Kwanini magonjwa ya figo, ini pamoja na mapafu yanaondoa vijana wengi sana?

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Zamani ilionekana UKIMWI ni tishio kwa Dunia nzima, kwa dhana kwamba ni lazima mtu atakufa tu.

Siku hizi magonjwa ya ini, mapafu kujaa maji, Figo kushindwa kazi yake yamekuwa tishio sana na yanaondoa uhai wa watu wengi sana hasa vijana.

Sijui sababu kubwa ni matumizi ya pombe au sigara bila kula vizuri, kunywa maji mengi n.k?

Lakini mbona wazee wetu wanakunywa pombe miaka nenda rudi lakini hawasumbuliwi na magonjwa haya kama vijana wa leo?

Madaktari wameshindwa kabisa kuthibiti vifo vya magonjwa haya kiasi kwamba mtu akishaumwa tu haya magonjwa anahesabu kifo wakati wowote.

Kwanini yameshindikana?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Wengi issue ni NGOMA, figo ni geresha tu. Mara nyingi ni ngoma ndiyo huwaua, ukiwa na ngoma ni rahisi mno magonjwa kama ya figo, ini, moyo, BP, cancer aina zote ikiwemo ya koo, kisukari n.k, kukupata na kukuondosha kabisa duniani.

Issue ni kuwa wengi wa hao vijana wanauawa na UKIMWI ambao kwa kiasi kikubwa huwasababishia hayo magonjwa uliyotaja.

Tuache ngono zembe, AIDS is real!!!
 
Pombe na sigara kupitiliza ,,pia kuna hizi sumu tunakula kila siku kama sukari especially ya kwenye bidhaa za viwandani kama juice, soda,pipi nk. Mafuta ya kupikia yanayotokana na mbegu ni hatari sana lakini ukijumkisha na madawa yanayopigwa kwenye mazao,mboga basi ni kama tunakula sumu inayotuua taratibu .
 
Wengi hufa na NGOMA, figo sijui ini ni geresha tu.
 
Wengi issue ni NGOMA, figo ni geresha tu. Mara nyingi ni ngoma ndiyo huwaua, ukiwa na ngoma ni rahisi mno magonjwa kama ya figo, ini, moyo, BP, cancer aina zote ikiwemo ya koo, kisukari n.k, kukupata na kukuondosha kabisa duniani.
Issue ni kuwa wengi wa hao vijana wanauawa na UKIMWI ambao kwa kiasi kikubwa huwasababishia hayo magonjwa uliyotaja.

Tuache ngono zembe, AIDS is real!!!
Watu wanatumia dawa za kuongeza kufubaza makali ya HIV virus.
 
Ngoma ndio inaondoa watu, vile tu ngoma sio ugonjwa bali ni hali...

Ndio maana yanatajwa magonjwa nyemelezi ambayo hutoa uhai wa wahusika...

Ukiacha hilo, matumizi makubwa ya pombe na vilevi vingine ambavyo kwa kiasi kikubwa ni chanzo cha magonjwa yasiyoambukizwa
 
Back
Top Bottom