Kwanini mtu akifeli kimaisha anakuwa "sadist"

Kwanini mtu akifeli kimaisha anakuwa "sadist"

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
6,364
Reaction score
15,148
Hali hii mara nyingi naiona hasa kwa watu wazima wenye umri kuanzia miaka 40 na kuendelea, unakuta kapambana sana hapo nyuma Kuna fursa alizipata akazichezea matokeo yake anakuwa na hali flani mbovu ya kiuchumi .

Sasa kinachokuja kutokea hapa kila atakaekuwa anakutana nae na anapitia maumivu flani basi utamuona sura yake inakuwa na bashasha au tabasamu pana. Sidhani kama hiyo hali inawasaidia .
 
Hali hii mara nyingi naiona hasa kwa watu wazima wenye umri kuanzia miaka 40 na kuendelea, unakuta kapambana sana hapo nyuma Kuna fursa alizipata akazichezea matokeo yake anakuwa na hali flani mbovu ya kiuchumi . Sasa kinachokuja kutokea hapa kila atakaekuwa anakutana nae na anapitia maumivu flani basi utamuona sura yake inakuwa na bashasha au tabasamu pana...sidhani kama hiyo hali inawasaidia .
Sadist ni namna ya yeye ku cope na failure yake, in his head ili asiumie lazima washushe katika level yake, and that how wanaponda kila kitu
 
90% hakuna binadamu anaependa mipango yako ifanikiwe ndio maana kila mipango uliyowaeleza watu kabla haijatimia kamwe haitimii , mara nyingi waliofanikiwa walifanya mambo kimyakimya watu wakaona matokeo tu, na kwenye utafutaji ukiwa na tamaa ya kupata na kujilinganisha na wengine kamwe hutapata , ndio maana wamiliki WA pesa ndefu wapowapo Tu wasiri na wenye akili ya kutulia maana pesa haikai kwa mwenye papara
 
MAISHA ni nini? Mtu akitumia Pesa na Rasilimali zake wanasema anachezea maisha. Na wengine humwambia 'huyajui maisha'. Na akianguka anaambiwa ALICHEZEA MAISHA.
MAISHA NI NINI??
Maisha ni hadithi yenye Pande mbili furaha na huzuni na hadithi hiyo hukamilika pale unapoondoka duniani wewe kama wewe na lazima utapitia Pande zote hivo mambo yakikunyokea usishangae na yakienda kombo usishangae fahamu ndio hadithi yako hiyo ambayo itaisha ukifa na kubaki wakisimulia wanaobaki kulingana na alama za masimulizi yako
 
Kufeli kwa kujitakia kunapelekea mtu kutafuta walio wake. lkn kufeli kwa kufelishwa na watu kunatengeneza hasira na kisirani kibaya na wengi huishia kulaumu na kuishia maamuzi mabaya!!!!
Waliochezea nafasi huishia kutoa ushauri kwa wafuatao njia zao. Tujifunze kuwapa ushauri wa kupenda kusubiri!!!!!

aaaa mi sijui nilichokiandika!
 
Hali hii mara nyingi naiona hasa kwa watu wazima wenye umri kuanzia miaka 40 na kuendelea, unakuta kapambana sana hapo nyuma Kuna fursa alizipata akazichezea matokeo yake anakuwa na hali flani mbovu ya kiuchumi . Sasa kinachokuja kutokea hapa kila atakaekuwa anakutana nae na anapitia maumivu flani basi utamuona sura yake inakuwa na bashasha au tabasamu pana...sidhani kama hiyo hali inawasaidia .
Mbona hata shule ya msingi tulikuwa tunaoneana wivu. Hiyo ni hulika ya binadamu wote regardless of age
 
Maisha ni hadithi yenye Pande mbili furaha na huzuni na hadithi hiyo hukamilika pale unapoondoka duniani wewe kama wewe na lazima utapitia Pande zote hivo mambo yakikunyokea usishangae na yakienda kombo usishangae fahamu ndio hadithi yako hiyo ambayo itaisha ukifa na kubaki wakisimulia wanaobaki kulingana na alama za masimulizi yako
Maisha ya mwanadamu ni hadithi Tu ...rip alhasan mwinyi
 
Back
Top Bottom