EWGM's
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 1,521
- 2,112
Nimefatilia Hili Saga La Bwana Mkubwa Makonda Kwa Muda Sasa Na Kila Kukicha Mambo Mapya Yanaibuka Kuhusu Yeye. Paul Makonda Ana Nia Safi Ya Kulisafisha Jiji Kuhusiana Na Madawa Ya Kulevya Lakini Taratibu Na Njia Sahihi Lazima Zifuatwe.
Amesema Anatumia Vyombo Vya Habari Ili Hata Mtoto Mdogo Wa Shule Msingi Ajue Kuwa Madawa Ya Kulevya Ni Hatari Na Wahusika Wake. Hivyo Wajiepushe Nayo Kwani Na Wao Wakishiriki Kwa Namna Moja Au Nyingine Wajue Hathari Zake Ikiwemo Kutajwa Hadharani.
Kwakusema Hivyo Ina Maana Aliowataja Kwenye Vyombo Vya Habari Kwa Namna Moja Au Nyingine Wanahusika Na Madawa Ya Kulevya. Hapo Juu Nimenukuhu Moja Ya Sababu Alizosema Makonda Kwanini Ametaja Majina Hadharani. Lakini Kwenye Kutaja Watu Lazima Uwe Na Ushahidi Na Uhakika Wa Uhusika Wao Mbadala Na Kutoa Kauli Mbili Zinazokinzana.
Pia Akaja Kusema "Aliowaita" Wakutane Na Wewe Pale Central Polisi Kwa Kamanda Siro Ili Mzungumze. Sasa Bwana Mkubwa Makonda Hapa Ndipo Ninapopata Kujiuliza Maswali. Kama Uliowaita Wanahusika Na Madawa Ya Kulevya Na Kuwatangaza Hadharani, Kwanini Usikabidhi Majina Yao Kwa IGP Au Kamanda Siro Ili Karatibu Za Kipolisi Zifuatwe, Na Mwisho Sheria Ichukue Mkondo Wake?
La Pili Kwanini Unataoa Kauli Zinazokinzana Kuhusiana Na Majina Unayoyataja? Kwa Mfano Umesema Umewataja Ili Hata Watoto Wa Shule (Jamii) Ijue Uhusika Wao Na Hapo Hapo Unasema Umewaita Ili Watoe Ushirikiano Na Kujua Ukweli Kutoka Upande Wao Kwa Shutuma Za Madawa Ya Kulevya?
Kimsingi Sitapenda Kuongelea Hadhi, Nyadhifa, Majina Yao Au Umuhimu Wa Majina Yao Kwa Jamii Na Kwa Familia Zao Sababu Haya Waziri Nape Aliyaelezea Kwa Ufasaha Kabisa Na Pia Havitazuia Uhalifu Wao Kama Kweli Walitenda.
Kwenye Hitimisho Ambako Kuna Hoja yangu Na Swali La Msingi Ni Kuwa Nchi Hii Inaendeshwa Kwa Kufuata Katiba, Kanuni na Sheria Za Nchi. Pia Hakuna Aliyejuu Ya Sheria na Katiba Za Nchi Na Hata Ukiwa Na Madaraka Kuna Maadili Na Kanuni Za Uongozi Lazima Zifuatwe Ili Kukuwezesha Kiongozi Kuheshimu Katiba, Sheria Na Kanuni Za Nchi Tulizojiwekea.
Tanganyika Law Society, Amnesty International, Tanzania & Zanzibar Human Rights Watch, Wanasheria Wa Kujitolea Kwa Wamekuwa Kimya Sana Kwenye Hili Swali La Msingi:
'Ni Kwa Mamlaka Yapi Na Kifungu Kipi Cha Sheria Kinachokumpa Ruhusa Mkuu Wa Mkoa Aite Watu Polisi Kutumia Vyombo Vya Habari? '