Dotto Mnzava
R I P
- Mar 6, 2014
- 864
- 427
Wakuu,
Nina maswali mawili matatu kuhusu maisha yetu kama wanadamu tunayoyaishi kila siku kabla mauti hayajatukuta, Ninahitaji kujua kwamba ni kwanini mtu ambaye pengine alikuwa mgonjwa au vinginevyo, kwanini anapokaribia kufa anahisi aibu?
Tukumbe kwamba kuna ukweli usiopingika kwamba tunajikunyata mtoto mdogo anapouliza kwanza swali hili, "kufa maana yake nini? Tunaywea kuzungumza au hata kufikiri juu ya mtu fulani tumpendaye anapokaribia kufa. Mauti ni adui wa watu wote kila mahali.
Sisi sote kwa wakati fulani, labda baada ya kufa rafiki yetu au mpendwa wetu, tumejisikia kana kwamba tumbo liko tupu, yaani, kuwa na hisia ile ya upweke inayopita ndani yetu tunapoangalia kwa haraka kuona mwisho wa uhai wa mtu.
Katika jambo hili la maana sana, lililojaa hisia nyingi, ni wapi basi, tunakoweza kujifunza habari za kile kinachotokea tunapokufa? Kwa bahati nzuri, sehemu ya utume wa Kristo hapa duniani ilikuwa ni "kuwaweka huru wale ambao katika maisha yao yote walikuwa katika hali ya utumwa kwa hofu ya mauti" (Waebrania 2:15). Na katika Biblia, Yesu anatoa ujumbe wenye faraja, kisha anajibu maswali yetu yote juu ya mauti na yale maisha ya baadaye kwa njia inayoeleweka wazi.
Mtu anapokufa kinyume cha hatua zile za uumbaji zilizoelezwa katika Mwanzo 2:7 hutokea "Nayo mavumbini huirudia ardhi yalikotoka, nayo roho (pumnzi ya uhai) humrudia Mungu aliyeitoa." - (Mhubiri 12:7).
Mara nyingi kwa wale Wakristo sijajua kwa wenzetu Waislam kuwa hili likoje lakini 'Biblia' hutumia maneno ya Kiebrania yamaanishayo "pumzi" (breath) na "roho" (spirit) kwa kubadilishana. Watu wanapokufa, mwili wao unageuka na kuwa "mavumbi" na "roho ("pumzi ya uhai") humrudia Mungu aliyeitoa. Lakini, je! kunatokea nini kwa ile roho hai (living soul)?
Mungu anapoiondoa kwetu pumzi yake ya uhai aliyotupa, roho yetu hufa. Lakini kama tutakavyoona baadaye katika somo hili, tukiwa na Kristo tumaini liko.
Kaka Pasco na mshana jr, mnaweza kutufungulia mjadala????
Asante..