Kwanini Makonda asifunguliwe kesi ya msingi Mahakamani?

Hivi unawezaje kuficha maovu yako ndani ya maovu ya mwingine?.....

Kama nyie vijana ndio mnapewa madaraka kumsaidia mkuu kuendesha nchi Basi tuna safari ndefu sana ......

Political mentality za kijinga always....
 
Hadi sasa watu wanalalamika kwanini Lema ashitakiwe kwa kumkelele Raisi ambaye kimsingi nI kiongozi wa dola ya utawala na Mke wa Lema ana kesi ya kumtukana RC Gambo.

Makonda na Mnyeti wanakabiliwa na tuhuma za kudhalilisha bunge.

Ikumbukwe Lissu alishawahi kutamka ya kuwa Majaji hawana akili.

Kwa msingi ule ule wa wivu wa mihimili ya dola,mahakama,bunge na korti kila mhimilI ukiamua kuwa na wivu je Lema,mkewe na wenzie watapona?

Jenga hoja bila matusi tafadhali.
Penye red si kweli! Lisu hawezi kusema hivyo asilani! Tafuta clips utajihakikishia alichokisema
 
Hoja hujengwa juu ya hoja, sasa unapotushauri tujenge hoja juu ya kioja, tukueleweje?
 
Tuseme kwa mfano kutaja list ya mafisadi ni kosa-je hii inahalalisha wengine kufanya kosa hilo, hasa ukikumbuka kuwa vyombo vya dola wanavyo? Pia ukumbuke sio wote wanaweza kwenda mahakani. Kama sheria ziko wazi basi Makonda awe wa kwanza kuzifuata!!!!
Makonda hajakiuka sheria yoyote mpaka sasa.Nashangaa tu watu povu linawatoka.si nyie mliokuwa mnapiga kelele serikali ichukue hatua?kuitwa polisi sio kosa
 
Makonda hajakiuka sheria yoyote mpaka sasa.Nashangaa tu watu povu linawatoka.si nyie mliokuwa mnapiga kelele serikali ichukue hatua?kuitwa polisi sio kosa
RC HANA nguvu yyt kisheria kumuita mtu polisi ktk tuhuma za jinai
Mbowe kafungua kesi leo Mahakama ya Katiba na Makonda atanyooshwa
 
Lema amefanyiwa siasa chafu na fitina!
Makonda anafanya siasa chafu na fitina..
Lema na Makonda ni watu wawili tofauti!
Lema ni kiongozi aliyechaguliwa na wananchi na hao wananchi ndio wenye haki ya kumwajibisha kulingana na mwenendo wake!
Makonda kaliaibisha bunge mamlaka husika zimwajibishe...
 
Lema yule ni mbunge wa kuteuliwa na wananchi Makonda ni mkuu wa mkoa wa kuteuliwa na rais. Lema anawananchi zaidi ya 90.000 nyuma yake.
 
RC HANA nguvu yyt kisheria kumuita mtu polisi ktk tuhuma za jinai
Mbowe kafungua kesi leo Mahakama ya Katiba na Makonda atanyooshwa
Kama RC ana uwezo wa kumuweka mtu ndani saa 48,atakosa wapi uwezo wa kumuita mtu polisi?
Haya Mbowe kaitwa na kamanda Siro,atakwenda haendi?Kutumia nguvu nyiingi hivo ni kuogopa polisi au kuna kitu anaficha?
 
Mkuu Tafadhali Naomba Unipe Hiko Kifungu Cha Sheria Kinampa Makonda Madaraka Kuita Watu Polisi Tafadhali!

Bila Shaka Kamanda Siro Anajua Sheria Inamtaka Afanye Nini Ikiwa Anamuhitaji Mbowe Kwa Mahojiano, Central Polisi.

Sina Shaka Kabisa Na Weledi Wa Kamanda Siro Kuwa Atatumia Utaratibu Maalum Uliopo Kumuita Mbowe

Lakini Kwa Nini Tusihoji Mahakamani Ni Kifungu Gani Kinachompa Mamlaka Paul Makonda?
 
Mleta hoja uko sahihi 100% na maswali yako sidhani kama yatajibika. Tatizo ni kwamba tumeshaweka "common sense" pembeni kwa sasa, tunatumia zaidi "common shit". Kwa hiyo hata ukiuliza maswali ya msingi utaambulia embarrassment.
 
Kama RC ana uwezo wa kumuweka mtu ndani saa 48,atakosa wapi uwezo wa kumuita mtu polisi?
Haya Mbowe kaitwa na kamanda Siro,atakwenda haendi?Kutumia nguvu nyiingi hivo ni kuogopa polisi au kuna kitu anaficha?
Anaweza kumuweka mtu ndani kama 'ata hatarisha amani' within his/her juristication
Hana uwezo wa kuniweka mm mahabusu masaa 48 kama nimetenda jinai
Tuhuma za jinai kama hizi za madawa ya kulevya ni kazi ya Polisi na Mahakama tu
RC hana nguvu kuingilia kesi yyt ile ya jinai!
 
Back
Top Bottom