Laana, Mizimu, Roho, Vifungo na Madhabahu katika koo na jinsi vinavyowatesa wengi kimaisha

Eli Cohen

JF-Expert Member
Jun 19, 2023
1,309
4,017
Ndugu zangu naelewa kila mmoja anapitia ya kwake kimaisha na kila mmoja anafahamu historia ya safari ya mapito ya ukoo wake.

Tambueni kuwa kuna kero na karaha nyingi za kujirudia zinazotesa koo nyingi. Na inafikia wakati hadi matatizo haya yamekuwa ni ya kuzoereka kutokana na kuchukulia poa au kutokuwa na umoja wa kujaribu wa kuyatatua madhira hayo.

Kinachofatia ni kuhangaika kwa waganga, wachungaji feki, mashehe watoa majini, kurushiana lawama za kulogana baina ya ndugu, etc.

Laana inarithika katika vizazi, laana inasaka wapi pa kutua ili ijitukuze, kwa maana bado inalilia damu ndani yenu kutokana na uchungu uliofanyika na mababu au mabibi zenu kwa watu wengine.

Madhabahu yaliyowekwa na mababu yalijitengeneza kiroho ndani ya ukoo na sasa yakaangaza na kukaa enzi na enzi. Madhabahu hayo yalifanyika katika matambiko ya kishirikina au kuenzi mizimu. Kuumaanisha walikaribisha roho hizo ziweze kuangaza ndani ya damu na vizazi vya ukoo.

■Kuna koo ambazo unakuta wanawake karibia wote wanapitia mateso ya ndoa. Hii unakuta kuna bibi aliwahi kufanya kitu kibaya na wakamlaani yeye na kizazi chake.

■kuna koo unakuta mabinti wanasumbulia na mizimu ya kuagua na uganga eti kisa bibi zao walifanya hivi.

■kuna koo unakuta kuna roho ya visasi na kufanya mauaji inatembea ndani yao. Yani hawakuachi hivi hivi lazima wakufanyie damage ndio walidhike hata kama ni mwanae amemkosea pakubwa.

■kuna koo unakuta majina flani wakipewa watu wanakuwa wafuska sana kwa sababu mtu huyo nae alikuwa mfuska.

■Kuna koo unakuta watu wengi hawana vibali vya kukubalika, anapiga kazi sana, anaona vimatunda lakini ghafla mambo yanasambaratika tena anaanza upya kwa kujitafuta. Hii unakuta kuna watu babu zao waliwafanyia ubaya na wakawanenea maneno ya laana kwa uchungu.

■kuna koo unakuta umoja hakuna. Ni fitna, kufanyiana uchawi, husda na vinyongo vibaya.


Mtu wa kawaida anaweza kusema haya ni mambo ya kawaida kutokana na mapito ya maisha, lakini ni kwa sababu hajapitia tabu hizi na hajashuhudia kiuhalisia jinsi gani kuna jamii ambazo matatizo yao ni sugu na ya kujirudia.

Na matatizo haya sio mapitio ya kila siku ya maisha bali ni mapitio ya uzamani ulioharibika na kurithiwa ndani yao. Tatizo ni kuwa hakuna wa kusaidia kwa maana kila mtu unakuta na yeye ana miroho ndani yake, yani unakuta moto unakutana na moto. Ila kuna wale mnaopata mwanga kidogo, mjifunze kukemea hizi roho kwa imani yenu binafsi na kwa usaidizi wa watumishi wa Mungu wa wazuri na huku ukitanguliza sadaka ya kuikomboa familia yako.
 
Mkuu umeona mbali sana kwani haya mambo tunayaishi sana, nitakupa mf nina ndg zangu wakike wote wameishia kuzalishwa na wanaume ingawa kuna mmoja aliolewa kabisa lakini nwisho wa siku muoaji akatokea kumchukia na hatimae akamsingizia kaiba hela hivyo akadai kwamba hawezi kuishi na mwanamke mwizi na ukifikiria tayari alishamzalisha mtoto mmoja, huyu mwingine nayeye kazaa na mwaname wa dini tofauti na yeye pasi kujua maskini na ukiangalia familia ya yule jamaa ni wadini kinoma, basi wakatafuta visababu vya kumuweka pending mwenzangu namie mpaka sasa hakuna cha ndoa wala nini na mimba walimjaza mpaka kajifungua yupo tu hapo home analea Mtoto na anaamini ipo siku ataolewa na jamaa kumbe mwenzangu namimi hana time nae tena.dada yetu wa kwanza alizaa na mume wa mtu hiyo nayo ilikua ni shida nyingine

Sasa ulivyoandika hivi nimejikuta nafumbua macho kuona yaliyowakuta hawa ndg zangu siyo ya kawaida

Ingawa hata mimi pia kila ninapoianza safari ya mapenzi, kila Meli inapong'oa nanga inageuka ferri mtomvi. Yaani nakua ni mtu wakuumizwa tu kila wakati.
 
Kuna watu Lindi waliambiwa mizimu haitaki wamiliki hata kiwanja.
watoto wa familia ile walikuwa na elimu na kazi nzuri ila wooote walikufa wakiwa wameuza Kila kitu na kuwa wa kulala mitaan
The same style ya kushambuliwa kwa watoto wote na vifo pia vilifanan
 
Kweli mkoloni kakufanya Mtumwa wa Milele. Babu zako ambao walitunza Babu zako na Baba yako mpaka wewe ukazaliwa unawaita Mashirikina na Mashetani? Yaani unaamini Mungu aliyeletwa na Wakoloni kwenye Jahaazi la kubebea Watumwa? Unawakandia Wazee wako kisa stori za Uongo za kwenye vitabu vya Uongo? . Siku mkitambua kuwa Mungu wa kweli anapatikana Afrika na Anafanya matukio live ndiyo Mtaacha kusifia hizo Imani za kitumwa. Ebu fikiri Mtu hana Mtoto anafinyiwa tambiko kwa Mganga Majibu yanatoka baada ya muda Mfupi Mama kapata Mtoto eti unamuita Mtoto wa dawa halafu akifanya Shekh au Mchungaji bila mafanikio husemi kitu .

Yaani Mtu anadanganywa na Imani za kutunga kama Adama na Hawa,Safina ya Nuhu, Stori za Ruthu. Hivi nyie Watu mnawaza sawasawa kweli?

Unaambiwa mke wa Nuhu alipogeuka nyuma aligeuka kuwa mwamba wa Chumvi swali Nani aliona amegeuka mwamba chumvi? .Eti wanyama wote walipanda safina hivi simba alikula nini kwa hizo siku zote ndani ya safina? Samsoni alimuua Simba jangwa la la Palestini hivi kweli Simba huwa anaishi Jangwani? Eti waisrael walikuwa Watumwa Misri hivi kweli nyie Mnaamini hili? Sasa kilitokea nini Mpaka Waafrika wageuka wao ndiyo Watumwa? Stori kama kuvuka bahari ya shamu kwa siku moja tu km 1400 lakini km 700 zimewachukua miaka 40 ? .Wewe Muafrika Mwenzangu Heshimu Bibi na Babu zako acha zarau maana ndiyo wenye Spiritual power zidi yako na Wana DNA yako moja kwa moja. Fuata mila zenu ufanikiwe acha kuigiza ukweli kabisa Ustaraabu wa Wageni huwezi kufanikiwa maana kule kwao wanakuona ni Mtumwa tupu .
Hayajakukuta na hujawajua watu wewe
 
Hayajakukuta na hujawajua watu wewe
Mungu wa Afrika hasomwi vitabuni anafanya kazi moja kwa moja miujiza yake ni kweli kabisa sasa angalia huko Palestina Wanamuomba allar bado wanakufa kama takataka .Mungu hayupo kwenye Dini Mungu wa Mtu Mweusi anatisha Directly utasema uongo kanisani utasema uongo Msikitini lakini huwezi sema uongo kwenye kilinge cha Waganga na mizimu utakwisha . Ogopa Afrika na mila zake . Mizimu kwa Afrika ni Roho za Mababu na Mababuzi.
 
suguye anawapiga sana masikini kwa gea hizo na kusababisha familia na koo kufarakana
Niliposoma hiko kitabu cha uongo kwa kina nimebaini ni stori za uongo Mtupu
1. Mungu gani huyo anayebebwa na shetani mpaka kilimani?
2.Ni nani aliyekuwa anarekodi wakati huyo Mungu anaumba Dunia?
3.Hivi jua liliumbwa siku ya ngapi na kabla ya kuubwa Jua mwanga gani uliokuwepo?
4.Yesu alivyokwenda Mlimani kusali peke yake muandishi wake alikuwa nani mpaka mazungumzo yake na Mungu yawe kitabuni?
5..Eti ukiwa na Imani unaweza ukaamuru mti ng'oka na utang'oka lakini Yesu huyo huyo akasaidiwa kubeba msalaba tu maana aliushindwa ili akatundikwe.
6.Hivi inakuaje mnatembea kwa mguu km1400 kwa usiku mmoja lakini km 700 tu miaka 40 Hao wanaIsrael na Mussa wao
7.Imani yako inasema Umerithi zambi za Adam na Eva lakini kituko kwani Hamjarithi Utajiri wa Suleiman
8. Eti Nuhu alijenga Safina sababu ya Gharika kuu na akapakiza viumbe jike na dume swali linakuja (i)Taarifa ilifikishwa vipi Afrika,Ulaya,Amerika kusini? na Australia ?(ii)Simba alikula nini kipindi chote cha gharika ndani ya Safina(iii) Watu walikula nini baada ya mafuriko hayo makali maana ardhi ilikuwa tupu mazao yamekaisha na mafuriko? (i)Kangaroo alisafiri vipi mpaka Australia
7.Baada ya kula Tunda huko bustani ya Eden Mwanamke Eva akasema Atazaa kwa Uchungu Swali hawa ng'ombe wetu hapa Tarime mbona wanazaa kwa Uchungu wametenda kosa gani?
8.Kwenye Sodoma na Gomola tunaambiwa Mke wa Ruthu aligeuka Mwamba wa Chumvi swali ni hili nani aliyemuona kwamba amegeuka Mwamba wa Chumvi wakati walipewa taarifa kuwa ni marufuku kugeuka?
9.Hivi ni Mungu gani huyo aliyevumilia miaka 400 ya utumwa tuliofanyiwa na kuuzwa mnadani kama maembe halafu ataniadhibu kwa kutokumuamini?
10.Eti msamehe Mtu 7x70 kwa makosa aliyotenda Lakini huyo Mungu kashindwa Kumsamehe Adam na Eva kwa kula Apple moja?
11.Samson alimuua Simba kwenye jangwa la Palestina aaahaaaa Toka lini simba anaishi kwenye jangwa?.

Hakika ninakuambia kama kungekuwa na Nguvu kwenye jina la Yesu hao Wazungu wangeficha kama inavyofichwa Teknolojia ya Nyuklia.

Heshimu sana Babu wa Mababu zako maana wao ndiyo wenye DNA zako wewe umetoka kwao Dini ni tamaduni ndani ya tamaduni kuna mila ndani ya Mila kuna Imani na Imani ndiyo Wageni wakaita Dini hakika nakuambia Imani ya Kiafrika wala haina Masharti magumu na Inafanya kazi kwa Ubora wa juu sana na Ibada zake ni kwa Mwaka mara moja au mbili lakini Imani zingine lazima ufanye kila muda kila wakati lakini Matokeo 0.

Heshimu Afrika heshima maadili na mila ulizoachiwa..

Unaweza sema Uongo Kanisani Unaweza sema Uongo Msikitini na hakuna kinachoweza tokea usije sema Uongo kwenye Mizumu au kwenye Kilinge cha Mganga utakwenda na Maji .Toa ahaadi ya Pesa ya sadaka kanisani na Msikitini usipotoa hakuna kitakachotokea Usije thubutu Kwa Mganga au kwenye Mizimu hutoamini macho yako. KILINGE HAKITANIWI WALA HATUSEMI UONGO .
 
Hizi ni Fiction stories.

Illusions.

Hakuna Laana, mizimu wala roho.

Uzembe, Ujinga na Ukosefu wa maarifa ndio hukwamisha watu kwenye maisha.
Kuna jambo moja tu kuhusu hivi vitu,ni ngumu kumuelekeza mtu akaelewa,ni hadi yakukute..ni kama hivi tu umelekezwa na haujaelewa

Nikuambie tu kitu kimoja mkuu,kama kila kitu kwenye maisha yako kinaenda sawa,thank GOD.
 
Kuna nyumba ukiingia Mama yupo Baba yupo Ila mtoto/watoto ni wa Dada wa kazi na Kaka wa kazi, Baba na Mama sio wazazi ni Provider tu au tuseme walezi Ila Dada wa kazi na Kaka wa kazi ndio wanakua km wazazi wa watoto

Ibada njema!
 
Back
Top Bottom