Kwanini Mungu yupo?

Hopefully
Kwahyo Jibu lako ni kuwa binadamu hatuwezi kung'amua swali langu??
Kwanini hatuwezi? Je Quran imesema hatuwezi kung'amua swali langu?

Kama tumeumbwa kuabudu...kwanini tunaabudu? Mungu anapata faida Gani na ibada zetu?
mungu anatupenda tumwabudu kwasababu yy ni mwingi wa rehema mwenye wivu na hasira hana kubagua kwasababu wote ni wake amen
 
Maanake Mungu sio muumbaji wa kila kitu, kuna vitu vimekuja vyenyewe na yeye hana uwezo wa kuviumba
ukisema yeye unahisi Mungu ni personality kama wewe katika maumbile ya kimwili?
 
Mungu yupo kwa sababu yeye ndio sababu ya kuwepo kila kitu void,time,infinit, nothing and everything.All has come by him through him.Yeye ni source of anything and everything. Swali la msingi ni kwa Nini wewe upo? Who are you and why are you here.?

Wazungu wametengeneza James Web telescope kujaribu kutafuta majibu ya maswali Yao kwenye outer space.
 
Katika wachangiaji woote humu ndani, wewe pekee ndio umeongea point 👏na kwa point hii, huu mjadala naona ufungwe tu sababu mkuu umemaliza kila kitu, binadamu hakuna tunachokijua kuhusu ulimwengu huu ilichobakia tunarukaruka tu assumptions and imaginations nyiingi
 
Hauwezi kuujua ulimwengu sababu mwenye ulimwengu wake YUPO.
Na Kuna mambo ametuficha makusudi kuonesha uwezo wake.

ndo maana qnasema ninyi wote ni viumbe vyangu,kwangu mmetoka na kwangu mtarejea na nitawahukumu.
Pia anasema sikuumba binadamu na majini ila WANIABUDU
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Iv unakumbukumbu ata moja kama ulishawahi kuwa na mungu afu akakuleta apa duniani?
 
Hakuna kitu tulichofichwa bana... miaka 700,000 iliopita dunia ilikua na viumbe tofauti kabisa waliopo sasa.

Binadamu hatukua hivi kama tulivo. Kumaanisha kwamba hatukuumbwa siku ya 6. Kumaanisha kwamba hakuna anae control maisha hapa duniani kwahio hakuna MWENYE huu ulimwengu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hakuna mwenye ulimwengu.huu ulimwengu umetoka wapi?
 
Yupo

Kwa lugha nyepesi hamna jibu kama vile hamna jibu kwamba Mungu alitokeaje? Uumbaji ni kwa sababu Yeye Yupo na aliamua kwa mapenzi yake kuumba vitu vyote, ila sii kwamba yupo ili aumbe. angeweza kuwepo bila kuumba chochote kile. Hakuna Sababu iliyomshurutisha akawepo. Uwepo wa Mungu hauhitaji sababu yoyote ile.

Yeye yupo siku zote bila Mwanzo wala Mwisho. Sisi tunasababu ya kuweko kwa sababu kuna aliyetuumba na ana sababu zake za kutuumba.

Ila Mungu hana wa juu yake ambaye alimpa Sababu ya kuweko, ama aliyemwanzisha kwa kusudi fulani.
 
Hakuna Mungu isipokuwa Allah tu.
 
Wewe upo? Kwanini upo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…