Kwanini mara kadhaa binadamu anapokaribia kufa huhisi aibu?

Kwanini mara kadhaa binadamu anapokaribia kufa huhisi aibu?

Umejuaje kua wote wanajisikiaga aibu? Mwingine anaweza kuwa na shida zake tu zinazomfanya ajisikie ivo...
 
ni kweli lazima mtu anapo karibia kufa anachangamka kwa sababu huko tunako kwenda ni kuzuri sana, hakuna magojwa, wala kuugua hakuna kula, hakuna kuvaa, ni kuzuri sana sana tuta vaa mwili wa kiroho spiritual body usiyo haribika tutaepukana na tabu za Dunia hii bibilia inatuambia wazi nyumbani kwa baba yangu kuna makao mengi kama sivyo ningeliwambia ili mradi uishi maisha yanayo mpendeza Mungu sikuzote za Maisha yako ukiwa hapa Duniani.
 
Wakuu,

Nina maswali mawili matatu kuhusu maisha yetu kama wanadamu tunayoyaishi kila siku kabla mauti hayajatukuta, Ninahitaji kujua kwamba ni kwanini mtu ambaye pengine alikuwa mgonjwa au vinginevyo, kwanini anapokaribia kufa anahisi aibu?

Tukumbe kwamba kuna ukweli usiopingika kwamba tunajikunyata mtoto mdogo anapouliza kwanza swali hili, "kufa maana yake nini? Tunaywea kuzungumza au hata kufikiri juu ya mtu fulani tumpendaye anapokaribia kufa. Mauti ni adui wa watu wote kila mahali.

Sisi sote kwa wakati fulani, labda baada ya kufa rafiki yetu au mpendwa wetu, tumejisikia kana kwamba tumbo liko tupu, yaani, kuwa na hisia ile ya upweke inayopita ndani yetu tunapoangalia kwa haraka kuona mwisho wa uhai wa mtu.

Katika jambo hili la maana sana, lililojaa hisia nyingi, ni wapi basi, tunakoweza kujifunza habari za kile kinachotokea tunapokufa? Kwa bahati nzuri, sehemu ya utume wa Kristo hapa duniani ilikuwa ni "kuwaweka huru wale ambao katika maisha yao yote walikuwa katika hali ya utumwa kwa hofu ya mauti" (Waebrania 2:15). Na katika Biblia, Yesu anatoa ujumbe wenye faraja, kisha anajibu maswali yetu yote juu ya mauti na yale maisha ya baadaye kwa njia inayoeleweka wazi.

Mtu anapokufa kinyume cha hatua zile za uumbaji zilizoelezwa katika Mwanzo 2:7 hutokea "Nayo mavumbini huirudia ardhi yalikotoka, nayo roho (pumnzi ya uhai) humrudia Mungu aliyeitoa." - (Mhubiri 12:7).

Mara nyingi kwa wale Wakristo sijajua kwa wenzetu Waislam kuwa hili likoje lakini 'Biblia' hutumia maneno ya Kiebrania yamaanishayo "pumzi" (breath) na "roho" (spirit) kwa kubadilishana. Watu wanapokufa, mwili wao unageuka na kuwa "mavumbi" na "roho ("pumzi ya uhai") humrudia Mungu aliyeitoa. Lakini, je! kunatokea nini kwa ile roho hai (living soul)?

Mungu anapoiondoa kwetu pumzi yake ya uhai aliyotupa, roho yetu hufa. Lakini kama tutakavyoona baadaye katika somo hili, tukiwa na Kristo tumaini liko.

Kaka Pasco na mshana jr, mnaweza kutufungulia mjadala????

Asante..

Nimechelewa kuja, lakini si mbaya ngoja nijiandae nakuja
 
Hii mada ni nzuri na ina ukweli. Kwenye Biblia tunapewa majibu juu ya hili. Kuna aina mbili za maisha baada ya kifo.

1. Mtu anayekufa akaenda mikononi mwa Mungu ("Ufunuo 13:13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao."). na,

2. Mtu anayekufa na kwenda hukumuni ("Luka 16:
23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. 24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.").

Sasa ukiona mtu ana amani na furaha kisha akafa, huyo amepokelewa mikononi mwa Bwana Yesu, na anafurahia kufa maana huko aendako ni kuzuri kuliko huku duniani. Wakati ukakuta mtu anahangaika, anajipiga-piga, anahofu na huzuni kabla ya kufa, ujue huyo ameingia kwenye taabu kuu!

Kifo kipo ila kuna dawa ya kukishinda usikiogope, nayo ni damu ya Bwana Yesu inayosafisha dhambi. Ukisafishwa dhambi zako una ujasiri wa kukikabili kifo kwa furaha ("1 Wakorintho 15:
55 Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako? 56 Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. 57 Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.").

***** Bwana Yesu alishinda kifo kwa ajili yako*****
 
Wakuu,

Nina maswali mawili matatu kuhusu maisha yetu kama wanadamu tunayoyaishi kila siku kabla mauti hayajatukuta, Ninahitaji kujua kwamba ni kwanini mtu ambaye pengine alikuwa mgonjwa au vinginevyo, kwanini anapokaribia kufa anahisi aibu?

Tukumbe kwamba kuna ukweli usiopingika kwamba tunajikunyata mtoto mdogo anapouliza kwanza swali hili, "kufa maana yake nini? Tunaywea kuzungumza au hata kufikiri juu ya mtu fulani tumpendaye anapokaribia kufa. Mauti ni adui wa watu wote kila mahali.

Sisi sote kwa wakati fulani, labda baada ya kufa rafiki yetu au mpendwa wetu, tumejisikia kana kwamba tumbo liko tupu, yaani, kuwa na hisia ile ya upweke inayopita ndani yetu tunapoangalia kwa haraka kuona mwisho wa uhai wa mtu.

Katika jambo hili la maana sana, lililojaa hisia nyingi, ni wapi basi, tunakoweza kujifunza habari za kile kinachotokea tunapokufa? Kwa bahati nzuri, sehemu ya utume wa Kristo hapa duniani ilikuwa ni "kuwaweka huru wale ambao katika maisha yao yote walikuwa katika hali ya utumwa kwa hofu ya mauti" (Waebrania 2:15). Na katika Biblia, Yesu anatoa ujumbe wenye faraja, kisha anajibu maswali yetu yote juu ya mauti na yale maisha ya baadaye kwa njia inayoeleweka wazi.

Mtu anapokufa kinyume cha hatua zile za uumbaji zilizoelezwa katika Mwanzo 2:7 hutokea "Nayo mavumbini huirudia ardhi yalikotoka, nayo roho (pumnzi ya uhai) humrudia Mungu aliyeitoa." - (Mhubiri 12:7).

Mara nyingi kwa wale Wakristo sijajua kwa wenzetu Waislam kuwa hili likoje lakini 'Biblia' hutumia maneno ya Kiebrania yamaanishayo "pumzi" (breath) na "roho" (spirit) kwa kubadilishana. Watu wanapokufa, mwili wao unageuka na kuwa "mavumbi" na "roho ("pumzi ya uhai") humrudia Mungu aliyeitoa. Lakini, je! kunatokea nini kwa ile roho hai (living soul)?

Mungu anapoiondoa kwetu pumzi yake ya uhai aliyotupa, roho yetu hufa. Lakini kama tutakavyoona baadaye katika somo hili, tukiwa na Kristo tumaini liko.

Kaka Pasco na mshana jr, mnaweza kutufungulia mjadala????

Asante..

Nilishawahi kuweka mada inayofanana na hii hapa jukwaani, kiukweli sio aibu bali ni mchanganyiko wa mambo mengi woga wasiwasi huzuni nknk, na kuna baadhi yetu huonyeshwa maisha yetu ya nyuma Kama mkanda wa video kabla ya kukata roho
 
Kifo kina aibu.utu unapotaja kutoka huona binadamu wenine kama viumbe tofauti ndio maana huona aibu.hata ivo kifo huja kwa style yake hata akichangamka wakufa au kugeuka kitandani Jambo kubwa ni kwamba huwezi kuona jicho la kufa linapofumba eidha mtajisahau kupiga story au kuendea kitu kwa ajili ya mgonjwa hapo kifo hupata nafasi ya kuingia.

Kwa wenye imani ya kulokole na roho mtakatifu hutaarifiwa mapema ndiyo maana hata kama haumwi wengine huweza kuaga kabisa kuwa muda fulani atamaliza safari yake.

Dalili za kufa:

Ukianza kuota unaongea au kuona watu waliokufa unaowajua ni dall mbaya.

Kuota umepapanda ndege halafu hufiki unakokwenda ni dall

Dalili hizi unaweza kuziona na ukichukua hatua ya kukemea kwa maombi ya kumaanisha kifo kinaeeza kuahirishwa na Mungu au wakati mwingine Inawezekana ni kifo kinachotaka kusabbidhwa na nguvu za kichawi su ajali.Mungu husikia kilio chako.

Kwa leo ni hayo.
 
Halafu kama sikosei huyu kaka aloleta huu uzi nae alitangulia mbele ya haki mwaka jana kwa ajali,
R I P Dotto
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom