Kwanini Marekani ameshindwa kuimaliza Iran haraka?

Huu ndiyo Ubazazi na Udunya ambao nimekuwa nikiusema hapa muda mrefu.

War is waged on Objectives, if the Objectives are not accomplished then it's a waste of time.

Lengo kuu la Marekani kuvamia Iran lilikuwa ni Decapitation-Insurection-Collapse. Ilitakiwa saa hizi watu wawe wameingia barabarani wameshaipindua serikali na vikosi vya Marekani, Israel, UAE, Qatar, Kurd na NATO wameingia na kumalizia kazi dhidi ya Iran. Lengo kuu halijafanikiwa, kama kule Vietnam.

Tatizo jingine ambalo wewe hulitizami na unafanya ushabiki hapa ni kwamba Marekani ni tofauti na Urusi kwasababu anamiliki kambi za jeshi Middle-East yote. Kisheria kambi za jeshi ni kama Ubalozi, zinachukuliwa kama eneo la nchi (Territory of America). Ndiyo maana ukishambulia kambi ya jeshi unakuwa umetangaza vita dhidi ya nchi husika. Lakini jingine, vita hatupigani kwa kushindana kuua raia (Civilians) ambao wanalindwa na sheria, tunashindana kuua wanajeshi wanaopigana (Combatants).

Kisiasa utaweza kuona utaofauti kwasababu ninyi mnataka iwe Conventional Warfare, lakini ukweli ni kwamba hii ni ASYMETRIC WARFARE kama kule Vietnam na Afghanistan. Mwaka 1979 Urusi alivyovamia Afghanistani alifanya vilevile kama ambavyo Marekani amefanya kwa Maduro-Venezuela na kwa Ayatollah-Iran. Warusi walivamia Ikulu Kabul na kumuua Raisi wa nchi na viongozi (A Decapitation). Baadaye vita iliyotakiwa iwe ya wiki, ikaishia kuwa ya miaka 15, iliyojaa mauamivu.

Urusi alidhibiti anga lote la Afghanistani kwa ndege za kisasa zilizofanya mashambulizi, lakini hawakushinda vita. Waliua maelfu ya watu lakini lengo kuu la kuitawala Afghanistan halikufanikiwa. Marekani hata ajaze madege ukanda wote ule, tayari lengo la kwanza halijafanikiwa, na walau ungekuwa umesoma masuala ya kiusalama ungefahamu kwamba vita hatushindi kwa kupitia jeshi la anga (Air-Force), bali jeshi la ardhini (Army/Infantry) ambapo itatakiwa Marekani na Israel wavamie Iran nchi ambayo imezungukwa na milima kama Afghanistani.

Hivi umeiona hata ramani ya Iran, jinsi ilivyo kweli ???

Marekani akijidanganya kuvamia kijeshi Iran, aisee watachinjwa kama kuku. Kiufupi kama alishindwa kulitawala (Occupy) taifa la Iraq, dogo lenye watu milioni 20, ataweza kweli kulitawala taifa la Iran kubwa mara nne ya Iraq na lina watu milioni 100 ??? Hivi mnavyojibugi hivi huwa mnakuwa mmkunywa nini wajameni ??? Ati bro ???
​
 
Tupo hapa,
Wiki ya kwanza ndiyo ishakata hivyo....
Wiki ingine ikiisha ntakuita hapa, lakini usikimbie.....
​
 
Fuct
 
HATA wewe unalinganisha visivyolinanishika,hakuna kitu Cha maana ulichoandika.

1) Iran Ina vikwazo Kwa zaidi ya miaka 40,wakati Ukraine Haina vikwazo vyovyote.

2) Ukraine ilikua inafundishwa na NATO kwa miaka zaidi ya minane ,wakati Iran ikiwa Iko vikwazoni

3) wiki ya kwanza TU ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ilikaribia kuingia Kiev,west wakaidanganya Urusi kua Ukraine Iko tayari kwa mazungumzo,wakaenda uturuki kuongea kumbe NATO wanajipanga kumsaidia Ukraine,
Ndio maana Hadi Leo NATO wapo Ukraine .
Wakati Iran anahangaika peke yake.
4) Sio mpango wa Urusi kumuua Zelensky wala Regime change Ukraine Bali Ukraine isijiunge NATO na haijajiunga.
Wakati Israel na USA waliidanganya Iran kua wiki ijayo mazungumzo yataendelea ndio ikapelekea Viongozi wa Iran kutoka na hofu ya kuvamiwa walikaa au waliishi Kwa Imani kua wiki ijayo wataemdelea na mazungumzo,walijiachia,kumbe wenzao ni waongo na hawakua waaminifu,walavamia na kumuua Ayatollah na wenzake,wakati Israel na USA wakifanya hayo Benjamin Netanyahu alikimbilia ujerumani kujificha.
5)Iran sera Yao sio kuua Viongozi wa nchi nyingine ,wakati Isarel sera yake ni kuua Viongozi wa nchi maadui
Vivyo hivyo kwa Urusi na Ukraine Urusi Haina mpango wa kumuua Zelensky wala viongozi wa Ukraine lkn Ukraine na west sera Yao ni kuua Viongozi wa nchi nyingine(Ugaidi).

6) Vita vya Urusi imechukua miaka minne Urusi ikipigana na Ukraine inayosaidiawa na All collective west,wakati vita vya Israel-USA - Iran bado haijaisha,tusubiri itaisha lini ndio tuone ulinganifu.wakati Iran ikipigana peke yake dhidi ya Israel Marekani Qartari,Sound Arabia, Jordan,UAE, Bahrain,n.k ambazo zilisaidia sana kuangusha makombora ya iran

7) Iran haijashambulia marekani moja kwa moja kwa sababu za kijiografia na Irani Haina uwezo huo,lkn imepiga Kambi zote za jeshi za USA na ndani ya ardhi ya Israel,hii maana yake kama Marekani ingekua ilipo Turkyl eo hii nayo ingepigwa.
Hata hivyo Kambi za kijeshi za USA ni sehemu ya Marekani kijeshi hivyo zingeachwa zingeshiriki kuipiga Irani,ndio lengo la kuwepo makambi hayo kuirahisishia marekani kuishambulia nchi jirani na Kambi hizo.
Lakini kwa bahati mbaya kwa marekani wanajeshi wote wa USA waliokua kwenye Kambi hizo wamezikimbia kabla na baada yavkupigwa,hivyo lengo la kujenga kabisa hizo limefeli aubhalijasaidia kitu.
8) Abraham Lincoln imeshambuliwa na ikahamishwa au kukimbizwa,hivyo Nayo umeshindwa kufanya kazi iliyokusudiwa au iliyosababiswa kupelekwa ghuba.
9)kama alivyosema mtoa mada toka Dunia hii iumbwe hii ni mara ya pili baada ya Miaka mingi kwa marekani kupigwa kwa miundombinu yake ya kijeshi silaha na vifaa vingine kama rada viwanja vya ndege na bandari za melivita na kuharibiwa vibaya kama kama ilivyotokea ndani ya siku nne TU,baada ya Pearl Harbour attack.
10) katika histotia ya Dunia hakuna kipindi ambacho Marekani ameomba msaada kijeshi kama mwaka huu,na hata kaomba Msaada wa viwanja vya kurushia ndege zake na kanyimwa na Hispania,Sasa najiuliza Kambi zake za middle east zimemsaidia Nini na alizijenga za Nini?
Katika historia ya USA haijawahi kushindwa kuokoa raia wake kwa maelfu waliokwama middle east kama kipindi hiki.,wamekwama aisee.maana kule ghuba ndege za kiraia zimeshindwa kuruka.
Kwa kifupi Iran kazua balaa kubwa.
11) Kuna uzuiaji mkubwa wa habari za Iran inaposhambulia Israel na USA,habari zinatoka kwa kuchujwa mno tofauti na habari zinazorushwa kutoka Vyombo vya magharibi zikiishambulia Iran.
Tutayajua mengi baadae.
12) Sina uhakika lkn inasemwa USA aliiomba Italy ikaiombe Iran wayamalize iache vita ,Iran ikakataa kumaliza vita.
 
Bwana Armata, Marekani ya leo 2026 haina nguvu kama Marekani ya 1964.

Marekani ya mwaka 1964 was a formidable military behemoth lakini alishindwa Vietnam.

Anga lote la Vietnam lilikuwa limejaa ndege za Marekani huku chini wamejaa maelfu ya askari.

Marekani alilipua hivihivi na kufutilia vijiji vya watu ambapo mwishowe aliuawa watu milioni 4.

Alifanya yote lakini akashindwa....

Wanachoshindana sasa Marekani na Iran ni PAIN-ABSORPTION, ambapo kweli Iran katandikwa kelubu za kutosha na kutisha. Haya ambayo Marekani kafanya Iran, yangefanyika kwingine nchi ingekuwa ishaparanganyika. Mpaka sasa Iran katushangaza, serikali yote haipo lakini bado wanapigana vita. Sasa Marekani naye ameguswa, na Iran analenga kufanya kilekile alichofanya Vietnam (Kill many American Boys and send them home in body bags). Iran akiweza kuua hata Wamarekani 5000 tu, kelele zitatokea nyingi mno Marekani na Donald Trump na Pete Hegseth watashughulikiwa ipasavyo.

Ponapona ya Marekani ni kushinda hii vita, jambo ambalo haliwezi kufanyika kwa kuua majenerali. Mwaka 1934 kwenye Chinese-Civil War, Chiang-Kai Shek aliua maelfu ya wanajeshi wa Mao Zedong wakiwemo majenerali lakini yote hayo mwisho wake alichoka yeye, maana wakomunisti walikuwa wamejikataa, wakamshinda akakimbilia Taiwani mwaka 1949.

Likivuka hili wiki tu, wiki ijayo utatembea hapo Dar kwa mguu nakwambia. Mbaya zaidi hadi kule USA, Europe kutakuwa na hali mbaya maana Iran anashambulia Energy Infrastructure kuhakikisha kwamba Attack zake zinakuwa na The Multiplier Effect. Wamarekani wako mbali na Iran, lakini Iran has sent them A War Bill. Mfumuko wa bei utakaotokea Wamarekani watakuwa wa kwanza kuumia. Tena sanaaa.
​
 
Kuvamia taifa jingine huru, kijeshi kwasababu linafanya maamuzi yake kisiasa ni kosa kisheria.

Urusi mwenyewe aliwaruhusu Wayukraini watoke kwenye Muungano mwaka 1991.

Kinachofanyika hapa ni siasa za mataifa makubwa (Great Power Politics) ambapo ukweli mchungu ni kwamba sheria inakataza, ila uhalisia ni kitu kingine, kwamba ukiingilia maslahi ya taifa kubwa halafu wewe ni kitaifa kidogo ndiyo madhara ambayo yanaikuta Ukraine. Sheria inamlinda Ukraine, lakini uhalisia wa siasa za dunia una taswira nyingine kabisa. Marekani na NATO walimponza Ukraine, naye akijidanganya akaingia mazima, mwishowe yakamkuta.

Taiwan na Japan wasipojifunza watakuja kupigwa na kitu kizito nao wasiamini.....

​
 
Umenena vyema, mimi nashangaa Mtanzania anayeongozwa na ccm akawa na maarifa ya kusoma ramani ya mapambano kumshinda Trump aliyezungukwa na CIA na MOSSAD juu.

CIA na MOSSAD zikae chini for years waje na suluhisho halafu mtu uje tu uone US na Israel zimekosea, HAPANA.
 
Wewe jamaa yangu unachekesha sana! Yaani unadiriki kabisa kuiita japani kuwa ni taifa dogo?
Kama eneo ndiyo ukubwa wa taifa basi Tanzania ni taifa kubwa kuliko taifa lolote la ulaya. Japani ni taifa la 3 kwa ukubwa kiuchumi duniani na lina watu milioni 125 how unasema ni taifa dogo?
 
Iran yuko kwao lakini mashambulizi yake yote yatamfikia kila Mmarekani kule Hollywood na Chicago. Mashambulizi ya Iran mbali tu na kuua wanajeshi, yana The Economic Multiplier Effect kwasababu hii vita inapiganwa World's Major Energy Choke-Point. Sasa mabazazi na madunya, yenyewe yanadhani kwamba Iran anataka kuua wanajeshi tu. Iran anataka kuua wanajeshi, lakini kubwa zaidi ni kuvuruga mlolongo mzima wa usalama wa nishati ya dunia (World's Energy Security).

Kama ikiendelea hivi, hadi wale Wamarekani wa Tandale watamlaani Donald Trump na Benjamin Netanyahu kwa kuvamia Iran. Mfereji wa Hormuz ukifungwa tu, na miundombinu ya mafuta ya Saudi Arabia, UAE na Qatar ikalipuliwa kule Marekani kutakuwa na madhara makubwa mno kiuchumi, hasa kwenye mzunguko wa dola (Dollar Circulation).

Maumivu yakiwa makubwa, watakaolaumiwa ni WAYAHUDI WA MAREKENI (The Israel Lobby) na Netanyahu kwasababu ukisikiliza kina Tucker Carlson wanalaumu hii vita kwa Israel na magenge ya Wayahudi wa Marekani ambao wanailazimisha Marekani iingie vitani ilhali hawana maslahi huko.
​
 
Mtanzania mwenye akili ni lazima afahamu kwamba CIA na MOSSAD siyo makampuni ya mafuta.

Pia Mtanzania mwenye akili ni lazima afahamu kwamba uchumi wa dunia unaendeshwa na Fossil Fuels, hivyo kinachotokea Ghuba ya Uajemi hakihitaji PhD in Economics kufahamu kwamba wiki zijazo hata yeye mwenyewe anaweza akawa anapiga jalamba kutembea ya mguu kutoka Mbezi-Beach hadi Mwenge.

Akili ni nywele, kila mtu ana zake....
​
 
US kaingia cha kike safari hii
Karuka sarakasi huku kavaa taulo.....

Ukweli mchungu ni kwamba, The Persian Gulf (Ghuba ya Uajemi) ni eneo ambalo linatuwezesha hata mimi na wewe kuweza kuwasiliana hivi hapa mtandaoni. Ni eneo ambalo linaathiri maisha yetu kwa kiwango kikubwa kupita maelezo. Tatizo ni kwamba Mabazazi na Madunya ya humu ndani yanadhania kila kitu ni ushabiki ilhali hayafahamu kwamba wahanga wa kwanza wa Energy Crisis watakuwa wao kwasababu ya mfumuko wa bei (Inflation) na uhaba wa dola (Dollar Scarcity) kwasababu mafuta ni moja ya bidhaa inayoongozwa kusambaza dolla hapa duniani.

Kiukweli Trump kacheza vibaya mno, na aliyemshauri (Netanyahu) katulia pembeni....
​
 
Unachekesha wewe ambaye umeshindwa kusoma kwa ufahamu.

Japan kwa Uchina ni taifa dogo mno.

Japana kwa Uchina ni dogo kiuchumi, dogo kiukubwa, dogo kieneo, dogo kitamaduni na dogo kiumri.

Japan ni kubwa kwako wewe mtanganyika chogo a.k.a Bazazi Bin Dunya ila dogo kwa Uchina....
​
 
kwenye namba 5.
Nilitegemea ungetumia akili kidogo kufanya comparison ya kijiografia kati ya IRAN na USA kulinganisha RUSIA na UKRAINE..
Niliiacha kimtego ili mdhihirishe uvivu wa Urusi. Ukitumia akili ya kijiografia unaona Urusi ilivyo na advantage kwenye kuishambulia Ukraine.

Marekani inasafiri kwa ndege na meli kilomita 7,000 kuifuata Iran, wakati Urusi hata kwa miguu inaifikia Ukraine, mwaka wa nne huu.
 
Iran kwa sasa ipo kwenye wakati mgumu mno.

The regime is focused on surviving not winning.

T14 Armata
 
Mabazazi na Madunya wa humu ndani akili zao ziko likizo....

Mimi nimekuwa nao humu ndani tokea mwaka 2012 na nimesema nao sana.....

Walinitukana sana miaka ya 2016-2018 kuhusu siasa za dunia, mwaka 2022 wakazidisha......

Ila sasa naona wanaanza kuelewa kwamba International Politics is not a Masturbation Contest....

International Politics Affects Their Daily Lives....But these fools can't comprehend the gravity...

Binafsi napenda hii vita iendelee ili Mabazazi na Madunya ya Mbezi, Kawe, Mwenge na Masaki yajifunze, pale siku watapoambiwa wapaki gari nyumbani, huku Google ikiwa haifanyi kazi kisa Data Centres zimelipuliwa. Kiukweli hii vita ni ya kifala sanaa...
​
 
When you throw a stone to a pack of dogs, the first one to holler is a bitch hit by the stone.....​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…