Nimesikitishwa sana na kitendo cha mwanaJF mwenzetu kumzushia kifo Mwenyekiti wa Tume huru ya uchaguzi Kenya IEBC bwana Wafula Chebukati, kitendo hicho si cha kiungwana, kiutu na kidiplomasia hata kidogo. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi sio mtu mdogo, hivi serikali ya Kenya na wananchi wa Kenya wakisikia kuwa Watanzania wamemzushia kifo kiongozi wao watatufikiriaje, kwamba tunataka vurugu zitokee ili tupate nini, hatuoni kwamba kitendo hicho ni cha kuongeza uhasama baina ya nchi yetu na Kenya.
Uchaguzi wa Kenya umeshaisha na mshindi kapatikana kama aliyeshinda hukumtaka lakini ni vyema kuheshimu maamuzi ya wakenya wenyewe hakuna haja ya kuwaombea mabaya.
Aliyezusha ni mwanaJF mwenzetu nitashangaa sana kama MODS wataendelea ku entertain vitu hatari kwa ustawi wa ujirani mwema kama hivi.
Kama ni utani na kuzushiana mambo ya kisiasa kama haya tufanyiane humu ndani lakini tusivuke mipaka.
Ni Ushauri tu.