Kwanini majina ya mwisho/ukoo huwa maarufu sana kuliko majina ya mwanzo?

kiafrikaafrika yanaonesha heshima mbele ya jamii hasa ikiwa jina lako la mwanzo linatumiwa na wengi ikiwemo watoto. mf John, Ally. 'rais John anahutubia' wengi watakuona huna adabu kwa mila zetu ila Arabs hutumia majina ya mwanzo. pili ni majina ya upekee ambayo yakitumika ni rahisi lengwa kutambulika.
rais Peter kawasili-hii italeta maswali ni Peter gani?
rais Mkurunzinza Kawasili-kauli hailet maulizo inajitegemea.
JIU;IZE KWANINI WAZAZI WENGI HAWAPENDI WATOTO WAO WAJUWE MAJINA YAO YA MWANZO HADI WAWE WAKUBWA. Utasikia mama B na sio jina lake la Amina
 
Jina la kwanza, la kwako, la pili la baba na la tatu la babu au ukoo. Babu au ukoo umedumu mda mrefu kuliko la kwanza au pili. Hivyo chenye mda mrefu kinajulikana zaidi
 
Kwasababu ni majina ambayo ni very unique hivyo ni rahisi kumtambua mtu kupitia jina hilo mfano haya majina ya kizungu katika kikundi cha watu mnaweza jikuta hata watu watatu mnatumia jina moja hivyo inakua vigumu kuwatofautisha.
 
majina ya ukoo yapo kipekee na ni rahisi kushikika mfano nikija kiijini kwenu nikakuuliza kwa jina la kwanza naweza nisikupate coz wapo wengi wenye jina kama lako. lakini nikikuulizia kwa jina la ukoo ni rahisi sana watasema tu ukoo wa fulani huyu. na hayo ndio majina yetu halisi ya kibantu. tofauti na majina ya kwanza mengi ni ya kigeni.
 
Heshima kwenu wana jf,

Jamani wajuzi naomba kujua
Hivi ni kwanini majina ya mwisho ya ukoo hutambulika au kuwa maarufu zaidi kuliko jina la kwanza?

Mfano Jakaya Mrisho Kikwete linalojulikana sana ni Kikwete?
John Pombe Magufuli jina maarufu ni Magufuli,
Julius Kambarage Nyerere jina maarufu ni Nyerere

Naomba kujua iko hii, wana jf naomba kujua

Kwa maoni yangu ni hivi, Sisi tumetawaliwa na Waingereza na ndio maana tumeathirika na utumiaji wa majina ya babu zaidi, Ila kwa wazenji, wao hutumia jina la mwanzo tu Ila kiserikali ndio hutumika la babu kutokana nao pia walitawaliwa na Uingereza.
Wazungu hufata kutokana na makabila (nchi ) zao, mfano Wahispania hawatumii sana jina la ukoo, hutumia majina yao ( nao kama wazenji , kiserikali hutumika zaidi jina la ukoo).
Waingereza ndio walikuwa wababe enzi hizo, na baadae wakaja wamarekani ambao nao ni koloni pia la Uingereza wakasambaza matumizi ya hicho kitu.
Lakini kwa kikawaida kila nchi / jamii inafuata taratibu zake.
 
Majina ya Paul, Omar na mengine ya aina hiyo yameingia Afrika na walioleta dini barani humu, majina kama kawambwa, Kimweri, Banzi nk yanapata mvuto maana ndiyo majina halisi ya Kiafrika
 
Majina ya Paul, Omar na mengine ya aina hiyo yameingia Afrika na walioleta dini barani humu, majina kama kawambwa, Kimweri, Banzi nk yanapata mvuto maana ndiyo majina halisi ya Kiafrika
Asante mkuu agiza coca kama zote hiv maake umenifunza kitu
 
Kwa maoni yangu ni hivi, Sisi tumetawaliwa na Waingereza na ndio maana tumeathirika na utumiaji wa majina ya babu zaidi, Ila kwa wazenji, wao hutumia jina la mwanzo tu Ila kiserikali ndio hutumika la babu kutokana nao pia walitawaliwa na Uingereza.
Wazungu hufata kutokana na makabila (nchi ) zao, mfano Wahispania hawatumii sana jina la ukoo, hutumia majina yao ( nao kama wazenji , kiserikali hutumika zaidi jina la ukoo).
Waingereza ndio walikuwa wababe enzi hizo, na baadae wakaja wamarekani ambao nao ni koloni pia la Uingereza wakasambaza matumizi ya hicho kitu.
Lakini kwa kikawaida kila nchi / jamii inafuata taratibu zake.
Asee watu mnamajibu mazuri sana mkuu pongez sana kiongoz kwa ufafanuzi unaoeleweka vizuri
 
Ridhiwan kikwete kwanini sio Ridhiwan mrisho?! Make baba yake in jakaya babu yake ni mrisho. Afu huyu mh jina lake la kwanza ndo maarufu
 
Heshima kwenu wana jf,

Jamani wajuzi naomba kujua
Hivi ni kwanini majina ya mwisho ya ukoo hutambulika au kuwa maarufu zaidi kuliko jina la kwanza?

Mfano Jakaya Mrisho Kikwete linalojulikana sana ni Kikwete?
John Pombe Magufuli jina maarufu ni Magufuli,
Julius Kambarage Nyerere jina maarufu ni Nyerere

Naomba kujua iko hii, wana jf naomba kujua
Nijuavyo mimi, jina la tatu ni jina la ukoo ambalo ni jina la baba yake na baba yako, yaani jina la babu ambalo unakuja kuitwa na kulitumia wewe, ndiyo jina lako unalolitumia na kueleweka sana tangia utotoni.

Mfano wewe unafahamika sana kama Masanja.

Majina yako kamili ni Abert Abrahamu Masanja.

Jina lako la ubatizo ni Abert, baba yako anaitwa Abraham, babu yako anaitwa Masanja.

Sasa tukija kwenye mchanganuo wa majina yanayofahamika sana kwa hawa watu watatu ie: mtoto, baba na babu katika mabano.

Yaani mtoto: Abert Abrahamu (Masanja).

Baba: Abrahamu Masanja (Abert).

Babu: Masanja Abert (Abrahamu).

Kama nimebugi ninaomba kusahihishwa.
 
Ridhiwan kikwete kwanini sio Ridhiwan mrisho?! Make baba yake in jakaya babu yake ni mrisho. Afu huyu mh jina lake la kwanza ndo maarufu
Hilo jina limetengenezwa kutokana na umaarufu wa baba'ke mzazi.
Kikawaida anatakiwa aitwe Ridhiwani Jakaya Mrisho.
 
Back
Top Bottom