Kwanini mama wake huangalia kucha?

Kwanini mama wake huangalia kucha?

Hujawahi sikia msemo huu " huyu jamaa aliangukiwa na kitovu", wanawake mna mambo sana. Kwa hiyo Wamama huwa wanawahi kitovu kisiangukie kunako ..... Hizo ndio za wanawake, hata wewe walikuangalia kucha !!!!!

mh mkuu naskiaga hafu kikimdondokea mtoto wa kiume anakuwa si riziki mtaani kuna watu wa aina hyo aise inatisha na inaogopesha
 
Mama wakwe wengi kutoka makabila mengi kama siyo yote hapa Tanzania wana tabia ya kuangalia watoto wachanga wanapozaliwa viungo vyake vya mwili kama kucha, vidole, miguu, mikono nk, Lakini huwa wanaangalia zaidi kucha na vidole vya miguu na mikono kuliko viungo vingine. Mama wakwe hawa ni wamama wa mume wa mtu. Nilijaribu kuwauliza baadhi yao lkn hawakunipa majibu ila wanasifia tu mtoto ni mzuri, mwenye kujua siri hii tafadhali atujuze ili tuelimike wote, Asante

Hata wewe siku mtoto wako akikuletea mjuu utamwangalia vizuri, na sehemu za kumwangalia ni hizo unazoambiwa. Moja ya kazi ya DNA test ni kuondoa utata wa mambo kama haya.

Mjukuu wako kazaliwa na vimacho kama vya akina Hwang ho,hutadadisi? kama kwenye ukoo wenu hamna aina hiyo ya macho? Mjukuu kaja na pua kama ya Churchil,hutatafuta kaitoa wapi?

Sitetei hivyo vituko vya Wamama, ndio maana nimekupa na vingine zaidi, sisi bado ni Waswahili, kuachana na Uswahili itachukua muda sana.
 
Alaaa kumbeee! nashukuru Mkuu kwa taarifa
 
Back
Top Bottom