurejesha wanarejesha kweli?
  4. je kama Sabodo aliwapa CHADEMA kwa makelele milioni 100 je aliwapa CCM ngapi kimya-kimya? (haiwi umpe mtoto wa jirani ugali huku wako akilia njaa)
  5. hapo kuna mambo meeeeeengi ukishajiuliza hutopata majibu, mchakachuo + wao wanajua siku ya mwisho mtapiga kelele wee yataishia hapo wao wanapeta.
Ndio maana nimeamua kuyakubali matokeo yao huku nikiyapinga. Matokeo hayo ni ya ovyo kabisa. LAKINI WANASEMA FUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE.
Hawa viongozi wetu wajifunze la sivyo watasindikiza DAIMA, mwisho wa siku HESHIMA yao ITASHUKA. Jambo ambalo sitaki kabisa hata...:A S 114:

Ndio maana nahimiza watu KUFIKIRI kwa uwezo wao wote hapa sio kwenda kwenda tu na kupelekwa pelekwa:thinking:

;
 
Mkuu inawezekana unafikiria kwa upana kuliko wengine humu. Tulainishie basi hatua zichukuliwe.
 
Kichwa Cha habari hakiendani na hoja ulizotoa,i weke kivivingine labda tutakusoma.Mtiririko mna mpangilio wa hoja utaleta hitimisho sahihi,ila kwa sasa hitimisho halina uhusiano wa kina na hoja zako
 
Ndugu:
Embu fikiria mtu unapewa pesa za kukusaidia kampeni wakati kampeni zimeshaanza, je kama ni kweli wana mapenzi na wewe kwanini hawakukupa miezi mitatu kabla? ukiwaza ukaenda mbali sana (wanapokupa wanataka hizo pesa mtoane nazo macho kwanza) kwa maana vyama vyetu hivi vinaishi kwa mizinga (watu kujitolea) na mikopo, inakuwaje pale waliowakopesha wakisikia kwamba kuna pesa mamilioni zimekuja???:A S angry:
 
Kichwa Cha habari hakiendani na hoja ulizotoa,i weke kivivingine labda tutakusoma.Mtiririko mna mpangilio wa hoja utaleta hitimisho sahihi,ila kwa sasa hitimisho halina uhusiano wa kina na hoja zako
Ndio maana nikasema kunahitajika fikra za ziada, ikiwa dogo hujalielewa je kubwa utalielewa??? Nilisema nanyi kwa mithali lakini sasa nimeamua kuwaweka wazi bado mnashindwa kuelewa??? enyi wana wa kizazi hiki:bowl:
 
Ndugu:
Embu fikiria mtu unapewa pesa za kukusaidia kampeni wakati kampeni zimeshaanza, je kama ni kweli wana mapenzi na wewe kwanini hawakukupa miezi mitatu kabla? ukiwaza ukaenda mbali sana (wanapokupa wanataka hizo pesa mtoane nazo macho kwanza) kwa maana vyama vyetu hivi vinaishi kwa mizinga (watu kujitolea) na mikopo, inakuwaje pale waliowakopesha wakisikia kwamba kuna pesa mamilioni zimekuja???:A S angry:

crap
 
Jamani falsafa ni kuwa marafiki wakati mkitofautiana mitizamo!hata hivyo hoja za jamaa zipo makini.anatualika tufikiri mbali zaidi ya tunayoona kwa macho yakawaida na tunayosoma ama kusikia ama kunusa.ukihisi harufu ya mzoga unaenda mbele unajiuliza mzoga huu mbwa, mtu ama myama yupi?
Tena jk ni dikteta mbaya zaidi maana wajinga wengi wanaishia kumwona anachekesha uso wakaishia pale,beyond the smile kuna tatizo,visasi, unafiki,na ufisadi wa aina saba hadi kumi.tunayoona kwenye tume, kewnye uchaguzi huu na tutakayoshuhudia miaka hii mitano ni shule kubwa kabisa!haya tungoje tuone
lakini kama vyama vya upinzani ni vyetu, na tuvijenge sasa kuanzia serikali za vijiji, kata, halmashauri na later tukirudi kwenye election 2015 tutawapiga bakora mara tano ya hizi,tutapata wabunge 150 na uchaguzi wa rais tutagawana kura neck to neck!
Tupate pa kuanzia!
Nawasilisha
 
Nenda mbali zaidi, je u tayari kuiona Tanganyika ikiwa kama palestine??? Hujiulizi kwanini kazi ya IGP ilifanywa na mnadhimu wa jeshi?
Je wadhani mkiandamana mtakutana na FFU? waulizeni wazanzibari yaliyowakuta wakati ule? kwa kawaida askari wa kutuliza ghasia huishia barabarani mambo yakaisha! kule watu walitafutwa mpaka mvunguni:tape::A S angry: je kwanini wakuu wa mikoa takriban wote ni wajeshi??? jamani shime tufikirie hapo kisha....
 
Jamani falsafa ni kuwa marafiki wakati mkitofautiana mitizamo!hata hivyo hoja za jamaa zipo makini.anatualika tufikiri mbali zaidi ya tunayoona kwa macho yakawaida na tunayosoma ama kusikia ama kunusa.ukihisi harufu ya mzoga unaenda mbele unajiuliza mzoga huu mbwa, mtu ama myama yupi?
Tena jk ni dikteta mbaya zaidi maana wajinga wengi wanaishia kumwona anachekesha uso wakaishia pale,beyond the smile kuna tatizo,visasi, unafiki,na ufisadi wa aina saba hadi kumi.tunayoona kwenye tume, kewnye uchaguzi huu na tutakayoshuhudia miaka hii mitano ni shule kubwa kabisa!haya tungoje tuone
lakini kama vyama vya upinzani ni vyetu, na tuvijenge sasa kuanzia serikali za vijiji, kata, halmashauri na later tukirudi kwenye election 2015 tutawapiga bakora mara tano ya hizi,tutapata wabunge 150 na uchaguzi wa rais tutagawana kura neck to neck!
Tupate pa kuanzia!

Nawasilisha
Hili ndilo neno kuu hapa, neno la hekima, neno lililojaa likashiba. HAYO NDIO MAPAMBANO YA KWELI, Nyumba haianzwi kujengwa paa bali msingi wake. na msingi ukiwa imara ubora wa nyumba utaanzia hapo. Je wale wanaodai kuandamana na kudai haki kwa nguvu je wakishapata vilema wataidai tena???
 
ndugu:
Embu fikiria mtu unapewa pesa za kukusaidia kampeni wakati kampeni zimeshaanza, je kama ni kweli wana mapenzi na wewe kwanini hawakukupa miezi mitatu kabla? Ukiwaza ukaenda mbali sana (wanapokupa wanataka hizo pesa mtoane nazo macho kwanza) kwa maana vyama vyetu hivi vinaishi kwa mizinga (watu kujitolea) na mikopo, inakuwaje pale waliowakopesha wakisikia kwamba kuna pesa mamilioni zimekuja???:a s angry:
brother naheshimu mchango wako lakini uake ukitambua nchi yetu iko ktk transion period(kipindi cha mpito) katika safari za kisiasa ni kiutawala.unapokuwa na watu wenye elimu duni,uelewa mfinyu ni ngumu sana kuendesha siasa za ki mapinduzi maana hawa watu huwa wanaamini chochote wananachoambiwa na wanaowaamini hata kama si chanya.kwa mazingira hayo inakuwa ngumu sana sumaku kunasa chuma kilicho ndani ya ganda gumu la mbao.kuhakikisha tunajenga mfumo mzuri wa kidemokrasia na kisiasa lazima gharama zihusike katika mchakato mzima wa kufikisha elimu na ujumbe kwa raia walio wengi.vyama vingi havina ruzuku ya kufikia kujiendesha,hivyo mizinga na misaada inachangia kutufanya kufikia angalau lengo moja.vp basi jamii ya wasomi wakubali mabadiliko wakati jamii kubwa ya mbumbumbu wakikumbatia maradhi na uozo kwenye jamii.hivi ni vita na katika vita huchagui siraha,kikubwa ni ushindi na ushindi ni safari ndefu.lets join hands than being realistic than pesmistic.karibu tuendelee kujadili
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom