Kwanini mahusiano/ndoa nyingi hazidumu?

Kweli kabisa elimu juu ya ufahamu wa ndoa yenyewe na yaliyopo katika ndoa bado inahitajika kwani kwa miaka ya sasa hivi watu wanaingia kwenye ndoa kwa matarajio ya kukuta vitu fulani ambapo mwisho wa siku wakiingia wanakuta ni kinyume chake hivyo kuzifanya zisiwe zenye kudumu.
 
mkuu naomba uje uongelee hili swala kwa undani .. hayo mengine yatafuata ... tukiweza hapo mengine nadhani yatakuwa mepesi.. asante sana mtani barikiwa sikukuu njema
 
hizi POINTS nimezipenda sana

>UONGO & USIRI
>ELIMU FINYU YA NDOA
>FIRKA HASI

hizo ndio ugonjwa mkuu unaoshambulia hadi Ini la Ndoa..

Yaani tena hizo mbili.. ya juu na ya chini sio ndoa tu hata Urafiki wa kawaida haudumu kabisa kila siku utakuwa unabadilisha marafiki
 
mkuu huwa hukoseagi...nimejifunza kitu apa kwass ambao bado tunatangatanga na dunia...
 
mwanamke au mwanaume kuendelea kimapenzi na mtu ambae ameanza nae muda mrefu lakini mwisho wa siku asimuoe!akaendelea nae ijapokuwa ana ndoa au wote wako katika ndoa!kutoachana na X ndio chanzo kikubwa cha kuvuruga ndoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…