Kizazi bora kinajengwa na wazazi bora. Fikra,mawazo na akili zetu jinsi tunavyotaka ndio zinavyotupeleka. Sote ni dhaifu, lakini hakuna wakati mzuri kuonesha udhaifu wako mbele za watu. Ni kweli mkamilifu hayupo, kila mwanadamu hutenda dhambi, wakati wote mtu haipendezi kuzitangaza dhambi zake.
Mwenye kusimamia uovo, uchafu na dhambi yoyote akiwa na akili zake timamu huyu yumo hasarani, IMANI yangu, Islam inakataza ZINAA,sijui imani yako wewe!? Bado ninashaka kubwa,kwani naamini hakuna imani yoyote inayoruhusu " TEST BEFORE USE" .
Watu wanasema dunia itakapokaribia ukingoni, watu watatokwa na hofu moyoni mwao, kwa juhudi zao zote watasimamia maovu na kuyatetea kwa nguzu zao zote. Kila anae kubali kuonja kabla,hakosi sababu ingawa ni sababu za kifedhuli zilizokosa fikra na akili ya kawaida tu ya mwanadamu. Si kila kitu lazima uende darasani. Unapokosa ustahamilivu daima utaidhulumu nafsi yako, bikra yako ni zawadi kubwa kwa mume au mke wako huo ndo ustahamilivu wa maisha. Tusijifanye kama hutufaham,tusijifanye kama hatuoni, hizo ni dhambi kubwa ambazo zitatesa mno. Mwenye kuisaliti nafsi yake, hatoshindwa kumsaliti mwenzake. When you make your first love illegal, ni sawa na kuisaliti nafsi yako, hii dhimbi wengi zinawatesa,you are witness...
MWENYE KUTENDA, ATATENDEWA PIA. NA MWENYE KUISALITI NAFSI YAKE,HATOSHINDWA KUKUSALITI. STOP KIDDING YOURSELF GUYS...ALLAH KNOWS BEST.