Lituye
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 1,862
- 5,680
Katika nchi nyingi za kiafrika ambazo watu wanauawa hovyo, kutekwa, majanga kama mafuriko, wakulima hawana masoko wafanyakazi mishahara duni biashara kudorola halafu unakuta Television ya taifa hilo kila uchao linapiga nyimbo za kumsifia rais.
Nchi hizi hutegemea fedha za Mabeberu ktk kukopa na wananchi ndio wanalipa madeni hayo yenye riba kubwa. Lakini wakipata pesa kutoka kwa Mabeberu utasikia eti Rais katoa pesa kujenga barabara. Pesa wametoa Mabeberu kwa mkopo halafu yana jitukuza eti ni Rais katoa wakati yeye mwenyewe analipwa mshara na malupulupu na wananchi wanyonge wa nchi hizo. Kwa nini madikteta hupenda sana kusifiwa?
Madikteta hupenda kujionesha yako jirani na watu na yanapendwa. Utayaona yanaigiza kula chakula au kunywa chai wakiwa na watu na wakiwa wanakula lazima tukio hilo litangazwe ili watu waone kuwa Dikteta amekula na watu au amekunywa chai na watu.
Kule Kenya nakumbuka Rais Moi vyombo vya habari vilikuwa vikimuita Mtukufu Rais Daniel Araph Moi. Nyimbo katika radio zilikuwa zinamsifia yeye na KANU tu. Kumbe watu huku wakimuimbia nyimbo za sifa Moyoni wanamng'ong'a hiloo linapenda sifa.
Leo KANU ya Moi iliyokuwa ikisifiwa na kutukuzwa tunajua ilipo.
Maendeleo hayana vyama.
Sent using Jamii Forums mobile app