Kwanini magari mapya kwetu yana umri mkubwa?

Kwanini magari mapya kwetu yana umri mkubwa?

kALEnga kidamali

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2015
Posts
542
Reaction score
753
Kwa sasa imekuwa ni rahisi kujua ukukuu wa gari kwa kuangalia namba za usajiri, ukiona namba AAA basi hiyo ni imetumika sana tofauti na ile yenye namba DDD, hata madalali wamekuwa wakimshawishi mteja kwa kigezo hicho lakini hata Bei pia imekuwa mara nyingi ikipangwa kulingana na hizo namba za usajiri (hapa kwa gari uses zilizosajiriwa nchini).

Sasa katika utafiti wangu kwa kipindi cha hivi karibuni nimegundua kuwa hizi gari tunazoziona zinang'ara tena namba D kiukweli umri wake mara nyingine huwa ni mkubwa yaani production yake unaweza kuta kuta ni miaka zaidi 15 au 20 iliyopita. Pia nimeshangazwa kuona hata baadhi ya brand nyingine ambazo hapa nchini ndio kama fashion kumbe ni za miaka mingi iliyopita huko kwa mabeberu.

Je hali hiyo imechangiwa na nini? na ni kwann haya magari tunayoyaona ya kisasa baadhi huwa yameshapitwa na wakati kwa mabeberu?
 
Simple tu. Wabongo tunaweza ku afford magari ya bei rahisi. Magari ya zamani ni cheap sshv kwetu sabab huko nje washayatumia na kununua mapya. Rav4 LE ya 2019 nje zinauzwa $26,500 (kama 61.5M za huku), na hyo ni kabla hujapigwa kodi ya kuimport na bado hujalisafirisha. Ssa unafikiri ni watu wangap hapa bongo wanaweza kununua gari la bei hyo? 2019 Toyota Camry USA inauzwa kma $25,000 (ni 59.2 M za bongo) hapo nayo bila kusafirisha, bila kodi. Wakat Camry new model zilizopo bongo ni za 2010 zinazouzwa mpk 20M ambazo watu wengi wanaona ni bei kubwa. Kwa hali hyo unategemea tutakua na latest models huku bongo ukiangalia na hali ya uchumi yetu

Na hyo mifano niliyokupa ni ya magari ambayo nje wana consider kma ni bei rahisi au bei ya kawaida. Hujaja kwenye ma Land Cruiser V8 zinazoanza $80,000 kuendelea mpk $120,000 (185M to 278M)
 
Asilimia nyingi ya gari unazoita mpya ni used huko zilikotoka.
Gari za 0-10KM mara nyingi ni serikali na taasisi zake ndo wanaagiza na wenye uwezo wachache, the rest zishatembea sana huko mbele kabla ya kuja bongo
 
Kodi kubwa zinachangia, Toyota alphard 2018 kodi peke yake 53milioni hapo hujaweka gharama ya kununua na kusafirisha
 
Back
Top Bottom