Kwanini Mikoa yetu haiendelei kiuchumi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Mikoa yetu haiendelei kiuchumi?

Discussion in 'Great Thinkers' started by Mchambuzi, Feb 24, 2012.

 1. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Kila tunapopata wasaa wa kujadili uchumi na hali za maisha ya watanzania, tumekuwa na jadi ya kuangalia zaidi hali ilivyo kitaifa na kisekta (MACRO LEVEL), bila ya kujadili sana hali na takwimu kimikoa/kiwilaya/kivijiji (MICRO LEVEL). Pamoja na kwamba huwa tunajadili hali za maisha ya watanzania waliopo vijijini, ni mara chache sana kwa sisi kudadisi hali za ndugu zetu hawa kwa undani, na huwa hatuendi mbali zaidi tu ya kutambua kwamba wingi wao ni karibia 70% ya jumla watanzania wote (milioni 42), na pia kutambua kwamba wengi wao (karibia 80%), wanajishughulisha na Kilimo.

  Nia yangu ni kujaribu kuja na mada itakayotusaidia kuziba pengo hili la mjadala. Katika post yangu ya kwanza, sitajadili lolote zaidi ya kuweka tu takwimu muhimu na kumalizia kwa maswali ambayo nina amini yatatusaidia kuupa mjadala uhai.

  Kwanza nadhani ni muhimu tuka tazama takwimu za uzalishaji wa sekta mbalimbali/mchango wa sekta mbalimbali katika Pato la Taifa (GDP), kwa kufananisha mwaka 2000 na mwaka 2010. Takwimu hizi zitakuwa na msaada katika mjadala, hasa kutusaidia kuelewa kwa undani kuhusu sekta gani zinatoa fursa zaidi za ajira, sekta zipi zinapanuka/zinasinyaa pamoja na madhara kwa umaskini kutokana na kupanuka/kusinyaa kwa sekta husika n.k..

  Table 1: Mchango wa Sekta Katika Uzalishaji/Pato La Taifa
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]SEKTA[/TD]
  [TD]MWAKA 2000 (%)[/TD]
  [TD]MWAKA 2010 (%)[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Kilimo, uwindaji na Misitu
  · Mazao
  · Mifugo
  · Misitu na Uwindaji[/TD]
  [TD]29%
  · 21.7%
  · 5.1%
  · 2.7%[/TD]
  [TD]24.1%
  · 17.8%
  · 3.8%
  · 2.4%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Uvuvi[/TD]
  [TD]1.8%[/TD]
  [TD]1.4%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Industry and Construction [/TD]
  [TD]19.9%[/TD]
  [TD]22.4%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]· Madini[/TD]
  [TD]· 1.5%[/TD]
  [TD]· 3.3%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]· Viwanda[/TD]
  [TD]· 8.8%[/TD]
  [TD]· 9.0%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]· Umeme na Gesi[/TD]
  [TD]· 2.1%[/TD]
  [TD]· 1.8%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]· Maji (Water Supply)[/TD]
  [TD]· 0.5%[/TD]
  [TD]· 0.4%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]· Construction (Ujenzi)[/TD]
  [TD]· 5.2%[/TD]
  [TD]· 8.0%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Service Sector/Sekta ya Huduma [/TD]
  [TD]45.3%[/TD]
  [TD]43.9%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]· Trade and Repairs[/TD]
  [TD]· 12.8%[/TD]
  [TD]· 12.1%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]· Hotels and Restaurants[/TD]
  [TD]· 2.8%[/TD]
  [TD]· 2.3%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]· Transport[/TD]
  [TD]· 5.5%[/TD]
  [TD]· 5.1%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]· Communications[/TD]
  [TD]· 1.2%[/TD]
  [TD]· 2.1%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]· Financial Services[/TD]
  [TD]· 1.6%[/TD]
  [TD]· 1.8%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]· Real Estate and Business Services[/TD]
  [TD]· 10.7%[/TD]
  [TD]· 8.8%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]· Public Administration[/TD]
  [TD]· 6.6%[/TD]
  [TD]· 8.0%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]· Education[/TD]
  [TD]· 2.1%[/TD]
  [TD]· 1.4%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]· Health[/TD]
  [TD]· 1.2%[/TD]
  [TD]· 1.6%[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]· Other Social and Personal Services[/TD]
  [TD]· 0.9%[/TD]
  [TD]· 0.6%[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  Takwimu za pili ambazo ni muhimu sana zinahusu pato la kila mtanzania kwa mwaka (GDP Per Capita) kwa kila mkoa wa Tanzania. Tufahamu tu kwamba duniani kote, GDP Per Capita ni kiashiria (indicator) cha hali ya wananchi kiuchumi i.e. kipato/income. Zifuatazo ni takwimu za pato la kila Mtanzania kwa mwaka 2010. Nimechukua kumi bora na kuziweka in ‘order of ranking':


  Table 2: Vipato Vya Watanzania Kulingana na Mikoa Wanayotoka (GDP Per Capita)
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]MKOA[/TD]
  [TD]PATO LA KILA MWANANCHI KWA MWAKA (T.Shillings) (2010)[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]1. Dar-es-salaam[/TD]
  [TD]1,740,947 (million)[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]2. Iringa[/TD]
  [TD]979,882 (laki)[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]3. Arusha [/TD]
  [TD]945,437[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]4. Mbeya[/TD]
  [TD]892,877[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]5. Kilimanjaro[/TD]
  [TD]879,432[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]6. Ruvuma[/TD]
  [TD]866,191[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]7. Mwanza [/TD]
  [TD]829,647[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]8. Tanga [/TD]
  [TD]763,203[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]9. Morogoro[/TD]
  [TD]744,234[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]10. Rukwa[/TD]
  [TD]726,658[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  Je, ni Mikoa ipi yenye vipato duni?


  Table 3: Mikoa Maskini kuliko yote kwa kigezo cha Pato La Kila Mwananchi (GDP Per Capita)
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]MKOA[/TD]
  [TD]PATO LA KILA MWANANCHI KWA MWAKA (T.Shillings) (2010)[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]1. Singida[/TD]
  [TD]483,922 (laki)[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]2. Dodoma[/TD]
  [TD]485,211 (laki)[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]3. Kagera[/TD]
  [TD]491,713 (laki)[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]4. Kigoma[/TD]
  [TD]499,428 (laki)[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]5. Tabora[/TD]
  [TD]528,832 (laki)[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  Je, ni Mikoa ipi inachangia Zaidi Kwenye Pato la Taifa/Inayozalisha Bidhaa na Huduma Nyingi Zaidi Tanzania (GDP)?

  Table 4: Kumi Bora Kwa Uzalishaji Wa Bidhaa na Huduma (GDP).
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]MKOA[/TD]
  [TD]UZALISHAJI WA BIDHAA NA HUDUMA (GDP) T.shillings (2010)[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]1. Dar-es-salaam[/TD]
  [TD]T.sh 5.4 trillioni[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]2. Mwanza[/TD]
  [TD]T.sh 3.0 trillioni[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]3. Mbeya[/TD]
  [TD]T.sh 2.3 trillioni[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]4. Shinyanga[/TD]
  [TD]T.sh 1.9 trillioni[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]5. Iringa[/TD]
  [TD]T.sh 1.7 trillioni[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]6. Morogoro[/TD]
  [TD]T.sh 1.6 trillioni[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]7. Arusha[/TD]
  [TD]T.sh 1.5 trillioni[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]8. Kilimanjaro[/TD]
  [TD]T.sh 1.3 trillioni[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]9. Kagera[/TD]
  [TD]T.sh 1.3 trillioni[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]10. Ruvuma[/TD]
  [TD]T.sh 1.2 trillioni[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]11. Tabora[/TD]
  [TD]T.sh 1.2 trillioni[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]12. Rukwa [/TD]
  [TD]T.sh 1.1 trillioni[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  *Ukitazama orodha hii, ipo mikoa 12 na sio 10. Hii ni kwa sababu kuna mikoa miwili inalingana (Ruvuma na Tabora), na pia nimeongezea Mkoa wa Rukwa kwa makusudi kwa sababu upo katika kundi linaloitwa "The Big Four".


  Je, ni Mikoa ipi yenye michango midogo zaidi kwenye pato la taifa/uzalishaji mdogo zaidi wa bidhaa na huduma Tanzania?

  Table 5: Mikoa Yenye Michango Midogo Katika Uzalishaji/Pato la Taifa (bottom 5).
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]MKOA[/TD]
  [TD]UZALISHAJI WA BIDHAA NA HUDUMA (GDP) T.shillings (2010)[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]1. Singida[/TD]
  [TD]T.sh Billioni 661[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]2. Pwani[/TD]
  [TD]T.sh Billioni 608[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]3. Lindi[/TD]
  [TD]T.sh Billioni 621[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]4. Kigoma[/TD]
  [TD]T.sh Billioni 906[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]5. Mtwara[/TD]
  [TD]T.sh Billioni 927[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  Je, Mikoa Ipi Hupewa Kipaumbele Katika Bajeti? Kwa mfano, kwa mwaka 2010, jumla ya bajeti iliyotengwa kwa ajili ya mikoa yote Tanzania ilikuwa T.sh trilioni 1.7. Ifuatayo ni orodha ya mikoa iliyopewa kipaumbele zaidi.

  Table 6: Orodha ya kumi bora – vipaumbele katika Bajeti Ya Serikali.
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]MKOA[/TD]
  [TD]BAJETI YA MWAKA (T.sh)[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]1. Dar-es-salaam[/TD]
  [TD]T.sh Billioni 154[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]2. Mwanza[/TD]
  [TD]T.sh Billioni 135[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]3. Mbeya[/TD]
  [TD]T.sh Billioni 109[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]4. Shinyanga[/TD]
  [TD]T.sh Billioni 104[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]5. Kilimanjaro[/TD]
  [TD]T.sh Billioni 100[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]6. Tanga[/TD]
  [TD]T.sh Billioni 92[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]7. Kagera[/TD]
  [TD]T.sh Billioni 88[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]8. Morogoro[/TD]
  [TD]T.sh Billioni 86[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]9. Iringa[/TD]
  [TD]T.sh Billioni 85[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]10. Arusha[/TD]
  [TD]T.sh Billioni 81[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  Je, ni mikoa ipi inayotengewa fedha ndogo zaidi katika Bajeti ya Serikali?

  Table 7: Mikoa Isiyopewa Kipaumbele Katika Bajeti Ya Serikali (Bottom five).
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]MKOA[/TD]
  [TD]BAJETI YA MWAKA (T.sh)[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]1. Mtwara [/TD]
  [TD]T.sh Billioni 57[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]2. Kigoma[/TD]
  [TD]T.sh Billioni 56[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]3. Singida[/TD]
  [TD]T.sh Billioni 50[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]4. Manyara[/TD]
  [TD]T.sh Billioni 54[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]5. Rukwa[/TD]
  [TD]T.sh Billioni 49[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  Yafuatayo ni baadhi ya maswali ambayo nadhani yanaweza kuipa mada hii uhai zaidi:

  1. Je, wabunge wanapojadili bajeti na kujenga hoja mbali mbali kuhusu udogo au ukubwa wa bajeti husika, huwa wanazingatia nini zaidi? Umuhimu wa Sekta? Umuhimu wa Mikoa kiuchumi? Hali za wananchi kijamii na kiuchumi katika mikoa husika? Vigezo vya kisiasa?

  2. Je, takwimu hizi zina ashiria nini juu ya malengo ya serikali kwenye sekta za kilimo na viwanda?

  3. Je, Serikali inatumia vigezo gani kutenga viwango tofauti vya bajeti kwa mikoa:
  · Mchango wa mkoa/mikoa husika katika pato la taifa/uzalishaji wa bidhaa na huduma?
  · Hali ya za kiuchumi na kijamii za wananchi katika mikoa husika?
  · Vigezo vya kisiasa?

  4. Je, ile mikoa inayoitwa "The Big Four" – Iringa, Mbeya, Rukwa, na Ruvuma, hadhi hii inatokana na kigezo/vigezo gani?
  · Mchango wa mikoa hii minne katika uzalishaji wa mazao ya chakula (food crops)?
  · Mchango wao katika uzalishaji wa Kilimo kwa ujumla (food and cash crops)?
  · Mchango wao wa jumla katika Pato la Taifa (GDP)?

  5. Na mwisho, Je, nini iwe kipaumbele cha taifa (budget priority) kwa mwaka huu wa fedha na hata siku za usoni?
   
 2. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]Katika takwimu hizi, tunaona kuwa kwa upande mmoja, Tabora ni moja kati ya mikoa iliyo masikini kwa mfumo wa GDP (laki 528,832), lakini ni Tabora hiyo hiyo ambayo inachangia zaidi Kwenye Pato la Taifa/Inayozalisha Bidhaa na Huduma Nyingi Zaidi Tanzania (1.9 Trillion).

  Kwa nini inakuwa hivi? Inakuwaje mkoa unachangia zaidi pato la taifa lakini bado ukawa katika wanaoongoza kwa umasikini. Baadaye watu wa Tabora wakizua fujo za kutaka kujitenga waonekane wabaya.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,200
  Trophy Points: 280
  Ukweli ni kwamba hata hizo figures za kitaifa ni suspect, na pia unapofinyanga figures za kitaifa out of thin air ni rahisi zaidi kufanya obfuscation kwa kucheza na numbers, lakini kadiri unavyoshuka chini katika hiyo hierarchy, ndivyo ufinyanzi huu wa figures ambazo si za kweli unakuwa mgumu. Ni rahisi kusema uchumi wa nchi unakua kwa asilimia 7 hata kama umedumaa na haukui. Ni vigumu kusema uchumi wa kaya moja unakua kwa asilimia 7 kama haukui.

  Huwezi kuwa na uchumi wa nchi unaokua, halafu hapo hapo uchumi wa mikoa usikue. Hili linaonyesha hizi figures nzuri za kitaifa si za kweli.

  Pia nchi yenye corruption kama yetu huwezi kutegemea consistent figures kwani ulaji mwingi.

  I should know about this, nawaona watumishi wa serikali tangu enzi za Malima Mipango wanavyohangaika kufanya overtime wakati wa bajeti ili tu kufinyanga mnamba zioane na uongo wao usiosimama katika uchumi halisi.
   
 4. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Ni sahihi kabisa, hasa ukizingatia pia kwamba Tabora ndio wazalishaji wakubwa wa Tobacco ambayo inalipatia taifa fedha nyingi sana za kigeni. Vilevile Tabora ndio wanakiweka kiwanda cha TCC mjini.

  Majority ya bajeti za mikoani zinatumika kwa ajili ya administration katika wilaya za mkoa husika na pia procurement; Unaonaje wazo la kuruhusu mikoa ipate asilimia fulani ya mapato yanayotokana na mazao/rasilimali zake badala ya kugaiwa inequitably kama njugu na serikali kuu kutoka kwenye chungu kimoja?

  Kwa njia hii, hata ile mikoa ambayo haijajaliwa kuwa na mazao na rasilimali za kutosha itaweza kuwa identified easily na kutengenezewa utaratibu wa kuchangiwa na mikoa mingine yenye surplus au kitu kama hicho.

  Ni wazo tu sijali structure vizuri lakini natumaini limeeleweka.
   
 5. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Hizi ndio takwimu za National Bureau of Statistics, Serikali kupitia wizara zake mbalimbali, na pia World Bank. Sasa tunafanyaje katika hali hii ya kufinyanga finyanga?
   
 6. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Kwa twakimu hizo juu, kwa wastani mkazi mmoja wa Dar Es Salaam anapata shilling 150,000 Kwa mwezi. Ukichukua inflation na matumizi, hakuna sababu watu wasiwe wezi.
   
 7. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Halafu WorldBank nao wanatujia na ripoti yao ya mwaka 2012 titled - Tanzania Economic Update: Stairways to Heaven (2012). Yani kweli pamoja na taabu yote wanayopata watanzania nyakati hizi, taasisi kubwa kama WorldBank yenye heshima na wasomi/wataalam wa kupindukia inakuja na utafiti wenye 'title' iliyojaa mzaa mzaa na kutuhadaa utafikiri na wao ni REDET?

  Ndio maana huwa nasema kila wakati kwamba WorldBank na IMF wapo kwa ajili ya kutuangamiza tu, hawatusaidii lolote katika kupunguza umaskini, kwao Umaskini umekuwa ni Biashara inayofaidisha wadhamini wao - Multinationals (kupitia FDI), wanaokuja kwa dhamira kuu ya kutudhulumu na rasilimali zetu, huku wakitumia nguvu yao ya fedha kutenganisha viongozi wetu na wananchi.
   
 8. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Nchi hii tusipoangalia, haitachukua muda kabla hatujaingia kwenye vurugu kama za Nigeria kule Delta ambapo maskini walichoka kushuhudia wageni wanakuja na kuchota rasilimali zao huku wakiwaacha wao kapa. Ndani ya miaka kumi Tanzania itakuwa na mafuta, gesi, migodi ya uranium, migodi mingi zaidi ya dhahabu, shaba, makaa ya mawe n.k.

  Lakini je itakuwa kwa faida ya nani? Kwa faida ya mikoa/kanda husika au kwa faida ya wageni huku chenji kidogo ikienda kuweka mambo sawa kwenye majiji machache tu, hasa Dar-es-saalam?

  Tangia uhuru imekuwa jadi kwa serikali kujikita zaidi kuboresha huduma za barabara, afya, elimu n.k kwenye miji mikuu tu kama moja ya njia ya kufanya wananchi hasa 'urban elites' wasi rise up.

  But this Time, Only Time will tell.
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Feb 26, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,154
  Trophy Points: 280
  Mchambuzi,

  ..labda ungetuletea mgawanyo wa fedha za miradi ya maendeleo.

  ..pia ungetuletea mchanganuo wa idadi ya miradi baina ya mikoa mbalimbali.

  ..zaidi, unaweza ukawa hujatenda haki kwa kuangalia data za mwaka mmoja tu.

  NB:

  ..can you explain to me kwanini sekta ya MADINI inachangia only 3.3% ya pato la taifa?
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,200
  Trophy Points: 280
  Hiyo "Stairway To Heaven" ni bonge la kijembe kutoka kwa hawa "preachers of hope" wenye "economic hitmen" agenda.

  Yaani wanatuambia kabisa tunaitafuta mbingu kwa ngazi!!
   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Uzuri ni kwamba hali bado si mbaya sana. Lakini swali lako ni la msingi sana. Ukumbuke kuwa tulichukua nchi aliyojenga mkoloni, na toka alipoondoka ni Nyerere tu alijaribu kujenga miji mingine, lakini hakufanikiwa sana. Tanzania hatuna sera yoyote ya msingi, kuhusu kuendeleza mikoa, hata Dar es salaam ya mwaka 1961 na ya sasa zina tofauti sana. Nayo pia haeidelei (quality) ya sasa imerudi nyuma katika mambo mengi sana, kama vile miundo mbinu, usafi, usalama na mpangilio wa mji, nyumba zimeongezeka angalia quality yake, mbaya sana. Watu wanaotakiwa kufanya kazi hiyo hawapo, hakuna mtu yoyote katika ngazi ya taifa au mkoa, anaefikiri kuboresha na kuendeleza mikoa.

  Kibaya zaidi ni kuwa utasikia mkuu wa mkoa wa Morogoro ni mmakonde, ambaye hana interest hata kidogo ya maendeleo ya Morogoro, zaidi ya nafasi yake kisiasa,au mkuu wa mkoa wa wilaya ya karatu ni mbena. Hakuna system inayofanya watu waone kuendeleza mkoa ni kwa manufaa yao, bali wanaona ukuu wa mkoa, RDD, DDD etc ni kazi za kuingiza fedha tu, hazina maana sana ya matokeo ya kazi. Ufanye kazi au uzuge kazi yako iko palepale.

  Tatizo lililopo ni kwamba kwa sasa tunafuata mfumo ambao fedha zote zinapelekwa hazina kuu, na hazina kuu ndio inagawa fedha hizo kwa mikoa, na mgao huwa hauangalii ni nani ametoa mchango zaidi katika pato la taifa. Na bahati mbaya zaidi inapogawa huwa zinaenda mdomoni kwa wachache walioko Dar es salaam. Ndio maana unaona pamoja na kuwa Dar es salaam ina mzunguko mkubwa wa fedha, it is more of a big village than a small city.

  Nadhani kama serikali ingekuwa na utaratibu wa ku-allocate fedha vizuri kwa wale wanaochangia zaidi kwenye pato la taifa, wangekuwa mbele kuliko sasa kwa system ya kuwavuta ambao hata hawavutiki. Kila mwaka wanapewa pesa lakini hawaendelei.
   
 12. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,557
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Hizi statistics za kitaifa na kimataifa zinaendeleza kilekile kinachoitwa economic propaganda.Wanatusifu kuwa uchumi wetu unakua ili tucheke na kufurahi na tuendelee kuwakaribisha wamiliki rasilimali zetu.Na hawa wa ndani wao wanakula na jumuia za kibepari kwa kutudanganya kuwa tunapiga hatua.Haiwezekani nchi inayopiga hatua pato la mwananchi kwenye mji wake muhimu na wa kibiashara kuwa 4750Tsh kwa siku!Kipaumbele chetu tunaambiwa ni kilimo lakini angalia bajeti ya kilimo inavyokuwa haikidhi!Nayo pia haifanyi hata kile kidogo ilichopaswa ifanye kusaidia kilimo in it real sense.Fedha nyingi zinaishia kwenye maonyesho ya kilimo na kwa wajanja wachache.
   
 13. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Ninakubaliana na wewe Mkuu kuhusu wazo la kuipatia mikoa madaraka zaidi juu ya ukusanyaji, utumiaji na ugawa(na)ji mapato. Ile nyimbo ya siku nyingi ya "Madaraka Mikoani" ni uzuri wa mkakasi tu.
  Mapendekezo yangu katika kuboresha utendaji na uzibaji wa mmianya ya wizi na rushwa ni kama ifuatavyo:
  -Tupenguze wanasiasa katika sehemu za utendaji.
  Leo hii wakuu wa mikoa na wilaya na makatibu wao mara nyingi ni majenerali wanajeshi wastaafu au watu ambao hawana ujuzi katika fani yoyote ya utendaji za vitambi vyao. Nafasi za utendaji badala ya kupewa wanasiasa zingekuwa za kuomba kwa ajili ya sifa za kielimu/uzoefu.

  Pia katika uvunaji/ukusanyaji/usimamizi na matumizi ya mali na rasilimali za mkoa, kila mkoa kwa mujibu wa nafasi yake katika uchangiaji wa pato la taifa, ingetakiwa kutoa asilimia inayostahiki kwa serikali kuu badala ya serikali kuu kukusanya kwanza halafu kuwagawia "kitu kidogo".

  - Pesa na rasilimali nyingi za nchi hupotea katika mfumo wetu mbovu wa ukusanyaji na ulipaji. Utashangaa mtu anaenda kulipa kwenye kidirisha cha shirika au ofisi. Au mtu anapita kwenye sehemu za ukusanyi mapato/malipo na kikoba chake na vijirisiti vya karatasi ya mchele anakusanya malipo, baaada ya masiku, wiki au miezi ndio anapeleka pesa sehemu husika na pengine huko baada ya kuchakachua ndio wanapeleka benki kwa wakati wao. Wizi mtupu. Kwa kuwa wizara, mashirika na taasisi hizi zinazo akaunti zao benki, kwa nini mtu asipewe risiti ya deni lake na kuenda kulipa benki moja kwa moja? Kwa uzembe huu ndio tunakuwa na msululu wa wafanyakazi na malipo hewa.
   
 14. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Mchambuzi,

  Model ya maendeleo katika mikoa hipo hapo hapo Tanzania. Chukua mfano mkoa wa Kilimanjaro na hususa ndugu zetu waChagga.

  Maendeleo yamekuja kwanza kwa kuwa na renewable economic engine, kilimo cha kahawa. Kilimo hiki ndicho kilichowapa financial resources wenzetu na kuweza kufanya mambo mengi bila kutegemea sana juhudi za serikali. Kwa sasa hivi wameshafanya diversification na wengi wao hawategemei sana kahawa.

  Kwa maoni yangu, mikoa ambayo hipo nyuma kiuchumi, inabidi zitafutwe economic engines ambazo zitaweka kipato mikononi mwa wananchi. Wenzetu Wachagga hawakuanza kupeleka watoto shule. Walianza kulima kahawa. Walianza kuzalisha kabla ya kuanza kutumia kwenye huduma za jamii.

  Mipango ya sasa ya maendeleo ambayo imelenga kuitajirisha serikali kuu na baadaye serikali kuwalipa wananchi kwa kujenga mashule duni haujasaidia toka enzi za Nyerere. Na wakati umefika kwa wachumi wa Tanzania na serikali kuangalia ni jinsi gani sehemu mbalimbali za nchi zinaweza kuwa na mifumo ya uchumi yenye kuleta maendeleo na kutegemeana.

  Swali linalokuja ni jinsi gani serikali itaanzisha economic engines kwenye maeneo yenye rasilimali zenye kumilikiwa na investors kama vile dhahabu, au gesi, au mafuta? Ni rahisi sana kwa serikali kutumia mapato kwenye ujenzi wa shule au hospitali. Je kuna models zozote zinazoweza kutumika?
   
 15. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #15
  Feb 28, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280

  Mkuu, kuna tofauti kati ya GDP per capita and GDP as a whole. Usishangae kuona kwamba wakati Tabora ina mchango mkubwa katika pato la taifa(GDP) lakini ni moja ya mikoa maskini kabisa nchin kwa kungalia GDP per capita (pato la mkila mwananchi). Among other things, always, GDP per capita huwa inakuwa affected na population. Kama ujuavyo, Usukumani (including Tabora) ni highly populated regions in the country.....this's in contrast to areas like Lindi ambako ingawaje mchango wake kwenye pato la taifa ni mdogo, lakini haipo kwenye mikoa maskini zaidi nchinki ( basing on GDP per capita) simply because population ya Lindi ni ndogo sana....i think ndo least populated region in the country! Hivyo basi, ili Tabora itoke kwenye kundi la wenye per capita ndogo zaidi nchini basi inatakiwa kuzalisha zaidi maintaining its population constant!! na kwavile practically u can't keep population constant, then increase in production rate ( as per GDP) inabidi iwe higher than increase reproduction rate/population increase.
   
 16. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #16
  Mar 13, 2012
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Ndugu Mchambuzi itapendeza ikiwa utatuletea takwimu za miaka ya nyuma za hali ya mikoa yetu ili tuweze kuliongelea suala hili kwa uzuri zaidi kama vile ulivyotuwekea takwimu za pato la taifa na mchango wa sekta mbalimbali.

  Ukija kwenye suala la maendeleo ya mikoa kwa ujumla, hapa kuna vitu mbalimbali ambavyo ni vyema tukavifikiria. Mosi, upatikanaji wa rasilimali aidha asilia, nguvu kazi au mitaji katika mikoa hii. Kutokana na kwamba mfumo wa uchumi wa nchi bado upo katika misingi ya awali ya uzalishaji, rasilimali kubwa ni ile asilia kwa maana ya ardhi, mito, maziwa n.k. Ukiondoa Dar es Salaam ambako ndio kitovu cha kuunganisha shughuli zote za nchi, utaona ya kwamba takribani mikoa 6 inayofuatia katika orodha ya uzalishaji wa pato la taifa inategemea sana matumizi ya ardhi kama rasilimali katika mchepuo wa shughuli za kilimo, madini na uvuvi. Tatizo kubwa la rasilimali asilia ni kwamba hata siku moja haziwezi kuwepo katika kila pembe ya nchi au mkoa husika, kwa maana ya kwamba si kila wilaya, kata au kijiji cha Mwanza, Shinyanga, Arusha n.k itakuwa na rasilimali hizi.
  Katika ugawanyo wa mifumo ya uzalishaji, uwekaji huu wa mayai katika kapu moja (kwa maana ya kutegemea rasilimali ardhi pekee) ni hatari kwa sababu inanyima fursa ya kuendeleza na kutapanya uzalishaji pasi na ardhi. Katika hili ni vyema pia ukaangalia idadi ya vijana waliomaliza angalau darasa la saba katika mikoa hii au idadi ya biashara, viwanda, SACCOS, VICOBA au vikundi vya ushirika vya awali vilivyosajiliwa.

  Pili, kutokana na mfumo wa utawala uliopo kutoa kipaumbele kikubwa kwa sera za maendeleo kupangwa kuanzia juu kwenda chini badala ya falsafa inayoimbwa kila siku ya kuhusisha wananchi toka ngazi ya chini, kumekuwa na changamoto za utekelezaji wa sera mbalimbali pamoja na ukinzani baina ya serikali kuu na zile za mitaa. Hali hii imechangia kukwamisha matunda taraji ya sera nzima ya marekebisho ya tawala za mikoa na serikali za mitaa pamoja na sera nzima ya utekelezaji wake kupitia mfumo wa fursa na vikwazo katika upangaji. Leo hii ni jambo ya kawaida kukuta kata kinataka barabara inayopitika ili waweze kurahisisha usafirishaji wa mazao lakini wakapewa majengo ya shule ya msingi kwa sababu elimu ndiyo kipaumbele cha taifa.

  Tatu, uwezo wa kuendeleza vijiji, kata na mikoa husika unategemea sehemu ya niliyoanisha hapo juu na pia uwezeshaji wa kifedha wa jitihada za wananchi. Mabadiliko katika mfumo wa tozo za serikali za mitaa mwaka 2004 uliziondolea nguvu ya kifedha pamoja na uwezo wa utendaji (msome Boex, 2009, http://www.dpwg-lgd.org/cms/upload/pdf/fiscal/Intergovernmental_Finance_Reform_as_an_InternationalDevelopmentStrategy.pdf, URT (2007), http://www.logintanzania.net/docs/lgfr2007.pdf). Mabadilio haya yalitokea kwa kushindwa kubuni njia mbadala na endelevu katika suala zima la mapato ya serikali za mitaa kama vile Fjeldstad na Semboja (2000) walivyoanisha.
  Upelekaji wa vyanzo vyetu vya mapato serikali kuu unazinyima halmashauri uwezo wa kujiamulia na kutekeleza vipaumbele vyao.

  Mkuu mchambuzi ni vyema pia katika mada hii tukaweka wazi kuwa mchango wa uzalishaji wa pato la taifa siyo kiashiria kizuri cha maendeleo katika ngazi hizi za chini (meso na micro level) kwani hii hubainisha uzalishaji tu na si kile kiasi kinachobakia katika mifuko ya wakaazi wa mikoa au vijiji hivi. Leo hii mchango wa uzalishaji wa pato la taifa kwa mkoa mpya wa Geita au maeneo ya mkoa wa Mara ni mkubwa sana pengine kushinda hata sehemu za mkoa wa dar es Salaam ingawa bado kuna umasikini wa kutupwa kushinda maeneo haya.
  Kwa kawaida viashiria vizuri ni vile vya pato halisi la wananchi kupitia tafiti za bajeti na matumizi ya kaya.
   
 17. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #17
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Sijui nijibu nini, ila nashangaa sana tabora yetu inabadilika pole pole sana kama vile haibadiliki kabisa. Nina imani kuwa yote hayo yanatokana na mtizamo mfupi sana wa ndugu zangu kuhusu maisha. Inapokuja wakati wa kupiga kura, wote wanakurupukia CCM tu kwa sababu walipata baiskeli, au khanga wakati wa kempeini, halafu wanasahuliwa. Kuna wakati Profesa Lipumba alikataliwa na mjomba wake ambaye ni CCM damu, eti kwa vile Lipumba na wa upinzani. Mtazamo mfupi wa ndugu zangu kuhusu maisha nadhani unachangia sana kutufanya tusiwe na maendeleo. Angalia uchaguzi wa Igunga, makada wa CCM wametuvunjia heshima kwa namna nyingi tu, lakini bado tumewapa kura.

  Ili kujibu swali hili, ni lazima nikiri kuwa sehemu zisizoendelea zina watu wenye mtizamo mfupi sana wa maisha, na hivyo watu wake wanatumiwa vibaya na CCM bila wao wenyewe kujijua. Unaweza kuona wazi kuwa mikoa yenye wabunge wa upinzani au mikoa ambayo CCM ilishinda kwa mbinde sana iko katika viwango tofauti na hii ambayo CCM ina uhakika wa kushinda.
   
 18. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #18
  Jul 28, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Hii ni thread ya muda kidogo lakini nimependa hoja zako hivyo naomba kuchangia kidogo. Kama nakusoma between the lines, CCM thrives kutokana na a belief system iliyojijenga kwenye jamii kwamba ni chama cha watu, bila ya kujali ukanda au ukabila; pia nadhani the fact kwamba Nyerere as a statesman hakutumia madaraka yake kupendelea maeneo fulani fulani ya nchi yetu, sana sana alijitahidi in a way to stall kasi ya maendeleo katika mikoa iliyopendelewa na mkoloni huku akitumia resources za taifa kujaribu kunyanyua maeneo ambayo yalikuwa nyuma kuliko mengine. Inawezekana hii strategy imechangia mikoa mingi kubaki nyuma kutokana na utekelezaji mbovu, na katika nyakati hizi, siasa za kasungura kadogo ndio zimeharibu kabisa kwani nyuma ya pazia, viongozi wanaotoka katika maeneo fulani wanajikita zaidi katika kuhakikisha wanapeleka maendeleo katika maeneo yao wakiwa madarakani. Lakini swali la msingi hapa linakuja - je how do we define maendeleo katika mazingira ya mjadala huu.

  Mimi nadhani mbali na upeo mfupi wa wananchi kama unavyosema ambao wanadanganyika na khanga na pombe za mnazi, nadhani tatizo lilipo pia ni imani ambayo bado ipo sana huko vijijini kwamba ni kwanza, kuna kasungura kadogo hivyo inabidi wananchi kuwa wavumilivu mpaka kasungura haka kakue zaidi; pili na muhimu zaidi ni kwamba wananchi wa vijijini hawajui haki zao za kikatiba - kiuchumi na kijamii na hali inakuwa mbaya zaidi pale ambapo miradi ya maendeleo inayotokana na juhudi zao kama wananchi badala ya fedha zao kama walipa kodi, inakuwa inapewa kipaumbele zaidi; kwahiyo inapotokea CCM inapita pita huko vijijini nyakazi za chaguzi, wananchi wengi wanakuwa hwataliii sana maanani kwamba ziel ahadi zinazotolewa ni haki zao za msingi, na sio hisani; lakini siku zinavyozidi kwenda mbele, taratibu upinzani unajitahidi kuwaamsha watambue kwamba wanastahili kufaidika kutokana na jasho lao ambalo ndilo linalolizalisha taifa hili mazao ya biashara ambayo yanatupatia fedha za kigeni, fedha ambazo kwa kiasi kikubwa zinabakia mijini, hasa mifukoni mwa wachache. Hivyo tusiwalaumu wananchi hawa badala yake tuwekeze katika kuwaelimisha zaidi.
   
 19. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2013
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Je, bandiko namba moja linatueleza nini kuhusu yanayojiri mtwara na pengine yatakayofuatia kwenye mikoa mingine ambayo ni rich in resources lakini yenye wananchi walala na waamka hoi?
   
 20. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2013
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Nilishawahi kusema hapa, na leo ninarudia. "MAISHA NI HATUA, KUSIWE NA 2 KWA A, KAMA HAKUNA 1 KWA B. Kusiwe na 3 kama hakuna 2 na 2" Ukishakiuka hapo USITARAJIE UTULIVU WA AINA YOYOTE KATIKA NCHI! Wanaita ni Idealism, eti ni waropokaji tu, ila haiwezekani! Wajamaa hao! Call it whatever, bado huo utasimama kuwa ndio MSINGI MAMA WA MAENDELEO YA KWELI, na kama hatuamini hilo basi ni kujitukana wenyewe kulalamikia tuyaonayo leo. The Meaningful Development must be SHARED equally! Zaidi ya hapo ni UBATILI na UPUUZI MKUBWA!
  Inasikitisha sana leo kuona Mtwara wanaona haki ya kudai huduma bora kwa vile tu kwao kumegunduliwa gesi. Jamii nayo inaona ni haki yao kupata huduma bora kwani pamepatikana gesi kwao! Huwa najiuliza binafsi, TUNATAKA KUHALALISHA NINI JUU YA HILI LA MTWARA? Je, ni haki kwa wanasingida kubaki duni kwani kwao hakuna kikubwa wachangiacho? Je, tunataka kusema barabara bora kabisa hadi vichochoroni zilizoko Moshi, ni haki yao kwani kwao unapatikana Ml. Kilimanjaro? Je, ilikuwa ni haki kwa Rukwa, Kigoma, Lindi, Singida na Tabora kama mikoa kutounganishwa na barabara za lami, wakati kuna wengine waliofikia kuunganisha wilaya zao kwa barabara za lami? Utafanyaje watu hawa wawili ili waheshimiana ama kuaminiana wakati umeshawatenga tayari? Ninauliza hivi "NGUVU ILIYOTUMIKA KUDAI HUDUMA BORA KWA WANAMTWARA, ILIKUWA WAPI HAPO KABLA? NA KWANINI IKAE KIMYA KWA SINGIDA, LINDI NA TABORA?" UNAFIKI, UNAFIKI NA USALITI KILA KONA! Pumbavu! Wanajiita wanaharakati, wengine wakombozi, lakini wote wamejaa UNAFKI. Ni WOTE!
  Watanzania wote ni sawa, ndivyo tunavyojua...sasa mbona kuna wale wanufaikao zaidi na rasilimali zetu? Wao ni aina gani ya watanzania? Na kuna aina ngapi za uananchi wa Tanzania? Na ipi imepewa uhalali wa kumiliki hisa kubwa ya matunda ya rasilimali zetu? Na kwa sababu zipi?
  Mwanamtwara ni mtanzania sawa na yule wa Dar, Mwanza, Morogoro ama Singida.
  Maendeleo ni hatua, hatua ya kwanza inatakiwa ianzie pale ambako inaweza kuwa rahisi kuwasaidia wengine kufikia hapo! Mfano, kama tumefika uwezo wa kujenga hospitali kubwa, basi kusiwe na mjadala ila ijemgwe Dodoma kwanza, sio kwasababu ni makao makuu, ila ni katikati ya tanzania. Mwanamtwara, sawa na wa kigoma, Rukwa, Kigoma, Mara, nk ndio mahali pekee wawezayo kuifikia kwa haraka pasi kuwa na wa kupoteza. Tutakapopata uwezo wa kujenga kama hyo ya pili, ipelekwe pembezoni, labda Mtwara, ama Tabora, ama Tanga, ama Mwanza. Lakini kilichopo leo, moja itajengwa Dar, nyingine Pwani, takayofuata Moro! Kwa upumbavu wetu tutashangaa kwani watu wanakimbilia Dar zaidi, kuongeza mgambo wa kuwatimua mabarabarani. Lawama si kwa Serikali tu, ni kwetu raia pia. TUPO WAPI? TULITOKEA WAPI KUYAONA YA MTWARA? Je, watanzania gani wamefikia hadhi na kupewa uhalali wa kujengewa Kigamboni wakati Mtwara wamekosa maji safi na salama? TUNAHALALISHA NINI?
  Sitaacha kumfundisha mwanangu kumvizia na kumdhuru yule aliyejenga ghorofa katikati ya vibanda vyetu vya makuti. HAKIKA HUYO SI MWENZETU.
  Mungu wetu anaita sasa!
   
Loading...