Kwanini mimi ni mzito kumsaidia mpenzi wangu?

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,752
4,463
Yaani nashindwa kujielewa nina tatizo gani mimi,je ni ubahili,uchoyo au umimi? Nikiwa na mwanamke huwa sipendi aniombe hela kabisa.

Hata akiwa na shida kubwa kiasi gani ambayo nahisi kabisa naweza kuitatua huwa nakuwa mzito sana kumsaidia vinginevyo hiyo shida isihusishe pesa,ila kama ni masuala ya pesa huwa nina uzito sana wa kutoa,hivi hii inachangiwa na niini wakuu?
 
Sio kosa lako, inawezekana wewe bado ni mvulana. Sasa unataka amueleze nani shida zake zote? Lakini pia inaweza kuwa ni tabia yako tu ya ubahili. Au labda una ukata mfukoni mkuu? Ila kama hali hiyo ya kutokumsaidia mpenzi wako unaichukia, basi ni rahisi kubadilika kwa kujizoesha kutoa.
 
Yeye ni mzazi wake au mme wake?
 
Mimi napenda sana kuwasaidia watu hususani mpenzi wangu na kila nikiwasaidia hupata zaidi na zaidi
 
Back
Top Bottom