Kwanini Mpendazoe hakupewa mafao Zitto apewe?

Kwanini Mpendazoe hakupewa mafao Zitto apewe?

kwa sababu hakuwa kibaraka wa ccm, vibaraka ndio wanalipwa zaidi wakimaliza kazi.
 
Ukita kuiba au kuuza madawa ya kulevya jiunge ccm utapata pesa nyingi sana kuna baadhi ya watu huwa wanasema ukiunga mkono vyama vya upinzani utafunguliwa kesi nyingi za uongo utatumiwa tar na kadhalika je ni kweli?

Hilo sio la kuuliza, yaliyowakuta Marehemu Majige na Chenyenge Mza si mnayajua?
 
Zitto naomba ujibu haya ingawa umeishasepa au unasoma kimyakimya
1. nanin muanzilishi wa ACT?
2. wafuasi wako kaijage na masud wa kasulu, walipewa mtaji wa kuuza dagaa, kuuza viatu na kuandaa vurugu kwa dr slaa dec 2013. je huoni yale yote yaliyokuwa kwenye mkakati wa mapinduzi ndani ya chadems uliyahasisi wewe kama ulivyoitwa MM?
3. nani mfadhili mkuu wa ACT- TZ?
 
Last edited by a moderator:
Badala ya kujadili mambo ya maana mnajadili watu makuward bwana ni shida kweli! kama inakuuma siuandamane kuelekea bungeni? kwahiyo wewe unafurahia zzk akipata njaa? itakufaidia nini katika ulimwengu huu.
 
zitto naomba ujibu haya ingawa umeishasepa au unasoma kimyakimya
1. nanin muanzilishi wa ACT?
2. wafuasi wako kaijage na masud wa kasulu, walipewa mtaji wa kuuza dagaa, kuuza viatu na kuandaa vurugu kwa dr slaa dec 2013. je huoni yale yote yaliyokuwa kwenye mkakati wa mapinduzi ndani ya chsms ulihadisi wewe?
3. nani mfadhili mkuu wa ACT- TZ?
Kha! Yukowapi huyo unaemuuliza? Yaani mijitu kama imepagawa vile!!
 
Zitto

Mkuu ulikuwa unawatetea watanzania lakini sasa unajitetea na kuwashawishi watanzania kuwa favour inayoipata kutoka CCM ni kwa utendaji wako mzuri Bungeni
 
Last edited by a moderator:
Kwanini anajitambulisha mjamaa, wakati haishi kijamaa?

Gari anayotumia ni ukwasi mkubwa.

Nyumba yako je?

Ujamaa unamaanisha nini? Kujiita tu mjamaa tu basi umekuwa mjamaa?

Walisema utawatambua kwa matendo... au matunda yao....

Tunayo mifano ya wajamaa tupieni wengine...
 
Zitto

nimetokea kuwa na maswali mengi sana kwako

  1. chadema walikufukazi vipi na chama chako kimemfukuza vipi Limbu]
  2. ilikuwaje mkakurupupuka kuanzisha chama to the extent ya kuwa na chama chenye jina sawa na association nyingine(na hiyo aasociation ishawandikia barua ya kuwaomba mbadilishe jina.....Agrigulture Council of Tanzania ) lakini kwa sababu ni ile favour ya kutumikia chama tawala mataendelea kubebwa
  3. Mbona chama chenu kimekuwa ni chama cha kutaka huruma kwa watanzania na sio kwenda kuuza sera zake kwa watanzania
  4. Mbona mnatumia nguvu nyingi kutangaza cham chenye umri wa mwaka mmoja
  5. Mbona unatangaza sera za ujamaa wakati wewe tayari ni tajiri au unataka watu waanzae kuwekea transaction zake na majina ya Account zako----remember one thing Zitto unatka kuwadanganya watnzania lakini huko benk wapo vijana wanaoipenda Tanzania zaidi yako na wenye uti kwa taifa lako zaidi yako kuwa makini unapowadangya watanzania
 
Last edited by a moderator:
Zitto

Heshima kwako mkuu Zitto. Kuna taarifa kwamba pamoja na kususia posho pamoja msamaha WA kodi lakini kuna udhibitisho kwamba umevuna fedha nyingi zaidi ya hizo posho kutoka NSSF,IPTL,BUZWAGI na baadhi ya mashirika mengine ya umma jambo ambalo umeshindwa kukanusha mpaka Leo.
 
Last edited by a moderator:
Haaah,haah watu wanamshambulia balaa,munkari punguzeni twende taratibu ndugu yetu asikimbie jumla
 
Badala ya kujadili mambo ya maana mnajadili watu makuward bwana ni shida kweli! kama inakuuma siuandamane kuelekea bungeni? kwahiyo wewe unafurahia zzk akipata njaa? itakufaidia nini katika ulimwengu huu.
ingekuwa pensheni inatoka mfukoni kwako sawa.
 
Mh:kuuliza sio ujinga mm nina maswali naomba unijibu.
je ni kweli unaurafiki wa karibu na rostamu azizi?
Kuna tetes kuwa una acc yenye zaidi ya sh bilion mbili ujerumani je ni kweli?
rudisha kumbukumbu nyuma kipindi cha Mwana.halisi iliandikwa mawasiliano yenye mashaka kati yake na Rostom.alipohojiwa na Dr.Slaa akaleta jeuri kuwa wasimchagulie marafiki
 
Naomba niweke sawa kidogo tu kuondoa upotoshaji wa makusudi. Kwanza mimi nasikia tu kwenye vyombo vya habari kuhusu suala la mafao. Halinisumbui. Nawakumbusha;

  1. Toka mwaka 2011 mwezi Juni niliacha kupokea posho za vikao. Kwa mwaka posho za vikao ni takribani shs 24 milioni.
  2. Wabunge hupewa msamaha wa kodi kwenye magari wanayonunua. Kwa kuwa napinga misamaha ya kodi nilikataa na mpaka namaliza ubunge sijatumia msamaha huo wa kodi.

Kwa hiyo suala la fedha sio suala la msingi kabisa kwangu kwenye maamuzi yangu.

Fact: Mpendazoe alilipwa kiinua mgongo chake kwa muda wa miezi aliyotumikia Bunge. Sio kweli kwamba hakupewa kiinua mgongo chake. Alipewa na tunaweza kuthibitisha

Kaka yangu Zitto Pole sanaa, Ungemsikilima Prof. Baregu na Marehemu Mama yako- yasingekutokea hayo yaliyokutokea , CCM siyo watu wazuri wanakutumia then wanakudump , pole sana jenga Chama chako sasa ,Ongea na LIMBU vizuri usiwe na haraka ya vyeo huko ACT. anza polepole watu wakikubali utakuwa tu mwenyekiti wa ACT. AchaTamaa ya Uongozi.
 
Naomba niweke sawa kidogo tu kuondoa upotoshaji wa makusudi. Kwanza mimi nasikia tu kwenye vyombo vya habari kuhusu suala la mafao. Halinisumbui. Nawakumbusha;

  1. Toka mwaka 2011 mwezi Juni niliacha kupokea posho za vikao. Kwa mwaka posho za vikao ni takribani shs 24 milioni.
  2. Wabunge hupewa msamaha wa kodi kwenye magari wanayonunua. Kwa kuwa napinga misamaha ya kodi nilikataa na mpaka namaliza ubunge sijatumia msamaha huo wa kodi.

Kwa hiyo suala la fedha sio suala la msingi kabisa kwangu kwenye maamuzi yangu.

Fact: Mpendazoe alilipwa kiinua mgongo chake kwa muda wa miezi aliyotumikia Bunge. Sio kweli kwamba hakupewa kiinua mgongo chake. Alipewa na tunaweza kuthibitisha
Mzalendo Mjamaa Zito Kabwe ivi Chadema umefukuzwa au umeng'atuka?toa ufafanuzi kuepusha usumbufu
 
Back
Top Bottom