Kwanini "michepuko" ihalalishwe kwa wanaume?

Roger Sterling

JF-Expert Member
May 10, 2015
12,213
2,000
Inawezekana ni ubinafsi, pengine upumbavu, ila nipe nafasi ya kuelezea.

Ki-DHANA
Hakuna mwanaume mwaminifu kwa mpenzi mmoja(All men cheat): Hii dhana imeletwa na kusisitizwa na wanawake wenyewe, na hakuna jinsi unaweza kuwafanya wakubali kuwa ni potofu. Kwao, wanaume tumezaliwa na vinasaba vya kutoridhika na mwanamke mmoja, pengine ni kweli. Sasa basi, kama tayari hatuaminiki, kuna haja gani ya kujaribu? Na kama ndivyo tulivyoumbwa, kwa nini tuhukumiwe?

KIMAHESABU.
Kitakwimu, duniani wanawake ni wengi zaidi ya wanaume. Na kuna msemo ambao pia umeanzishwa na hutumiwa na wanawake kuwa "wanaume wazuri wameshachukuliwa(all good men are taken)". Wewe mama ambaye una bahati ya kuwa kwenye ndoa/uhusiano na mwanaume wako, hebu jaribu kuwa katika viatu vya yule ambaye amekosa kwa sababu tu jamaa alikuona wewe kabla yake. Kwa nini msiache ubinafsi na kuchangia hicho hicho kidogo kilichopo?

Hapo hapo katika hesabu; kwa wale wanaoamini katika biblia (sina uhakika kuhusu vitabu vingine), imeandikwa kuwa mwanamke ametoka katika ubavu wa mwanaume ("Then the LORD God made a woman from the rib he had taken out of the man, and he brought her to the man."). Sasa piga hesabu mwanaume ana mbavu ngapi, na hiyo ndiyo idadi ya wanawake ambao anaweza/alistahili kuwamudu.


Ki-BAOLOJIA.
Kuna sababu kadhaa za kibaolojia zinazoashiria wanaume hawakutakiwa kuwa na mpenzi mmoja pekee. Moja ni suala la hedhi. Kila mwezi wanawake waliokwisha vunja ungo, huingia katika siku zao ambazo si salama wala haishauriwi kushiriki ngono. Ukizingatia kuwa wanaume mahitaji yetu ya kingono ni zaidi ya ya wenzetu(hatukujiumba hivyo), ni haki kuwa na back-up ili ikitokea tumezidiwa na ni moja kati ya siku za hatari za mmoja wa wapenzi wetu, tuweze kuhudumiwa.

Vivyo hivyo katika suala/kipindi cha uzazi.

Pia wanawake hupoteza hamu na uwezo wa kushiriki tendo kadiri umri unavyosogea, tofauti na wanaume.
 

Raimundo

JF-Expert Member
May 23, 2009
13,502
2,000
Ninapinga kabisha hii hoja, wengine tuna michepuko 10 sasa tuhalalishwa vipi?
Kila mmoja anakuhalalisha kivyake, muhimu usiwagonganishe.

Yaani anakutambulisha kwa mke wake kwamba huu ni mchepuko wangu halali, then mwingine hivyo hivyo kwa muda ambao wewe utaona unafaa kutowagonganisha.
 

Kisebengo Kibobori

JF-Expert Member
Oct 29, 2016
297
500
Kiuhalisia mwanaume kuchepuka sio basic need bali ni necesary need .. Lkn ili kulinda dhana ya mchepuko wife hatakiw sio tu kujua bali hata kuhis kama kuna kitu kama hicho kinaendelea na inanoga zaid pale unaechepuka nae nayy pia anakuconsider ww kama mchepuko wake yaan awe mke wa mtu hapo mtakua salama saaaana coz kila mtu anaenda kwa tahadhari akizngatia kutokuharibu ndoa yake....
Always kuchepuka kunaleta game flan hv amazing coz kila mtu anajitahid kumfunika huyo anaemuibia
 

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
22,967
2,000
ni ujinga na unafiki mwanaume kusex na mwanamke mmoja maisha yake yote.hata Mungu hakusema hivo
anzia adam ,kina mzee Ibrahimu,yakobo,na wengineo wazee wa heshima zao kina Daudi na suleimani hakuna kitu kama hicho cha kuabudu papuchi moja .kizazi hiki ndo mtaweza? acheni unafiki nyie watu
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
43,069
2,000
Sio michepuko kwa ujumla, bali kwa wanaume pekee.
Bado ninapinga mkuu, kwanza kuna risk ya kuambukizana magonjwa, pili ni quality time ya kuwa na mke wako utaipata saa ngapi? Ninadhani dhana nzima ya kuwa na mke mmoja ilikuwa sehemu ya socialization au ustaarabu na kuhakikisha mali inakuwa controlled katika kundi la familia pia dini. Kwanini kule Cana Yesu asifungishe ndoa ya wake wengi?
 

CHARMILTON

JF-Expert Member
May 30, 2015
6,348
2,000
Kweli kabisa Mkuu, umenena jambo la msingi sana.

Hatuwezi kuwa na mwanamke mmoja ilhali sex-drive zetu hazilingani.

Mwanamke ana wakati maalumu wa kuhitaji ngono lakini sisi ni 24/7 throughout the year.

Mimi nadhani mwanaume anatakiwa awe na wanawake minimum wanne au watano.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
43,069
2,000
Do haya mambo ya siri haya, ninakumbuka kuna baba alikuwa na familia yake, mama yake alikuwa mgonjwa basi alimuomba radhi mkewe kuwa ana watoto wa nje na angependa waje wamuone bibi yao, iwapo kifo kitamfika angalau wawe wametia machoni. Mama wa watu alikubali, watoto wameletwa ni 9, mke alibaki mdomo wazi, mume wangu katika miaka yote ya ndoa, muda wa kuzaa watoto 9 wengine uliupata wapi?
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
43,069
2,000
Kweli kabisa Mkuu, umenena jambo la msingi sana.

Hatuwezi kuwa na mwanamke mmoja ilhali sex-drive zetu hazilingani.

Mwanamke ana wakati maalumu wa kuhitaji ngono lakini sisi ni 24/7 throughout the year.

Mimi nadhani mwanaume anatakiwa awe na wanawake minimum wanne au watano.
5-7 days out of 30 days of the month? Jamani mbona mnakuwa maselfish?
 
Top Bottom