Nyerere pia alitaifisha majumba ya watu, mashule na hospitali kwa nia njema sio kwa nia ya kulikomoa kundi fulani katika jamii na kulinufaisha kundi lingine. Maamuzi haya yaliwajeruhi wakristo kwa waislamu lakini ilikuwa kwa faida ya sisi wote.
Nyerere kama binadamu alikuwa na mapungufu yake hakuwa malaika
Mbona Kikwete tunamlaumu sasa? Mapungufu ni mapungufu haijalishi yalifanywa na nani. Nyerere naye alifanya makosa mengi sana tu. Matatizo tuliyo nayo sasa kama taifa yeye ndiye chanzo kikubwa. Kama mwasisi wa taifa alishindwa kuweka misingi imara ya kuleta maendeleo, akatumia ujinga wa watanganyika kujiwekea uigo wa kutawala kiulauni bila kupingwa. Nadhani alitakiwa aweke misingi imara tangu mwanzo bila kujali u-naive wa watu wakati ule. Ndivyo kina Washington kule US walivo jaribu kufanya. Ni vigumu kumgusa Mwalimu, lakini pia hakututendea haki sana Watanganyika.
Aliwahi kusema katiba hii ilikuwa inampa nafasi ya kuwa dikteta! Sikuamini haya maneno yalitoka kwa mtu kama yeye. Yeye ndiye aliyesimamia utungwaji wa katiba hii 62 na 77. Kwa nini hakuweka misingi ya kuondoa udhaifu huu mkubwa kwenye katiba yetu. Alivotoka akahakikisha kaacha vipindi viwili tu kwa successors wake, kwa nini hakulifanya hilo mapema. Maana misingi ni misingi tu, haijalishi wewe ni nani.
Sina uhakika lakini kama ni kweli alitoa maamuzi ya kung'oa reli alifanya makosa makubwa sana. Huyu anayesema kinyozi haweki udobi kwa watu wenye vipara hana maadili kabisa. Kwani kwa vinyozi wananyoa nywele za kichwani tu? Inakuwaje kitongoji au mtaa mzima watu wote wasiwe na nywele? Huu ni upuuzi mtupu. Miundo mbinu ya kuunganisha nchi inajali tu kama una watu wanaishi pale. Madam watu wanaishi pale basi pasina shaka kuna shughuli zinazo waweka. Na ni haki kuwawekea miundo mbinu ya kurahisisha maisha yao.
Mambo ya kutenga nchi kihuduma ndiyo yanayopelekea Sudani ya kusini kujitenga. Tuitendee nchi yote kwa usawa. La kama tunashindwa basi tuikate kwa majimbo ili kila watu kwao wawe na serikari ya ndani ya kuendesha mambo yao.
Watanzania tukubali tunahitaji alternative power, a radical one which can bring the change we desire. Kufanya kitu kile kile kwa njia ile ile kwa wakati wote huku ukitegemea mabadiliko, utakuwa huna akili. Tunahitaji mabadiliko makubwa hii nchi, makubwa sana. Tunahitaji kufikiri tofauti na kutenda tofauti. Tunahitaji kujaribu, tusiogepe. Ndiyo dawa, Tuache Unyerereism, Umwinyiism, Umkapaism na Ukikweteism. Tunahitaji siasa mbadala. Staunch followers wa CCM should not worry, It is possible to have an alternative politics na nchi ikaenda tena vizuri sana. Wananchi tu wajue uwezo wao, kwamba mtu akiboa anatolewa, basi. Siyo CCM wanaboa halafu tunaogopa kuwaweka pembeni. Tuwaweke tu pembeni waone wengine wakifanya, wakirudi panapo majaliwa watajifunza.
RELI, BARABARA ZA KUUNGANISHA NCHI YOTE NA SIYO KUSINI TU NI MUHIMU KWA MAENDELEO YA TANZANIA.