Kwanini nasema Mechi ya leo ya Simba SC na Ruvu Shooting FC itakuwa Ngumu japo tukishinda nitashukuru na Kufurahi pia?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
1. Wachezaji wa Simba SC kwa sasa 95% ya Akili zao zipo katika Mchezo wa Shirikisho utakaochezwa Jumapili huko nchini Niger dhidi ya FC Gendamarie.

2. Wachezaji wa Ruvu Shooting FC ambao 85% yao ni Wanajeshi wanajua kuwa Wachezaji wa Simba SC huwa ni Waoga na hawapendi Kugongana hivyo watakuja na Mkakati wa Kuwachezea Nginja Nginja ( Kikwatakwata ) hali ambayo inaweza kuipa wakati Mgumu Simba SC katika kupata Ushindi.

3. Kwa Mbinu ambazo Vilabu vingi vya sasa vya Ligi Kuu ya Tanzania NBC vimebuni pindi vikicheza na Simba SC hasa ya Kupaki basi na kutafuta Sare ( Draw ) inaweza pia Kutumika / Kutumiwa leo na Ruvu Shooting FC itakapocheza na Simba SC pamoja na Kuchanganya na hii ya Kucheza Nginja Nginja hivyo kuipa wakati Mgumu Simba SC kupata Ushindi.

4. Kwakuwa ni Mechi ya ASFC tena ya ( Knockout Stage ) wasiwasi wangu endapo Ruvu Shooting FC wakija na hii Mikakati Miwili ya Kucheza Pira Nginja Nginja na Pira Paki Basi na Mechi ikamalizika kwa Sare ( Draw ) tukienda katika Matuta ( Penati ) kwa Ubovu wa Upigaji Penati wa Wachezaji wa Simba SC na Hofu iliyowaingia baada ya Kuzikosa katika Mechi mfululizo sina uhakika kama Simba SC itafanikiwa na hapa ndipo naona utakuwa mwisho wa Simba SC kwa Kutolewa na Kulitema Kombe.

Simba SC tukishinda leo nitashukuru mno na nitafurahi sana, ila kwa Mazingira yaliyopo na ambayo nimeyaainisha nina wasiwasi mkubwa na hii Mechi hivyo Watu wa Saikolojia wafanye Kazi yao kwa Wachezaji wa Simba SC, Benchi la Ufundi na Wachezaji wa Simba SC waicheze kwa Umakini, Mkakati na wahakikishe wanashinda ndani ya dakika 90 tu na tusiende katika Penati ( Matuta ) kwani huko ndiyo tutaumbuka zaidi.

Nawatakia Mchezo mwema Klabu zote za Simba SC na Ruvu Shooting FC katika Mchezo wao wa Leo na naomba Amani itawale kwa Wachezaji na Mashabiki huku wakitupa burudani zaidi Sisi Watazamaji na yoyote atakayeshinda namtakia Kila Ia Kheri katika Hatua inayofuata ya Robo Fainali kama sijakosea.
 
Hivi kwanini timu nuingi zikicheza na Simba mbinu ni moja tu kupaki basi?
Sio timu zinazozocheza na Simba tu bali hizo ni game approach za timu yoyote ambayo inajiona ni underdog dhidi ya mwenzie. Hivyo anajua uwezo wa kucheza total football haiwezi hivyo jambo la kwanza ni kujilinda zaidi kwa kutoruhusu goli. Jambo la pili ni kushambulia kwa kustukiza pindi wapatapo mipira. Kifupi wanaingia kwa lengo la kuzuia kufungwa tu. Hata ulaya hizo mbinu zinatumika sana na hata kwa Tanzania pia tumeona mfano wa mechi za Yanga dhidi ya polisi na Mbeya city jinsi walivyopaki basi.
 
Popoma at work
IMG-20220131-WA0011.jpg
 
Mbeya city hakupaki basi wote ni mashuhuda.
 
Back
Top Bottom