Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 19,147
- 43,079
Kwa wanawake wengi hujikuta wanapoteza hisia za mapenzi kwa mwanaume ambaye ni mwema sana,mpole sana, mstaarabu,hapendi ugomvi wala migogoro,mwanaume mwenye kuomba msamaha mara kwa mara hata kama makosa amefanya mwanamke,mwanaume mwenye kujitoa mhanga sana kubadilisha maisha ya mwanamke,mwanaume ambaye hana tabia mbaya zenye kukera kwenye jamii kama walivyo wanaume wengine.
Mwanaume mwema sana huwa hapendi ugomvi wala migogoro hivyo huwa kipaumbele chao ni kuhakikisha Mwanamke anakuwa na furaha,amani na utulivu,wanaume wengi wenye kujali sana huamini kwamba wanatakiwa kuhakikisha mwanamke anakuwa na furaha sana saa 24
Wengi hupiga simu mfululizo, kutuma sms mfululizo,kuomba msamaha hata kama hawajafanya makosa,wengi hupenda sana watoto na huwa wenye kuogopa sana watoto kukosa malezi ya baba na mama.
Wanaume wenye kupenda sana na kujali sana wengi huwa wanaogopa upweke,wengi huogopa mahusiano/ndoa kuvunjika,wengi huwa wanaumia sana pale ambapo wanakataliwa na Mwanamke hivyo wengi huanza kwa kujenga urafiki uliopitiliza kabla ya kumwambia Mwanamke wanataka kitu gani kisha huwa wanabaki na chuki, kinyongo, wivu uliopindukia pale ambapo mwanamke anapokuwa na mwanaume mwengine.
Wanaume wenye kujali sana huonyesha tabia zifuatazo
-Anataka ukaribu uliopotiliza na Mwanamke,anakuwa na wivu wa mapenzi kupindukia,
-Wakati mwingine huonekana king'ang'anizi sana
-hufanya vitu kwa shingo upande ili kuepuka kumkasirisha Mwanamke
-Wakati mwingine huanza kumpa Mwanamke vitisho vya kumuacha lakini anakuwa hana ujanja wa kumuacha isipokuwa anataka kunyenyekewa
-Huonyesha uvumilivu uliopotiliza hata Fumanizi za mara kwa mara na wengi hubambikiwa ujauzito kwa sababu ya kuonekana king'ang'anizi sana
-Anakuwa anataka kujua wapi Mwanamke alipo saa 24,kwa maana mwanaume anakuwa kama GPS kwa kumfuatilia Mwanamke
-Huwa anamsifia sana Mwanamke mara kwa mara utasikia "Siwezi kuishi bila wewe,Ukiniacha nitajiua","Sijawahi kuona Mwanamke mzuri zaidi yako dunia nzima "
-Kama sms hazijibiwi haraka hupata hasira kupitiliza kisha anapiga simu mfululizo na kutuma sms mfululizo, kujitumisha zawadi,kutuma sms kwa namba ngeni.
Nini hufanya Mwanamke kujuta sana baada ya kumuacha mwanaume mwenye kujali sana?
Mwanamke pale ambapo akijua unampenda sana kuliko mtu yeyote,akiona unamjali sana,unampa zawadi za gharama za mara kwa mara,akiona upo na hofu ya mahusiano kuvunjika kila siku anapotishia muachane moja kwa moja Mwanamke hupata uhakika kwamba hauwezi kumuacha hata akifanya makosa makubwa sana na vilevile hauwezi kuishi bila yeye.
Kitendo cha Mwanamke kujua kwamba yeye ndiyo kila kitu kwenye maisha ya mwanaume huanza kufanya vituko kama ifuatayo
-Kupuuza sms na simu kwa makusudi
-Atafanya makosa makubwa sana kwa makusudi kisha anageuza kibao kwa mwanaume
-Ataanza kutongozwa na wanaume wengine mbele ya mwanaume wake kwa makusudi
-Ataanza kuchati na wanaume wengine mpaka saa 8 za usiku na endapo akiulizwa anakuwa mkali kupitiliza
-Atagoma kupika, kufua, kufanya usafi wa nyumba,ataomba fedha nyingi sana kuliko uwezo wa mwanaume
-Anakuwa na hasira kupitiliza,ubishi, ukorofi, uchoyo, utemi,hatoi unyumba mpaka pale ambapo anajisikia yeye
-Anakuwa na safari za mara kwa mara kwenda nyumbani kwao kusingizia ananyanyaswa
-Akienda nyumbani kwao anakaa muda mrefu sana kinyume na makubaliano
Baada ya hapo akiona mwanaume anaomba msamaha,anapiga simu mfululizo, kutuma sms mfululizo, kujitumisha zawadi, kumbembeleza sana, kumkumbusha wema ambao amefanyiwa zamani badala ya Mwanamke kuona huruma kwa mwanaume kiburi, jeuri, majivuno na dharau huongezeka mara dufu kwa sababu anakuwa na uhakika kwamba hauwezi kumuacha hata akifanya makosa makubwa sana na vilevile hauwezi kuishi bila yeye.
Hivyo katika hali kama hiyo Mwanamke anaweza kubeba ujauzito wa ex wake au mchepuko wake kwa makusudi lengo amkomoe mwanaume ambaye anaonyesha kumpenda sana na kumjali kupitiliza.
Mwanamke anaweza kuuza mali za mume wake kisha anatokomea kusikojulikana
Endapo mwanaume kama alimfungulia biashara, kumchukulia mkopo, kumsomesha, kuwasomesha watoto ambao Mwanamke alizaa na wanaume wengine, kumkabidhi ATM card,kuandika majina ya Mwanamke kwenye mali za mwanaume ambazo Mwanamke hajachangia hata senti tano.
Basi Mwanamke akiona ameanza kupendeza, ameanza kusifiwa kazini au masomoni anamuacha mwanaume kwa makusudi kisha anakwenda kwa mwanaume wa HADHI yake.
Kisha akifika huko anakuta maisha ni tofauti
~Hakuna sms za mara kwa mara,hakuna faraja wala kuliwazwa
-Akifanya makosa habembelezwi anapokea kipigo ,matusi, kugombezwa, kufokewa, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kupelekeshwa, kufukuzwa nyumbani usiku wa manane.
Baada ya kuona amekonda, amepauka, ananuka jasho, amefubaa, hana dira yoyote ya maisha, ametelekezwa na ujauzito au watoto moja kwa moja akili yake inakumbuka kwamba kuna mwanaume alikuwa anampenda sana na kumjali lakini yeye alikuwa anamfanyia vituko kwa makusudi
Hapo akili yake humwambia akirudi kuomba msamaha, kusingizia shetani alimpitia atapewa nafasi nyingine na kupata faraja, kuliwazwa,kupewa mtaji ,kupewa matibabu.
Lakini kama akikuta mwanaume ambaye yeye alikuwa anamfanyia vituko ameoa Mwanamke mwingine huanza kulia,kujuta na kujilaumu.
Mwanamke anaweza kujuta kwa kumuacha mwanaume mwema endapo tu mwanaume mwema atakubali kuachika kisha mwanaume aoe Mwanamke mwengine kisha mwanaume apendeze,awe na furaha.
Lakini Mwanamke alimtelekeza mwanaume kisha akiona mwanaume anapiga simu mfululizo, kutuma sms mfululizo, kujitumisha zawadi, kumbembeleza arudi,kumuomba msamaha kwa upande wa Mwanamke badala ya kuona huruma anapata kiburi, jeuri,anakuwa mjuaji,anakuwa haambiliki, hashauriki, anakuwa na majibu ya mkato.
Njia pekee ya kukabiliana na Mwanamke ambaye hana shukurani ni ku-Move on na kuendelea na maisha mapya bila kufikiria kama Mwanamke asiekuwa na shukurani anaishi vipi.
Kufikiria kurudiana na Mwanamke ambaye hana shukurani husababisha mwanaume kutumika kama tambara la deki.