Kuna hawa wanaojiita TCRA sijui hata regulate kitu gani! Mitandao ya simu wametuwekea miundombinu mibovu ndiyo maana network zinakata kila wakati, TCRA haijawahi hata kutoa tamko wamekalia tu kujaza matumbo yao kwa kulipana mishahara mikubwa na maposho utadadhani nchi ni ya kwao peke yao. Nachukia sana unampigia mtu simu badala ya simu kuiita au kukupa msg kama haipatikani, wanakuwekea tangazo lao kwanza kwa dakika nzima ndiyo baadaye unajibiwa simu unayopiga haipatikani, pia kutuma ujumbe wa tangazo kwenye simu ya mtu bila ridhaa yake ni dharau kubwa sana ambapo TRCA walitakiwa wayaone haya na mengine mengi tuu na wachukue hatua. Nchi imegeuzwa shamba la bibi, hakuna kiongozi anayetimiza wajibu sasa kuanzia mkuu wa kaya mpaka mwenyekiti wa mtaa.
Mungu tusaidie 2015 tuikomboe nchi yetu kwenye mikono ya wanyang'au.