Kwanini mimi nimekuwa sina furaha kama wanafunzi wengine?

Passed

JF-Expert Member
Dec 15, 2017
561
156
Mbona wengine wanasoma kwa furaha zote kwanini hii hali inikute mimi tu nina nini? Nilianza masomo ya kidato cha tano na cha sita kwa usajili wa private candidate nikaacha nikaona nisije nikashindwa kufaulu kutokana na muda kuwa mchache nikaamua kwenda chuo.

Mwanzo nilianza kwa furaha zote badae ghafla tu hali ikabadilika na kuanza kuumia moyo 24 hrs na kutaka kugairi kusoma nilijilazimisha hadi nikamaliza mwaka performance ikawa nzuri sana.

Naombeni mnipe nguvu nifanye nini ili hii hali iondoke mana ilianza mwaka jana na kila siku inanisumbua roho inauma kama inataka kunyanyuka haitulii kabisa na kutwa inawaza shule tu. Mimi hii hali siitaki nahitaji niwe na furaha kama wanafunzi wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imesababisha hadi naumwa mgongo kifua kuwaka moto mishipa ya shingo kuuma na kichwani kama wamenitwisha mzigo nina mateso sana na chuo staki kuacha ila msongo wa mawazo unaendelea tu day by day nimechoka sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huenda ukawa huna furaha na unachokisomea na unamshaka na muskabali wa maisha yako kutokana na hicho unachokisomea, hujui ni nini hatma yako.

Na hii husababishwa na sababu tofauti tofauti, ila unaweza kuwa sawa maana hiyo ni mentality tu.
 
Kaonane n therapist huenda una mengi ya kuzungumza ila hujampata mtu sahihi wa kukuelewa,

Fanya sana mazoezi, epuka kukaa peke yako na kuwaza, pata muda wa kupumzika/kulala, jiweke karibu na Mola wako.

Corona Virus: Stay Home the only Medicine found.
 
Imekaa kisaikolojia zaidi kama unapenda kweli hiyo fani au la kiufupi suluhu ninayoona n kumaliza chuo na unaweza kwenda a level tena huku chuo tyr km hyo fan hutak unaweza endelea nayo uajiriwe au ujiajir kimaslah ya fedha lakini na bado muda haujakupita kwa lolote.
 
Pregabalin,
Mkuu kwanza pole na changamoto hizo. Mimi sikufahamu na ushauri wangu cha kwanza Nakushauri Usali/maombi (prayers) coz God yupo na ninaamini hakuna kinachoshindikana kwake.

Pia utafute watu unaowaamini uongee nao uwaelezee jinsi inavyokuwia vigumu kutulia na uchambue ushauri unaopewa cha mwisho nakushauri jiweke busy na vitu mbalimbali kama kufanya mazoezi(physical exercise) na kujichanganya na watu kwa kiasi(tafuta marafiki wa kukujenga kifikra ).

Ni hayo tu mkuu kwa maoni yangu.
 
Upo stressed, may be kuna expectations zimekwama. Kuwa confused/stressed ni jambo la kawaida pale expextations zinapokwama, hasa kwa mtu mwenye malengo makubwa makubwa.

Jambo la muhimu kwako ni kujiweka karibu na Mungu wako, mengine yatafuata. Provided u mzima na Mungu akiwa upande wako, kutoka 0 kwenda 100 siyo ngumu kihivo
 
Kwanza pole sana

Nachotaka kushauri mkuu ni kama ifuatavyo,

Moja ya side effect ya lockdown ndio hii,wapo wengi wanaopatwa na shida kama hizi mkuu ila goja nijikite kwako

_ kwa kipindi hiki nakushauri sana ujiepushe kukaa peke yako, kama ikiwezekana naomba (kama ni mpenzi wa kusikiliza nyimbo) sikiliza ukiwa peke yako chumbani au popote,hii itakufanya u relax na kusahau hili.

_pili fanya mazoezi, kimbia ukiwa unachukua tahadhari za corona, unaweza ukawa una tune hata ka muziki kidogo then automatically you will start forgetting this!

_ ongea na wanafunzi wenzako,mbadilishe mawazo wao wanafanya nini kipindi hiki wawapo nyumbani, kufanya vile utajikuta unaona kitu cha kawaida

Kingine kikubwa mkuu punguza kuwaza kuhusu mtihani, hebu kabla hujawaza vile fikiria ni wangapi wamekumbwa na hili tatizo? Je uko peke yako? Hivyo chukulia ni janga la kidunia kikubwa tuzido kuomba kwani ni wengi wamekutana na shida hizi pengine yako ni ndogo!! Labda ni kupe mkasa mmoja though it's not so good to share it here in!!

Kuna mama mmoja anafanya kazi kiwanda fulani stakitaja,alinipigia simu anauliza kama serikali watafunga yaani tutawekwa lockdown, yule mama anasema ndani hana chakula,kodi ya nyumba imeisha,mtoto wake ambaye ni mwanafunzi anazurura hovyo,mama yake mzazi anaumwa sana,then nikampa pole akaniambia ameamua kufunga na kusali ili Rais asifunge yaani kuwekwa lockdown maana hajui ataishije!!!

I was shocked kusikia vile lakini kiukweli yule mama alikuwa analia nikaelewa kiukwel watu wanapitia magumu, coming to the main point, shukuru sana ndg hata kwa hatua hiyo uliyofikia then sali kwani Mungu atatusikia, ni wengi wenye shida ndg!!

MTANGULIZE MOLA WAKO, EPUKA KUSIKIA HABARI MBAYA HASA ZA CORONA IKIWEZEKANA USIFUATILIE TAARIFA KAMA HIZO KWANI ZITAKUONGEZEA STRESS NDG!! MUNGU YU PAMOJA NASI,ATATUVUSHA!!

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu,cha msingi hapo ni kujiamini wewe binafsi don't compare yourself, focus on the positive.
Maisha ya chuo ukiangalia watu wengine wanaishije hautojipenda kamwe, hatufanani background zetu.
 
Muombe Mungu na pia tafuta hobby kama kucheza draft,kupiga kinanda,karata n.k me pia niliteseka sanakipindi nasoma nilikuwa sijiamini kabisa mpaka namaliza form 6 ila namshukuru Mungu I am a teacher now
 
Back
Top Bottom