kwanini marapa wa kike wameadimika Marekani karne hii?

orangutan

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
757
773
Kipindi cha miaka ya 1990-2000s mwanzoni hivi tumeshuhudia kukitokea marapa wengi wa kike waliokuwa wana uwezo mkubwa kwenye rap game ya USA. Baadhi ya marapa wa kike walioibuka miaka hiyo na kufanikiwa kutesa kwenye gemu la rap ni hawa wafuatao;
Lauryn Hill, Remmy Ma, Lil Kim, Da Brat, Eve, Missy Elliot,Queen Latifah, Foxy Brown, Mc Lyte, Vita, Salt-n-Pepa, Trina, Roxanne Shante, Rah Digga, Lil Mamma, Azaelia Banks hao wakiwa ni baadhi tu.Hawa marapa walifanikiwa ku-hit kwa muda mrefu na kufanikiwa kujitengenezea majina na umaarufu mkubwa kwenye hiphop na rnb. Na kuna baadhi yao mpaka leo hii bado wanaenda kutoa kazi nzuri au kutoa ladha adimu wanapopata cjance ya kufanya hata collab, kwamfano Lauryn Hill, Eve, Missy Elliot, Lil Kim na Eve.
Miaka ya 2000 katikati na kuendelea kumetokea ukame mkubwa wa marapa wa kike huko USA. Katika kipindi hiki tumewaona marapa wapya kama akina Nikki Minaj, Angel Haze, Rhapsody, Iggy Azaelia, na wengineo ambao hawajafanikiwa kujitengenezea jina kama walivyofanya wenzao wa kipindi hicho cha miaka ya 90s. Na ndio maana Nikki Minaj amefanikiwa kuwaburuza marapa wenzake hao kwenye category ya rapa bora wa kike kwa zaidi ya miaka saba mfululizo. Hii ni kwasababu iliyo dhahiri kabisa kuwa kwasasa hakuna ushindani tena wa marapa wa kike kama ilivyokuwa kipimdi hicho cha nyuma.

Wataalamu wa mambo karibuni jukwaani mchangie ni kwanini katika kipindi hiki marapa wa kike wamekuwa bidhaa adimu sana kwenye rap game. Eti leo hii Young MA nayeye anajiona ni hot rapper! WTF
 
Unajua kwenye muziki nako wakinadada wanategwa sana, na ili utoke mara nyingi lazima uwavulie watu chupi, hili limekuwa kikwazo sana kwa wanamuziki wakike....wako wanamuzili wengi ila ndo hivyo huishia kuimba vyumbani mwao, muziki unaacha alama mbaya sana kwa mwanamke tofauti na kwa mwanamme, wanawake wengi huwa na ndoto za kufika mbali kabla hawajajua figisu za mziki, lakini wakishaanza halakati zao ndo huona mambo mengi ya kukatisha tamaa kwao.ndi maana unakura wanaokuja kufika mbali huwa wachache sana, sio kwenye rap tu na rnb ila ni karibia aina nyingi za miziki wanawake ni adimu.
 
mkuu uko sawa. nimeielewa point yako
 
Huyu EVE huyu alikuwa matata sana pana kibao kinaitwa gotta man hilo beat lake tu mimi huburudika achilia mbali maneno
 
Back
Top Bottom