Kwanini napinga hoja ya Waziri Nyalandu juu ya Wachina! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini napinga hoja ya Waziri Nyalandu juu ya Wachina!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Geza Ulole, Feb 6, 2011.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,047
  Likes Received: 3,953
  Trophy Points: 280
  Mi nafikiri ustaarabu unahitajika zaidi na si ubaguzi kwenye kushughulikia suala hili maana tutajikuta tuko kinyume hata na UN Resolution on Race and Human Rights though we have ratified the resolutions kwa vile tu tunaona kosa la Mchina ni kufanya biashara Kariakoo! Bila kuangalia weakness za sheria zetu na economic policies pia! Wakati katiba ya Tanzania inakataza ubaguzi, Waziri anatokea kusikojulikana na kuanzisha kampeni ambayo iko "wholly race oriented"! yaani pamoja na kuwa hawa wachina wamevunja sheria, huyu waziri anadiriki kuanzisha kampeni "kwa sababu Wachina wamevunja" na si kwa vile sheria zimevunjwa na kila anayefanya biashara kinyume na sheria?

  Tujiulize huyu Mchina ana tofauti gani na Mpakistan au M-bangladesh au Mhindi au Muafrika mwingine yeyote anayefanya biashara Kariakoo kama anacho kibali cha kufanya kazi? Je kuna Wapakistan, Waafrika na Wahindi wangapi wanafanya biashara au kazi bila vibali Tanzania? Kwanini media yetu inaliona tatizo ni specifically Wachina tu (why race identity is an vivid issue here?) na si kutokuwa na valid permits kufanya biashara? au violation of the given working permits?

  Ninavyoona jamii yetu sasa inaelekea katika ubaguzi uliokithiri! maana machungu ya maisha tulionayo tunabaki kuyaelekeza kwa wageni ambao wengi wao ni muhimu katika ushindani na kukua kwa biashara kiujumla! tunavyoelekea ipo siku tutahamia kwa Wapemba na Wachagga pia kama tatizo la kutopeleka mkono tumboni! Na kusahau chanzo cha yoote haya ni serikali husika haina incentives za kuweza kumsaidia machinga kushindana au wenye viwanda kuweza kuzalisha kwa bei nafuu! Tuamke jamani lets not be arose by cheap politics and become racists! Our anti-Chinese campaigns will cost us direly if we don't open up that pandora box that contains all the formula of our economic woos!

  Meanwhile while Mauritius is atracting massive investments from them foreigners through improving their Judiciary system and offering incentives (tax and so on) to investors that are the same as those offered to the natives! sie tunawafukuza kisa chuki na tumeshindwa ku-compete nao kwa vile serikali haisaidii chochote katika kuboresha biashara ya mwananchi wa kawaida as a proof of failed policies za Mijitu isiyo visionary na kutojua jinsi ya kutumia opportunities za influx of foreigners katika biashara na kuongeza mapato! Ngoja Kagame au Kibaki au Museveni wawakaribishe na jinsi tulivyo na common market watakuwa wanauzia bidhaa zao tokea Kigali, Kampala na Nairobi huku watumiaji wakipaki Dar! BTW, where are our economists? are our politicians all what we have?

  Raia wa kigeni leo kuondolewa sokani Kariakoo l Send to a friend Friday, 04 February 2011 20:35 0diggsdigg

  Festo Polea na Patricia Kimelemeta


  LEO serikali inaanza kazi ya kuwakamata wafanyabiashara wa kigeni wanaofanya biashara za umachinga, katika Soko la Kariakoo, kwa kuwa wanafanya kinyume na taratibu za kisheria.  Hatua hiyo, inatokana na Wachina hao, kufanya shughuli hizo, ambazo zinaweza kufanywa na Watanzania wazalendo na hivyo kusababisha wakose mapato.


  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Viwanda, Biashara na Masomo, Dk Cyril Chami alisema kazi hiyo, ni endelevu na kwamba inaanzia Dar es Salaam na kwamba itaendelea katika mikoa mingine nchini.


  Alisema, wakati shughuli hiyo, ikiendelea wananchi wanashauriwa kuwa wazalendo kwa kutoa taarifa polisi, pindi watakapoona raia yoyote wa kigeni, anafanya shughuli hizo.


  “Mipango wa serikali ni kuhakikisha wafanyabiashara wote, wanafanya kazi kwa kufuata taratibu na sheria zilizowekwa, ikiwa ni pamoja na kulipa ushuru,”alisema Chami.


  Alisema serikali itaendelea kutoa mafunzo kwa wajasiliamali wadogo ili waweze kumudu soko la ushindani.


  Kwa mujibu wa Chami, serikali itaendelea kufanya uchunguzi ili waweze kuwabaini wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao, kinyume na taratibu na kuwachukulia hatua za kisheria.


  Alisema, serikali itaendelea kutambua uwekezaji, uzalishaji wa biashara ili kuongeza ajira na kipato kwa wananchi wengi.


  Chami alisema pia Serikali, itaendelea kuwakaribisha wawekezaji wa ndani na nje kwa lengo la kukuza uwekezaji na biashara kulingana na sheria na taratibu za nchi.


  Chami alisema serikali, itahakikisha kila taasisi inayohusika na usimamizi wa sheria za kibiashara, inatenga fedha za kutosha kwa ajili ya kufuatilia shughuli za kibiashara.  Waziri serikali itajenga kituo cha biashara kwa ajili ya kurahisisha uingizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi na kudhibiti ubora wa bidhaa hizo.


  “Kingine ni kujenga kituo cha mauzo ya nje kwa ajili ya kurahisisha biashara ya Tanzania kuuzwa nje ya nchi,” alisema.

  Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
  [​IMG]
  [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  Last Updated on Saturday, 05 February 2011 11:03

  Raia wa kigeni leo kuondolewa sokani Kariakoo l
   
 2. m

  mpangwa1 JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2011
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 279
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  By my nature I hate Chinese and Indians wherever they are because of the way of exploitation. they don't participate in any way in community development why should we keep them. Let them just go......
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,047
  Likes Received: 3,953
  Trophy Points: 280
  can they also "hate" by nature your brothers and Sisters in Beijing and New Dehli? you are suffering from ethnocentrism...
   
 4. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,433
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Hii ni moja ya thread unayoweza kuiita 'crap' bila wasiwasi wowote! Mwamzisha mada hana uelewa wa kitu anachojaribu kutetea na anajikanyagakanyaga kwenye maelezo yake.
  1.UN Resolution on Race and Human Rights inasema unaweza kwenda nchi yeyote na ukafanya biashara au kazi yeyote bila kufuata sheria? Je unajua ni kwa nini wewe hapo Tanzania huwezi kwenda ubalozi wa Ujerumani na ukaomba resident permit ya kwenda kuishi ujerumani kwa kazi ya kupanga bidhaa dukani?
  2. Kama wahindi au wapakistani (ambao sio raia) wanafanya biasharasha ndio wahalalishe wageni wote kuja Tz kufanya umachinga? Dawa sio kuwaondoa wote?
  3. Wacha mawazo ya ki-nanga, na fikiri nje ya box!
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu.... kwa taarifa yako wachina hawana tofauti na wamasai kwa kukurupuka na kuhama hama wakiangalia wapi nyasi za mifugo yao zipo... nyasi zikiisha wanacha mbun'go na vinyesi pamoja na soil degredation.... wachina wanatumia ujanja wa kizamani usiotumia sheria halali za uhamiaji... utakuta mchina ana resident permit category ya work permit ambayo inasema yeye ni researcher wa gemstones lakini utamkuta kariakoo anauza piki piki au yebo yebo.... jee huyu mtu anafanya biashara kwa lengo halisi ya kibali chake cha uhamiaji... wapo wanaokuja kama accompanied family members wa construction firms halafu utawakuta wanaendesha migahawa maarufu kama china town...... tatizo kubwa hapa ni aina ya wachina wafanyabiashara wanao kuja hapa nchini...china sasa hivi biashara ni ngumu na wanahaha sana.....wachina ni wachafu... selfish na hawaheshimu culture na well being ya wazalendo.... they want their business succesful out of low cost of investment and resources contrary to existing economic temperature
   
 6. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,047
  Likes Received: 3,953
  Trophy Points: 280
  huoni kama kuna elements za ubaguzi maana kuna "race factor" that specifically determined the crack down exercise against Wachina! kwanini Mh Nyalandu asiamrishe uhamiaji wa-crack down 'everyone' that lacks proper living permit? au working permit or 'business licence'? kwanini ali-specify kwamba mapambano yake ni dhidi ya Wachina kufanya biashara k'koo vs Wamachinga bila kujali status yao? how do we know kwamba woote wameingia na permit za uwekezaji na si wengine walipata permit ya kufanya kazi na licence pia? ilhali tunajua rushwa za uhamiaji!

  Why specifically Chinese na si kila yeyote anayefanya kama Wachina? Hivi wewe ukiwa India halafu wakatoa habari ya namna hiyo hutalalamika? au umesahau jinsi Watanzania walio India walivyokuwa wanalalamika via Issa michuzi blogspot juu ya ubaguzi? na mbona China, Marekani na Ulaya kila mtu anaruhusiwa kufanya biashara as long as you have business licence na working permit? no matter what kind of business? as long as legal accepted! unajua hii nchi haiwezi endelea kama tunakuwa na shallow thinking kama yako! take Chinese guys as a competition na usianze ku-distort my argument! We can't shut out competition and survive in this era of Globalization...! We need to school our skewed excellencies otherwise cheap politics will erase us from the Economic World map!
   
 7. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,047
  Likes Received: 3,953
  Trophy Points: 280
  tatizo napinga the crack down to be only against Chinese and not all other law breakers that is RACISM! Crack all the people jamani tuache ubaguzi!
   
 8. L

  LAT JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu...pakistani au mhindi utamkuta na passport ya Tanzania...... hawa wachina inakua ngumu kutumia ujanja wa citizenship bearer .... hata hivyo extent ya illegal aliens wengine ni ndogo sana.....

  mkuu labda ushauri tuwafukuze na wakongomani..... sasa sebene tutalipata wapi...ha haaaa hii itakua ni Xenophobia
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Geza Ulole,
  Tatizo si ustaarabu au kukiuka kanuni za UN. Tatizo hawa Wachina hajawaomba visa kuja Tanzania kama wahamiaji. Wengi wamekuja kama watalii na wengine walikuwa wakifanya kazi za mikataba ya muda na wametumia mianya hiyo kujipenyeza nchini. Kwa hiyo ninachosema protocal za uhamiaji zifuatwe. Kama hawa Wamachinga wa kariakoo wangeomba visa kuja kufanya Umachinga ubalozi wetu Beijing usingewapa visa. Kwa hiyo wanafanya biashara under fraudulent circumstances. Kila nchi zina kanuni na sheria zake za uhamiaji na kama tusipokuwa waangalifu tutajikuta tumekuwa jalala la illegal immigrants kutoka China. Kumbuka kwao wako karibu bilioni moja.
   
 10. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2011
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Anacholalamikia Geza Ulole ni ubaguzi unao target watu fulani. Sheria zetu ndizo zenye udhaifu lakini sheria zinapotumika kiubaguzi huu ni ubaguzi na kinyume cha maadhimio ya kimataifa ambayo sisi tumeingia mkataba. Nyalandu alichofanya ni kutafuta cheap popularity na kwa kitendo hiki nadhani kama kungekua na rais makini angemkemea maramoja... Tunapo enforce laws -tagerting wachina tu nadhani huu ni ubaguzi!

  Pili serikali yetu imekua haina mikakati yoyote ya kuwaendeleza wafanya biashara ndogo ndogo badala yake imekua adui yao mkuu kwawanyang'anya mali na kwawinda. Nikichukua mfano ambo kwa sasa ni white elephant project ni Machinga Complex. Logic ya umachinga ni kuleta bidhaa karibu na walaji. Huwezi kumpeleka mmachinga anayeuza sigara kutoka mtaa uliopo na kumkusaanya kwenye soko lililombali na walaji. Kilichotakiwa kufanya nikuwa-register kuwapa maeneo kwa kadiri ya bishara zao na pia kupunguza msongamano na kuboresha vioski vyao na usafi wa mazingira yao na baada ya hapo kuwatoza kodi kutokana na mapato yao. Kama ni mama ntilie kuwakopesha majiko ya gesi kuwajengea vioski vyenye maji safi na kuwakagua mara kwa mara usafi na ubora wa vyakula vyao! Namna hiyo mtakipiga vita kipindu pindu na sio kwa kumwaga vyakula vyao kila siku, kila mwezi, kila mwaka. Nashangaa kama nchi hii ina watu wanaokabili matatizo kwa ubunifu.
   
 11. s

  seniorita JF-Expert Member

  #11
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Do you have any idea how those Indians and Chinese detest Africans na ni wabaguzi wakuu wa rangi hasa kwetu sisi Waafrika kuliko hata Westerners. Wakija huku wanajifanya wanatupenda ili waendelee kuneemeka from our resources; jaribu kufanya biashara kwao tena bila kibali!!!JAmani hapa Wahindi wanawafanya watu wetu hawa wawaoshe miguu!!!! I am against any kind of discrimination, being of race, gender, religion or otherwise. But this must not shut my eyes not to see who many Eastern races detest us Africans....So kama wachina wamepatikana wanafanya biashara bila kibali, sheria lazima ichuke mkondo wake...full stop. Haya kusema kuna wengine, then go and state those names/facts to responsible authorities; na ukisharipoti na kuona kuwa hakuna hatua iliyochukuliwa against them, then raise your voice and speak against racial discrimination...otherwise, wewe mto hoja, your comments are baseless
   
 12. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #12
  Feb 6, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  ni ubaguzi usio na maana na ambao hautaipeleka nchi hii mbele. Waje mradi wafuate sheria tu.
   
 13. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #13
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Hatuwezi kuwakumbatia wageni kuja kufanya biashara ya nyanya au kazi ambazo zinaweza kufanywa na Watanzania wenyewe hiyo ndio sera popote pale duniani. Hawa wote wanaosema ubaguzi wanaishi dunia ipi ... .. ... ... ya bulicheka?


  Kwanza serikali imechelewa.
   
 14. NOT ENOUGH

  NOT ENOUGH JF-Expert Member

  #14
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 526
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Geza ulole uwe una andika thread fupi na zinazoeleweka, na siyo ma thread yako marefu utafikiri watu wana kazi ya kusoma thread zako tu, Binafisi sijaisoma yote though najua umeandika mambo ya muhimu ila watu wako busy na kazi nyingine.
   
 15. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280

  Wawashughulikie na waliojipenyeza kwenye mgongo wa EAC hasa kutoka Kenya, Uganda, Somalia, Burundi na Rwanda. Wale wanaotaka kwenda kuishi Comoro waende tu. Hatukupigania uhuru ili machingas wa kigeni waje kuuza nyanya.
   
 16. B

  Bwagamoyo Member

  #16
  Feb 7, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mpaka wachina wafikie hatua ya kuuza kama wamachinga,watanzania wenyewe walikuwa wapi? watanzania ni wavivu bwana kazi kulalamika tu pembeni,kwa nini wasijaze nafsi hizo siku zote bila kuwapa wachina nafasi?wenzao wachina wamekuja tu na kuona loop holes wanazoweza kuzitumia, wakati waTz wenyewe wamelala, halafu mnasema Bongo land, wenzenu wachina ndiyo wanatumia bongo.
  Halafu suala la kuwafukuza ni sawa tu kama hawana kibali au wanafanya biashara kiharamu, sasa na wale akina dada zetu wanaoenda china na kufanya biashara kule nao wafukuzwe???

   
 17. Chimo

  Chimo JF-Expert Member

  #17
  Feb 7, 2011
  Joined: Aug 31, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 60
  Nadhani pia Serikali ingelitupia macho na hawa wapakistan wamejaa kama kanya punda na biashara yao kubwa wana link na Madawa ya kulevya lakini wanatumia kivuli cha kufanya biashara ya uingizaji wa magari mitumba toka. UAE Na Japan, Leo angalia Kawawa rd. Kuanzia kwenye mataa magomeni mpaka Morocco kuna zaidi ya showroom 20, za kuuza magari na karibia zote zinamilikiwa Na wapakistan hawajui hata kiswahili cha kuombea maji
   
 18. Companero

  Companero Platinum Member

  #18
  Feb 7, 2011
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  + Guangzhou & Bangalore
   
 19. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #19
  Feb 7, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kufanya crack down kwa wafanyabiashara kiholela ni sawa lakini kutamka kuwa unatarget Wachina si haki hata kama hicho ndo wanachofanya.
   
 20. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #20
  Feb 7, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,519
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  Ni kweli approach aliyotumia Mh. Lazaro Nyalandu ni ya makosa makubwa hasahasa ukizingatia hao wachina wenyewe hawafiki elfu kumi. Ilitakiwa Mh.Nyalandu awasiliane na Idara ya Uhamiaji kimya kimya kukagua viza na hati za kufanya kazi/biashara za hao Wachina mmoja baada ya mwingine bila kupiga makelele mbele ya waandishi au machinga wa Kariakoo. Maana wananchi wanaweza kujichukulia hatua mikononi kwa vile Waziri kasema na kuwadhuru raia wageni hata kabla ya kufahamu kama wageni hao walifuata sheria kufanya hizo shughuli Kariakoo na kwingineko.

  Waziri Nyakandu akumbuke Tanzania tunategemea misaada mingi ya serikali ya China kama TAZARA, Chuo Cha Ulinzi wa Taifa n.k hivyo kila tamlo analotoa Nyalandu aliangalie kwa mapana yake na marefu pia. Idara ya Uhamiaji ingeagizwa kufanya kazi yake kimya kimya kwa kufuata sheria za nchi yetu kuhusu wageni kujishugulisha na biashara. Tujikumbeshe tunavyopigwa jeki na serikali ya China ktk picha:
  [​IMG]
  Waziri wa Ulinzi na JKT Dk. Hussein Mwinyi na Meja Jenerali Qian Lihua kutoka nchini China wakikata utepe wakati wa makabidhiano ya Chuo cha Kikuu cha Kitaifa cha kijeshi (National Defence College) kilichojengwa Kunduchi jijini Dar es Salaam leo.
  [​IMG]
  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akiwa ameshikilia mfano wa funguo baada ya kukabidhiwa na Meja Jenerali Qian Lihua kutoka nchini China ikiwa ni ishara ya kumkabidhi chuo hicho.
   
Loading...