Kwanini Mohamed Dewji "Mo" hatumii bidhaa zake?

Kwanini Mohamed Dewji "Mo" hatumii bidhaa zake?

aka2030

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
2,672
Reaction score
3,737
6C5EC9C7-C8B5-4313-8E87-4564D2551CAB.jpeg


Ukitazama hiyo picha vema Mo anatuma TV ya Sony na sio zile zake za Mo Electro. Je, kwanini hatumii brand yake?
 
Kwani jibu ulijui mkuu hata bei umeshindwa kujua kuwa ni tofauti kati ya Sony na MO!
 
View attachment 1487923Ukitazama hiyo picha vema mo anatuma tv ya sony na sio zile zake za mo electro je kwann hatumii brand yake?
Bora tv atasema zake bado hajaziwekea vitu vingi kama za nje but wewe unafikiri hata hizo sayona sijui cola nini kuna hata mwanafamilia wake mmoja anaezitumia sembuse yeye?

Yupo apige hela siyo vinginevyo!
 
Kuna rafiki yangu alikuwa Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom lakini line ya simu anayotumia ni Tigo. Kuna siku Mzee Baharesa nilimuona anakunywa maji ya Kilimanjaro wakati yeye ana maji yake ya Uhai. Mo Dewji ukimkuta pale New Africa hotel ambapo ni kama sebuleni kwake sijawahi kumuona akiagiza maji ya Masafi ambayo ni yake, yeye anaagiza Kilimanjaro maji. Mzee marehemu Mengi peke yake alikuwa proud na bidhaa zake, maji kwake yalikuwa Kilimanjaro tu. Haya kwenye mgahawa wa IPP pale The Guardian hiluwezi kukuta soda nyingine zaidi ya kampuni ya Coca-Cola na maji ya Kilimajaro.
 
Back
Top Bottom