Kwanini mtu anatoa machozi akiwa anasali?

Kinau Michael

Member
Joined
Aug 18, 2023
Posts
13
Reaction score
15
Hallow ndugu zangu nimeulizwa swali kwanini mtu akiwa katikati ya Ibada huwa anatoa machozi? Je anajuta, ni uchungu kwa anayoyapitia au ni imani sana?

Naomba nisaidieni majibu
 
Wanaolia ni walokole! Hiyo ni desturi yao
Ukiomba bila kulia au kutoa sauti unaonekana hujapandwa na roho mtakatifu.
Pia ukiwa kanisani ukiomba kwa kulia na kutoa sauti unaonekana wewe ni mtakatifu zaidi ya wote hapo ibadani.

Wengine wanalia kwa kukumbuka matatizo yao, hela ya kula hana anamuomba Mungu ampe.
 
Mimi ni catholic,kuna mda madhira yananikaba hadi najisikia kupiga mayowe kati Kati ta misa 🤣🤣🤣
 
Ukiwa unasali unaweza kulia kwasababu ya imani kua juu sana au yale matatizo uliokua nayo unayomuomba mungu akuondolee au kitu fulani ambacho huna unamuomba mungu akupe ndo unakuta mtu analia kwa nguvu zote akiamini mungu anamuona atamsadia

Bila shaka mtoa mada umeelewa?
 
Kusoma kwa lengo la kufaulu mitihani pekee hujikita kwenye kukariri maneno, fomula, na nadharia ili kupata alama za juu na vyeti, lakini maarifa hayo husahaulika haraka baada ya mtihani kukamilika.

Mtindo huu wa elimu ya makaratasi haumsaidii mwanafunzi kufikiri nje ya boksi, haumjengei uwezo wa kubuni suluhisho la changamoto za maisha, na unamwacha akiwa mtumwa wa kufuata maelekezo ya wengine bila kuhoji.

Tofauti na hapo, kusoma na kuelimika hubadili kabisa fikra, tabia, na mtazamo wa mtu; kunamjengea uwezo wa kuchambua mambo kwa kina, kutatua matatizo ya jamii, na kutumia unyenyekevu wa maarifa aliyonayo kupata busara inayodumu maisha yake yote hata baada ya kusahau mambo mengi ya darasani.Ukweli huu unadhihirika wazi tunapotazama baadhi ya watu wenye rundo la vyeti na shahada nyingi—kuanzia ma-masta hadi ma-PhD—lakini uelewa wao wa maisha, utu, na uhalisia wa mambo ni sifuri kabisa.

Watu hawa mara nyingi hutumia vyeo vyao vya kitaaluma kama ngao ya kuficha upungufu wao wa hekima, wakitaka kila mtu awasujudie na kuwaona miungu watu kwa sababu tu wana herufi nyingi mbele ya majina yao.

Huwa na tabia ya dharau, kushindwa kusikiliza maoni ya wengine, na cha kusikitisha zaidi, hawawezi kutumia usomi wao mrefu kutatua hata tatizo dogo la kijamii linalowazunguka; wanabaki kuwa "maktaba zinazotembea" ambazo zimejaa nadharia zisizo na tija huku wakiongozwa na mihemko na ubaguzi.Kundi hili la wasomi wa vyeti pekee huishia kuwa mzigo kwa jamii kwa sababu akili zao zimefungwa ndani ya kuta za madarasa waliyosoma na haziwezi kufanya kazi kwenye ulimwengu wa kweli. Wana uwezo mkubwa wa kunukuu vitabu vya wanafalsafa wa Ulaya au kutaja fomula ngumu za hesabu, lakini ukila nao meza moja, utagundua hawana uwezo wa kufanya maamuzi ya msingi ya kijamii, kiuchumi, au hata ya kifamilia.

Hali hii inathibitisha kuwa shule inatoa fursa ya kupata taarifa, lakini uelimikaji unahitaji utayari wa mtu binafsi kutumia taarifa hizo kwa busara, unyenyekevu, na kwa faida ya watu wengine, jambo ambalo vyuo vikuu havina mtihani wa kulipima.

Mwisho wa siku, jamii inapaswa kutambua kuwa mtu aliyelimika bila vyeti ni wa msaada mkubwa zaidi kuliko msomi mwenye shahada tano asiyekuwa na uelewa wa kiutu wala kiutendaji. Elimu ya kweli haipimwi kwa urefu wa wasifu wa mtu (CV) au idadi ya kofia anazovaa siku ya mahafali, bali inapimwa kwa uwezo wake wa kuleta amani, maendeleo, na majibu ya matatizo yanayoikabili jamii yake.

Tunahitaji kubadili mtazamo wetu na kuacha kuabudu makaratasi ya shule, na badala yake tuanze kuthamini na kukuza uelewa wa kweli, utu, na fikra tunduizi ambazo ndizo nguzo kuu zinazomtofautisha genius mwenye hekima na mtu mwenye vyeti lakini asiyeelimika.
 
Wanaolia ni walokole! Hiyo ni desturi yao
Ukiomba bila kulia au kutoa sauti unaonekana hujapandwa na roho mtakatifu.
Pia ukiwa kanisani ukiomba kwa kulia na kutoa sauti unaonekana wewe ni mtakatifu zaidi ya wote hapo ibadani.

Wengine wanalia kwa kukumbuka matatizo yao, hela ya kula hana anamuomba Mungu ampe.
Hii nimeipenda:
"Wengine wanalia kwa kukumbuka matatizo yao, hela ya kula hana anamuomba Mungu ampe".
Halafu Mungu hampi. Hapo lazma mlokole chozi limtoke.
 
Kusoma kwa lengo la kufaulu mitihani pekee hujikita kwenye kukariri maneno, fomula, na nadharia ili kupata alama za juu na vyeti, lakini maarifa hayo husahaulika haraka baada ya mtihani kukamilika.

Mtindo huu wa elimu ya makaratasi haumsaidii mwanafunzi kufikiri nje ya boksi, haumjengei uwezo wa kubuni suluhisho la changamoto za maisha, na unamwacha akiwa mtumwa wa kufuata maelekezo ya wengine bila kuhoji.

Tofauti na hapo, kusoma na kuelimika hubadili kabisa fikra, tabia, na mtazamo wa mtu; kunamjengea uwezo wa kuchambua mambo kwa kina, kutatua matatizo ya jamii, na kutumia unyenyekevu wa maarifa aliyonayo kupata busara inayodumu maisha yake yote hata baada ya kusahau mambo mengi ya darasani.Ukweli huu unadhihirika wazi tunapotazama baadhi ya watu wenye rundo la vyeti na shahada nyingi—kuanzia ma-masta hadi ma-PhD—lakini uelewa wao wa maisha, utu, na uhalisia wa mambo ni sifuri kabisa.

Watu hawa mara nyingi hutumia vyeo vyao vya kitaaluma kama ngao ya kuficha upungufu wao wa hekima, wakitaka kila mtu awasujudie na kuwaona miungu watu kwa sababu tu wana herufi nyingi mbele ya majina yao.

Huwa na tabia ya dharau, kushindwa kusikiliza maoni ya wengine, na cha kusikitisha zaidi, hawawezi kutumia usomi wao mrefu kutatua hata tatizo dogo la kijamii linalowazunguka; wanabaki kuwa "maktaba zinazotembea" ambazo zimejaa nadharia zisizo na tija huku wakiongozwa na mihemko na ubaguzi.Kundi hili la wasomi wa vyeti pekee huishia kuwa mzigo kwa jamii kwa sababu akili zao zimefungwa ndani ya kuta za madarasa waliyosoma na haziwezi kufanya kazi kwenye ulimwengu wa kweli. Wana uwezo mkubwa wa kunukuu vitabu vya wanafalsafa wa Ulaya au kutaja fomula ngumu za hesabu, lakini ukila nao meza moja, utagundua hawana uwezo wa kufanya maamuzi ya msingi ya kijamii, kiuchumi, au hata ya kifamilia.

Hali hii inathibitisha kuwa shule inatoa fursa ya kupata taarifa, lakini uelimikaji unahitaji utayari wa mtu binafsi kutumia taarifa hizo kwa busara, unyenyekevu, na kwa faida ya watu wengine, jambo ambalo vyuo vikuu havina mtihani wa kulipima.

Mwisho wa siku, jamii inapaswa kutambua kuwa mtu aliyelimika bila vyeti ni wa msaada mkubwa zaidi kuliko msomi mwenye shahada tano asiyekuwa na uelewa wa kiutu wala kiutendaji. Elimu ya kweli haipimwi kwa urefu wa wasifu wa mtu (CV) au idadi ya kofia anazovaa siku ya mahafali, bali inapimwa kwa uwezo wake wa kuleta amani, maendeleo, na majibu ya matatizo yanayoikabili jamii yake.

Tunahitaji kubadili mtazamo wetu na kuacha kuabudu makaratasi ya shule, na badala yake tuanze kuthamini na kukuza uelewa wa kweli, utu, na fikra tunduizi ambazo ndizo nguzo kuu zinazomtofautisha genius mwenye hekima na mtu mwenye vyeti lakini asiyeelimika.
Kongole mkuu kwa udadavuaji mahiri.
 
Amepagawa. Kupagawa sio kitu kibaya kivile. Kuna watu wanalilia timu za mpira, wengine mapenzi nk.
 
Mimi ni catholic,kuna mda madhira yananikaba hadi najisikia kupiga mayowe kati Kati ta misa 🤣🤣🤣
Hivi hizo ibada za kikristo ni ibada/Sala kweli?.. maana watu wamekaa kwenye mabenchi padre anapiga show,watapiga magoti padre ataongea,watainuka,wataenda kula mkate kwa foleni

Wale wengine ni makelele tu kana kwamba Mungu wao kiziwi,muziki watacheza dansi,watarudi nyumbani,hapo mtu kinakuliza nini!?
 
Unavo Judge utafikiri Wanakuabudu wewe, Kumbe wana abudu kwa Mungu wao.
 
Watu wengi walioshika sana dini wana matatizo ya akili.
 
Back
Top Bottom