Kwanini mtoto awe Mali ya baba?

Kwanini mtoto awe Mali ya baba?

makonko

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2017
Posts
239
Reaction score
271
Nimekaa nikatafakari saana

Hivi kwanini mtoto anakuwa Mali ya baba wakati kwa mawazo yangu Mimi naona mama ndo ana-play part kubwa sana, kwani mama anambeba mtoto tumboni miezi 9, haitoshi siku ya kujifungua leba ni siku ambayo Israeli mtoa roho anakuwa naye karibu sana(kufa/kupona).

Baada ya hapo kabila, ukoo vyote anafata kwa baba.

Why??
 
Kwani nani kasema mtoto ni wa mama? Ukoo ndio wa baba. na pia kuna baadhi ya jamii ukoo upo upande wa mama hasa watu wa mtwara
 
Matrilineality iko practiced maeneo mengi ya East Africa na Africa, hayo uliyoyahoji ni desturi tu ambazo kwa kizazi hiki cha kisasa mama anaweza kubadilisha...mbona single mothers ni wengi...Kwa mfano jamaa akikataa mtoto mwanamke anaweza mpatia utambulisho wake...nk nk
 
Hujafanya utafiti wa kutosha.
Wakikuyu mtoto ni mali ya mama.
Wamakonde pia mtoto ni mali ya mama ndio maana mmakonde humuamini mjomba kuliko baba.
Waembu wa Kenya nao utaoa utalipa mahari utaishia kufaidi puchi/nyapu tu mtoto ni wa mama.
 
ukienda bar kunywa bia kwanini usimeze na chupa,unakunywa bia tu chupa unaiacha?
ukinijibu hilo nitakuja kukwambia majibu ya swali lako...
Chupa c chakula/chakunywa, ukimeza chupa utakufa
 
Matrilineality iko practiced maeneo mengi ya East Africa na Africa, hayo uliyoyahoji ni desturi tu ambazo kwa kizazi hiki cha kisasa mama anaweza kubadilisha...mbona single mothers ni wengi...Kwa mfano jamaa akikataa mtoto mwanamke anaweza mpatia utambulisho wake...nk nk
Hivi ulishawahi kuona au kusikia mfano:- zubeda zainabu, mariam zurufa, Neema Joyce?
 
Mtoto ni za a wote na watu mnafanya kosa kubwa sana kusahau mchango wa baba.

Baba anatoa mbegu, mama anaitunza mpaka itakapokuwa mtoto. Baba ndio kiini cha hicho kinachokuja kutokea baada ya miezi 9.

Mama ni sawa na udongo, baba ni sawa na mbegu ya mahindi inayowekwa kwenye udongo na baadae kuwa muhindi.
 
Matrilineality iko practiced maeneo mengi ya East Africa na Africa, hayo uliyoyahoji ni desturi tu ambazo kwa kizazi hiki cha kisasa mama anaweza kubadilisha...mbona single mothers ni wengi...Kwa mfano jamaa akikataa mtoto mwanamke anaweza mpatia utambulisho wake...nk nk
Kwenye ishu ya single mothers it is possible since baba hataki kudeal na chochote kuhusu mwanae.
Lakin sasa kuna ishu kama ya baba na mama wako pamoja kwenye malezi hapo itakuwa ngumu kidogo.
 
Unajua sema ww ni jeuri.
1.Mungu mwenyewe alitupendelea hilo.
2.Baba anamiliki Mbegu Mama ana yai/shamba hivyu mwwnye mbegu anayepanda ndiye mmiliki wa kinacho zaliwa kinachomea.
3.Mungu ana wanawabariki akina ibrahimu ,yakobo na n.k na watoto waliopo viunoni mwao,narudia na watoto wa viunoni mwao.
4.mwanamke ni sawa na shamba haijalishi ni kame au kinyume chake linashambuliwa na wadudu wakati wa kutoa mazao na n.k
5.Bibilia ikitaja ukoo wa yesu hakuna mwanamke na n.k
 
Hujafanya utafiti wa kutosha.
Wakikuyu mtoto ni mali ya mama.
Wamakonde pia mtoto ni mali ya mama ndio maana mmakonde humuamini mjomba kuliko baba.
Waembu wa Kenya nao utaoa utalipa mahari utaishia kufaidi puchi/nyapu tu mtoto ni wa mama.

Kwenye vitabu shule nilisoma na kuaminishwa hivo.
Ila kwa sasa nipo naishi kwa Wamakonde sijakiona hicho kitu, History sio somo la kuliamini mkuu
 
Nimekaa nikatafakari saana

Hivi kwanini mtoto anakuwa Mali ya baba wakati kwa mawazo yangu Mimi naona mama ndo ana-play part kubwa sana, kwani mama anambeba mtoto tumboni miezi 9, haitoshi siku ya kujifungua leba ni siku ambayo Israeli mtoa roho anakuwa naye karibu sana(kufa/kupona).

Baada ya hapo kabila, ukoo vyote anafata kwa baba.

Why??
Wewe Kabila gani? kwenye kabila langu mtoto hajawahi kuwa mali bali ni binadamu. Unaposema mtoto ni mali una maana hata akiwa mkubwa kwa sababu ni mali ya baba hatamwangalia mama yake bila idhini ya baba? Naona mawazo yako yanakutosha mwenyewe
 
Back
Top Bottom