Kwanini Nape alishangiliwa katika mkutano wa UVCCM Dodoma?

Fitinamwiko

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
4,803
1,416
Nimesoma habari ya Mh Nape kushangiliwa alipoingia katika ukumbi wa Mkutano wa Uchaguzi wa viongozi wa UVCCM Taifa pale Dodoma.

Vijana waliamini uwepo wa Mh Nape katika uchaguzi ule, kwa kiasi kikubwa kungepunguza matumizi ya rushwa kwa wajumbe wa mkutano. Kama tunavyofahamu, ndugu Nnauye ni mmoja wa wahubiri wa kupinga falsafa ya UFISADI na MAFISADI ndani ya CCM. Baada ya Mh Nape kufanya lile Vijana wengi walilotegemea la kuwakabili watoa rushwa ambao walikuwepo meta chache toka mjengoni na wanajulikana, Nape alikimbiria jukwaani na kuchukua gitaa na kuanza kuburudisha wajumbe na kuweka mandhari muluwaa kwa watoa rushwa.

Kila siku nasema "Nape hajui kazi yake" alijua fika kulikuwa na mivutano pamoja na rushwa nje nje, kama angetimiza wajibu wake, kuangalia kitu gani kinaendelea, rushwa isingeshinda uchaguzi ule. Kwa Nape gitaa lilikuwa bora na kuwaangusha vijana wengi waliomtarajia, matokeo yake umoja unamegeka.

Kama wajumbe wangejua Mh Nape alikwenda mkutanoni kupiga GITAA na sio kuwakabili MAFISADI, je wangemshangilia?
 
nape ameshaufyta kwa lowassa na anajua lowassa ndo anapanga safu ya uongozi ndani ya ccm,hata hatima ya nafasi aliyo nayo nape hivi sasa iko mikononi mwa lowassa!
 
Si Nape huyu huyu alikuwa akishupalia EL ni GAMBA? Subiri tuone itakuaje huo mnyukano
 
Nape alishashindwa, kabakiza kula tuu ili kuepuka njaa. Sio nape tena wa enzi zile za jengo la uvccm Ilala. Huyu wa sasa ni kibaraka tuu wa EL, keshabadilika sana.
 
Tena EL anamtegemea sana huyu kijana katika mtandao wake. Si ajabu ndiyo aliyefanikisha ushindi wa kambi ya EL kwa kishindo.
 
Nape alishashindwa, kabakiza kula tuu ili kuepuka njaa. Sio nape tena wa enzi zile za jengo la uvccm Ilala. Huyu wa sasa ni kibaraka tuu wa EL, keshabadilika sana.
Kwenye siasa hakuna marafiki wala maadui wa kudumu. Mwanasiasa mzuri ni yule anayejua kusoma alama za nyakati. Nape sio mjinga hata kidogo.
 
sijui ni kwa nini walimshangilia lakini cha msingi ni kwamba mpaka tunafika hapa nape atakuwa ameshaelewa chama ni cha nani na kama bado basi amechelewa sana kwa vile sio kawaida. kwa uchaguzi wa vijana wa ccm nape ataelewa jinsi ambavyo watu huwa wanajipanga kwamba wanaweza kukushangilia halafu wakapuuza misimamo yako.
waliomshangilia walijua nape ANATAKA NINI LAKINI WAKAMPIGA CHINI
 
Nape alikuwa zamani, Vyeo vya kupewa vimemuua kisiasa amebaki kuropokaropoka na kuuza tu sura majukwaani.
 
Nimesoma habari ya Mh Nape kushangiliwa alipoingia katika ukumbi wa Mkutano wa Uchaguzi wa viongozi wa UVCCM Taifa pale Dodoma.

Vijana waliamini uwepo wa Mh Nape katika uchaguzi ule, kwa kiasi kikubwa kungepunguza matumizi ya rushwa kwa wajumbe wa mkutano. Kama tunavyofahamu, ndugu Nnauye ni mmoja wa wahubiri wa kupinga falsafa ya UFISADI na MAFISADI ndani ya CCM. Baada ya Mh Nape kufanya lile Vijana wengi walilotegemea la kuwakabili watoa rushwa ambao walikuwepo meta chache toka mjengoni na wanajulikana, Nape alikimbiria jukwaani na kuchukua gitaa na kuanza kuburudisha wajumbe na kuweka mandhari muluwaa kwa watoa rushwa.

Kila siku nasema "Nape hajui kazi yake" alijua fika kulikuwa na mivutano pamoja na rushwa nje nje, kama angetimiza wajibu wake, kuangalia kitu gani kinaendelea, rushwa isingeshinda uchaguzi ule. Kwa Nape gitaa lilikuwa bora na kuwaangusha vijana wengi waliomtarajia, matokeo yake umoja unamegeka.

Kama wajumbe wangejua Mh Nape alikwenda mkutanoni kupiga GITAA na sio kuwakabili MAFISADI, je wangemshangilia?

ya NGOSWE mwachie NGOSWE mwenyewe..wewe kama kijana msomi na muelewa bado uko ndani ya hicho chama unafanya nini? au na wewe unatafuta nafasi ya kufisadi?
 
Nimesoma habari ya Mh Nape kushangiliwa alipoingia katika ukumbi wa Mkutano wa Uchaguzi wa viongozi wa UVCCM Taifa pale Dodoma.

Vijana waliamini uwepo wa Mh Nape katika uchaguzi ule, kwa kiasi kikubwa kungepunguza matumizi ya rushwa kwa wajumbe wa mkutano. Kama tunavyofahamu, ndugu Nnauye ni mmoja wa wahubiri wa kupinga falsafa ya UFISADI na MAFISADI ndani ya CCM. Baada ya Mh Nape kufanya lile Vijana wengi walilotegemea la kuwakabili watoa rushwa ambao walikuwepo meta chache toka mjengoni na wanajulikana, Nape alikimbiria jukwaani na kuchukua gitaa na kuanza kuburudisha wajumbe na kuweka mandhari muluwaa kwa watoa rushwa.

Kila siku nasema "Nape hajui kazi yake" alijua fika kulikuwa na mivutano pamoja na rushwa nje nje, kama angetimiza wajibu wake, kuangalia kitu gani kinaendelea, rushwa isingeshinda uchaguzi ule. Kwa Nape gitaa lilikuwa bora na kuwaangusha vijana wengi waliomtarajia, matokeo yake umoja unamegeka.

Kama wajumbe wangejua Mh Nape alikwenda mkutanoni kupiga GITAA na sio kuwakabili MAFISADI, je wangemshangilia?
Mkuu, ngoma nzito, ametumia nguvu na juhudi zake lakini akaja gundua hapati sapoti yoyote chamani, na kwavile aliona madudu yaliyofanyika kule UWT, basi akaona liwalo na liwe, bora kupiga gitaa kuliko kujichosha na hizi rushwa. Tumsubiri nadhani atatoa tamko kueleza jambo hili ambalo tayari Mwenyekiti wake keshasikitika sana juu yaa rushwa iliyokubuhu katika chaguzi za chama chake.
 
Mh Nape kama msemaji wa CCM, mbona hautoi tamko kukanusha/kukemea matumizi ya rushwa au kuwapongeza washindi wa jumuia za Chama Taifa?
 
Alishangiliwa kwa sababu ni mahiri kwenye upigaji wa guitar.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hivi wandugu hizi rushwa ambazo zinajulikana watu wakishindwa tu uchaguzi, na wenyewe wanasema ziko nje nje, mbona mimi sielewi maana tuna simu za mikononi zenye camera nzuri zaidi ya mara 100 ya camera ya Muhidini Issa Michuzi ya miaka 5 iliyopita mbona hatuoni hata picha moja!!!

Mimi naona lililopo ni kuropoka tu, rushwa rushwa rushwa...
 
Back
Top Bottom