ng'adi lawi
JF-Expert Member
- Sep 27, 2014
- 2,956
- 1,114
Hivi karibuni tuliambiwa kuwa mahakama mpya ya mafisadi haina kesi za kutosha zilizofunguliwa hapo. Hivi kwa nini watuhumiwa wote wa kashfa zote zilizojadiliwa bungeni kuanzia EPA, Richmond, Meremeta, Tangold, Jairo, Radar na Escrow hawapelekwi huko? Ni ushahidi hautoshi au serikali inaogopa watu fulani? Ni vema wahusika wapelekwe huko ili kuonyesha nia thabiti ya serikali kupiga vita ufisadi. Ni heri washinde kesi kuliko kutopelekwa kabisa. Vinginevyo hakukuwa na haja ya kuwa na mahakama hiyo.