Kwanini majina ya mwisho/ukoo huwa maarufu sana kuliko majina ya mwanzo?

Miaka ya nyuma kuna mzee mmoja kutoka ukoo wetu aliwahi kuhudumu katika jeshi ila alikuwa na ukatili wa ajabu sana jina lake halikutoka masikio mwa wahanga wake hadi sasa kuna baadhi ya watoto walipata taabu kupitia jina lake.

Faida ni kuwa ukilitumia kwa mazuri litakuwa na manufaa hata kwa vizazi vijavyo.

Ila ukilitumia vibaya unaharibu sana kwa wajao.
Asante mkuu nimekusoma vilivyo
 
Heshima kwenu wana jf, jamani wajuzi naomba kujua ivi ni kwanini majina ya mwisho kutambulika au kuwa maarufu kuliko jina la kwanza? Mfano jakaya mrisho kikwete linalo julikana sana ni kikwete?,John pombe magufuli jina maarufu ni Magufuli, julius kambarage Nyerere jina maarufu ni Nyerere naomba kujua iko hii, wana jf naomba kujua
1. Wakati wa kulitamka msikilizaji huona hamna haja ya kushika ya mwanzo au husikia zaidi la mwisho

2. Wenye majina huwamiss/ huvutiwa na mababu zao maana wengi wao mababu huwa ni wakagis au watu wenye nyadhifa au kujulikana mfano
Chief nyerere
 
Naona kuna ukweli ndani ya ulichokisema
 
Surnames nafikiri zilianza Uingereza haswa mashuleni huo utamaduni ulianza zamani na wanakuwa nao.
Kwenye michezo kwa mfano mipira utaona wachezaji wote wanaitwa kwa majina ya mwisho.
Na wanasiasa pia

Lakini utaulizwa unapendelea kuitwa kwa jina gani ukisema la kwanza sawa au la mwisho ni sawa tu

Na sisi naona tumeiga kama baadhi ya wamawake kujiita ubini wa waume zao
 
Asante mkuu kwa ufafanuzi makini
 
Majina ya mwisho yako unique lkn pia watu wengi hupenda kuitwa hvyo hususani kwenye umri mkubwa, na kumbuka kule kwetu mtoto mdogo anakatazwa kabisa kumuita mkubwa kwa jina lake la kwanza, lkn la mwisho halina shida
 
Sawa mkuu nimekupata
 
Kwa uelewa wangu nadhan ni kwa ajili ya upekee wake tofauti na ilivyo kwa majina ya mwanzo na yakati yanakua yanajirudia rudia hvyo hufanya utambulisho kuwa na utata kwa mfano John wapo wengi na aitoshi kukamilisha utambulisho wa mtu ila ukitumia jina la mwsho mfano Lissu, inaeleweka haraka zaid
 
Sawa mkuu
 
Heshima kwenu wana jf,

Jamani wajuzi naomba kujua
Hivi ni kwanini majina ya mwisho ya ukoo hutambulika au kuwa maarufu zaidi kuliko jina la kwanza?

Mfano Jakaya Mrisho Kikwete linalojulikana sana ni Kikwete?
John Pombe Magufuli jina maarufu ni Magufuli,
Julius Kambarage Nyerere jina maarufu ni Nyerere

Naomba kujua iko hii, wana jf naomba kujua
Jina la ukoo inakua kama Tittle ya jumla na linatumika na wengi. Kwa mfano wewe canular ndio liwe jina la ukoo inamaana hata mwanao na mjukuu na kitukuu na kilembwe watalitumia hilo hilo kama ambavyo wewe umetumia kutoka kwa baba, babu na babu wa mababu

Sasa jina la ukoo waweza kum adress mtu bila hata kuweka Title nyingine ya heshima tofauti na unavyomuita mtu kwa specific jina lake au jina la kwanza. Mfano waweza kumuita mtu Mapunda, au Magufuli bila kuweka Mr au Bwana au Mzee na isiewe na ukakasi sana tofauti na kumuita mtu John lazima utangulize na Cheo kama Mzee, Mheshimiwa , Mkuu,Mr n.k
 
Ni utamaduni tu uliozoeleka ambapo ukifikia umri fulani watu huanza kukuita jina lako la Ukoo.

Hivi wazanzibar wana majina ya Ukoo maana utasikia mtu anaitwa Ahmed Salim Hussein.
 
Jina la ukoo inakua kama Tittle ya jumla na linatumika na wengi. Kwa mfano wewe canular ndio liwe jina la ukoo inamaana hata mwanao na mjukuu na kitukuu na kilembwe watalitumia hilo hilo kama ambavyo wewe umetumia kutoka kwa baba, babu na babu wa mababu

Sasa jina la ukoo waweza kum adress mtu bila hata kuweka Title nyingine ya heshima tofauti na unavyomuita mtu kwa specific jina lake au jina la kwanza. Mfano waweza kumuita mtu Mapunda, au Magufuli bila kuweka Mr au Bwana au Mzee na isiewe na ukakasi sana tofauti na kumuita mtu John lazima utangulize na Cheo kama Mzee, Mheshimiwa , Mkuu,Mr n.k
Asante sana mkuu kwa ufafanuzi mzuri
 
Back
Top Bottom